Watu 20 wafa ajalini Busega

Ni kwa Neema za Mungu tu, tunaishi. Tumrejee Yeye kwa maana hatujui siku wala saa...!
 
nimesikia startv muda si mrefu taarifa yao ya habari wamesema walifikwa na mauti katika ajali hiyo ni watu 12 tu, ni yupi tumwamini na ukweli ni upi
 
Walazwe mahali panapostahili..........amina.
 

Nimepoteza shangazi yangu kwn ajali hiyo, R.I.P my lovely Aunt
 
Tutaendelea kusema hivi mpaka lini? Tuchukue hatua za kuwawajibisha kama wameshindwa kuwajibika tusione ajali kitu cha kawaida!
Htaujaona ajali ni kitu cha kawaida bali wakati mwingine abiria tunachangia sehemu kubwa kwa sababu unaweza kumwambia dereva apunguze mwendo na abiria wengine wakakugeuka kuwa unawachelewesha, mimi imewahi nitokea nilipanda gari moja hivi dereva alikua anendesha kwa kasi nilimuonya lakini abiria wengine walinijia juu na kusema nawachelewesha isitoshe baadhi ya siti zilikua hazina mkanda ikiwepo yangu kuna Trafiki alisimamisha maeneo ya morogoro akasema abiria kuna tatizo mimi nikamwambia ndio dereva anatembea mwendo mbovu na pia kuna baadhi ya siti hatuna mikanda cha kushangaza abiria walinikalipia na kuonesha ile mikanda mibovu kama ndiyo mizima, baadae trafiki ilibidi akubaliane na wengi gari ikaruhusiwa tukaondoka, hapo utamlaumu dereva? hata sisi abiria tuanze kubadilika tena sana!
 
 
Jamani tunawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu na kuomba wale waliojeruhiwa kupona haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…