Watu 10 Mashuhuri waliouawa kwa kupigwa Risasi

Watu 10 Mashuhuri waliouawa kwa kupigwa Risasi

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,636
Reaction score
112,470
1-JOHN F KENNEDY
Alikua raisi wa 35 wa marekani, aliuwawa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne katika historia ya marekani kwa kupigwa risasi. Akiwa na mkewe katika gari la wazi akitokea kwenye hotuba, alipigwa risasi tatu. Mpaka leo hauna jibu la moja kwa moja kuwa nani alimuua John F Kennedy. Japokua Lee Harvey Oswald ndie alie husishwa na mauaji hayo. Lee Harvey Oswald nae aliuwawa na raia mmoja (Jack Ruby) siku mbili tu baadae alipokua akioelekwa rumande. Cha ajabu ni kwamba John Kennedy, Lee Oswald na Jack Ruby, wote wlifia katika hospital ya Parkland Memorial kwa nyakati tofauti.


2 -MARTIN LUTHER KING Jr
Anafahamika kwa harakati zake za kutetea usawa miongoni mwa waamerika weusi. Martin Luther King ambae alitumia dini ya ukristo kwa kutetea ukandamizaji kwa watu weusi, aliuwawa miaka mitatu baada ya mwana harakati mwingine Malcom X (yeye alitumia dini yake ya kiislam) kuuwawa mwaka 1965, wote waliuwawa wakiwa na umri wa miaka 39. Robert F Kennedy aliekua mdogo wa John F Kennedy na mgombea uraisi, alitoa hotuba kali kufuatia mauji ya Martin Luther King. Cha ajabu na kushangaza ni kwamba nae aliuwawa miezi michache baadae.

3- ABRAHAM LINCOLN
Alikua raisi wa 16 wa marekani, na ndie raisi wa marekani wa kwanza kuuwawa akiwa madarakani. Ali uwawa na Jonh Wilkes Booth mwaka 1865. John Wilkes Booth aliudhiwa na maamuzi ya Lincoln kutambua haki za watu weusi. Booth alimuua Lincoln kwenye maonyesho ya muziki. Booth nae aliuwawa siku mbili baadae baada ya kufanya jaribio la kutoroka na kushindikana.

4- BENAZIR BHUTTO
Alikua waziri mkuu wa 11 wa Pakistan na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa PPP. Alikua mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichangizwa na siasa zake safi za kidemokrasia. Aliuwawa December 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake ya land cruiser akitokea kwenye mkutano wa kampeni. Gari hilo lililokua na uwazi juu, lilikua na uwezo wa kuzuia risasi Lakini Bi Bhutto alisimama kuwapungia mkono wafuasi wake, ndipo alipo pigwa risasi na baadae mlipuko ulitokea na kuua watu wengine 20 katika eneo la tukio.

5- MAHATMA GANDHI
Pia alifahamika kwa jina la Muhandas Karamchand Gandhi. Ni maarufu kwa hotuba na kauli zake zinazo tumiwa hadi leo. Huyu ni kiongozi maarufu wa India ilio kua ikitawaliwa na Waingereza. Mahatma Gandhi alikua kiongozi wa kiroho na kisiasa alie uwawa tarehe 30 January 1948 na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu aliekua akiitwa Athuram Godse, alipokua akielekea kufanya ibada.

6- JOHN LENNON
Alikua mmoja kati ya vijana watanashati waliounda kundi la the Bittles lililo tambulika miaka ya 70 hadi 80. John Lennon alikua mmoja wa waanzilishi wa kundi la The Bittles lililo julikana Sana miaka hiyo, na alifariki December 8 mwaka 1980. Akiwa anaingia hotelini Lennon alisikia sauti ikimuita, na alipo geuka alipigwa risasi nne na kupoteza maisha. Baada ya mauaji hayo, muuaji Mark David Chapman aliiachia silaha na kukaa barabarani akisubiria akamatwe. Na baada ya kukamatwa, Mark David alihukumiwa jela kifungo cha maisha, na yupo jela hadi sasa.



7- MALCOM X
Kama ilivyokua kwa Luther King jr. Malcon X pia alikua mwanaharakati aliepigania haki za watu weusi. Alikua waziri kwa wakati huo, na aliuwawa mwaka 1965. Hii ilikua baada ya kuamua kuwa muislam wa kisuni na kuondoa uanachama wake katika chama cha National Islam. Watu wote walio husishwa na kifo chake walikua wanachama cha National Islam.

8- ROBERT .F. KENNEDY
Robert mdogo wa raisi wa marekani John Kennedy alie uwawa. Aliuwawa mwaka 1968, miaka mitao tu baada ya kaka yake kuuliwa. Ilikua ni miaka mitatu tu kupita tangu alipo uwawa mwanaharakati Malcon X, na miezi kadhaa baada ya kuuliwa mwanaharakati mwingine Martin Luther King jf. Huo ulikua ni mfululizo wa mauaji. Hata ikumbukwe Patrice Lumumba alie uwawa mwaka 1961 (miaka 7 kabla).

9- TUPAC OMAR SHAKUR
Jina hili sigeni kwa mtu yeyote mpenda muziki, hasa miondoko ya HipHop. Tupac aliepigwa risasi September 7 mwaka 1996, alipokua akitokea Las Vegas Nevada alipo kwenda kushuhudia pambani la Michael Tyson. Akiwa na meneja wake Suge Knight (ambae pia amekua akihusishwa na kifo hicho). Tupac alishambuliwa kwa risasi kadhaa zilizo toka kwenye gari moja nyeupe iliyo wazuia kwa pembeni. Tupac alifariki siku chache baadae katika hispitali ya University Medical Center of Southern Nevada. Wengi walihusishwa kwenye kifo cha Tupac huku idadi kubwa ikielekezwa kwa Christopher Wales (B.I.G) kuwa ndie alie husika moja kwa moja kwa katika mauaji ya Tupac. Baada ya miezi sita tangu kuuwawa kwa Tupac, Christopher Wales (B.I.G) aliuwawa na watu walio dhaniwa ni mashabiki wa Tupac.

10- JUVENAL HABYARIMANA
Aliuwawa baada ya ndege yake kushambuliwa na kuua watu wote walio kuwemo kwenye ndege hiyo, akiwemo Raisi wa wakati huo wa Burundi. Mauaji hayo ndio yaliyo chochea hasira za wanyarwanda hasa wahutu, na kuanzisha mauaji ya watutsi hali iliyo pelekea mauaji ya kimbari. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ufaransa, mauaji hayo yalifanywa na chama cha Rwanda Patriotic Front (RPC) na kumuhusisha Raisi wa sasa Paul Kagame, ingawa Kagame mwenyewe amekua akikemea vikali na huku akisema kwamba wafaransa wanajaribu tu kuficha maovu yao.
 
Duu kweli dunia mapito.na Lucky dube umemsahau kwenye list mkuu
 
Easy E.
Dady Kane
Rakim
Kadaff
Idd amin
Wote hao ni hip hop....


Marvin gaye alipigwa shaba na baba ake kwa tuhuma za ushoga.
 
Asante ushiboy. wakuu wengine mnasema Fulani hayupo ama kasahaulika ni vema nawe ukaandika ilitupate mfululizo wa watu hao kama alivyofanya mleta mada
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom