Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu 42 wakituhumiwa kuhusika na mlipuko uliotokea juzi usiku katika nyumba ya Kamishna wa Polisi, Hamdan Omar Makame.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.
“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.
=====================
Chanzo: Mwananchi
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo.
“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.
=====================
Zanzibar. Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watu 42 wakituhumiwa kuhusika na mlipuko uliotokea juzi usiku katika nyumba ya Kamishna wa Polisi, Hamdan Omar Makame.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya polisi Ziwani, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi unaendelea na bado watu wengine wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo. “Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Mkadam.
Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga aliyewasili jana Zanzibar, alithibitisha kukamatwa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamad Masoud. Kitwanga hakubainisha mambo ambayo yamesababisha kukamatwa na kuhojiwa kwa Masoud.
Kukamatwa kwake kumekuja baada ya ofisa huyo wa CUF, Jumatatu iliyopita kuongea na waandishi wa habari na kueleza kwamba hali ya kiusalama ni mbaya na haki za binadamu zinavunjwa hasa Pemba ambapo alilishutumu Jeshi la Polisi kwa kupeleka silaha nzito na idadi kubwa ya askari wanaorandaranda mitaani na kuwabughudhi wananchi.
Alisema kutokana na madhila hayo baadhi ya wananchi waliamua kukimbilia misituni na wengine kuanza kuhamia Mombasa, Kenya kunusuru maisha yao kama ilivyotokea mwaka 2001.
Akielezea kuhusu hali ya usalama kisiwani Pemba, Kitwanga alisema habari kuhusu Pemba hazina ukweli wowote kwa kuwa kuna watu wanatoa taarifa ambazo siyo sahihi kulingana na uhalisia wenyewe.
“Hali ya Pemba ni shwari na pia nataka kusisitiza nikiwa Waziri wa Mambo ya Ndani sijapata taarifa yoyote rasmi kama kuna watu wanakimbilia nchi jirani. Lakini hata hilo la watu kukimbilia msituni inabidi tujiulize Pemba kuna msitu mkubwa wa watu kwenda kujificha? Haya mambo ni ya kuzusha, watu waende wakajionee wenyewe,” alisema Kitwanga.
Alisema hakuna dalili yoyote ya watu wanaokimbia kutoka Zanzibar kukimbilia Tanzania Bara kutokana na idadi ya wasafiri kati ya Bara na Zanzibar kuwa ya kawaida.
Alisema kama kuna ongezeko lolote basi ni kutokana na sherehe za Pasaka kukaribia na si suala la kuogopa uchaguzi kama inavyoelezwa.
Waziri Kitwanga alisema yupo hapa Zanzibar ili kuhakikisha maandalizi yote ya uchaguzi wa marudio Jumapili unafanyika kama ulivyopangwa.
“Vitisho vinavyoendelea tulivitegemea, tunajua kama kuna watu hawataki uchaguzi na wanatumia mbinu mbalimbali ikiwamo ya milipuko kutisha watu. Wito wangu kwa watu wanaotaka kupiga kura wajitokeze kwa wingi na usalama wao upo,” alisema waziri huyo.
Chanzo: Mwananchi