Watoza ushuru wa magari Mwenge wanaibia serikali

Crocozilla

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
469
335
Kuna kikundi cha vijana wako pale mwenge na wamejipa kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho pale mwenge kwa muda mrefu sasa. Ila cha kusikitisha ni kwamba wanafanya haya;

Wanadai pesa bila RISITI yoyote ile
Wanatoza pesa nyingi 500 hadi 1,000 kwa saa
Wanatumia ligha chafu yakiwepo matusi kwa wateja
Wanatumia vitisho ikiwepo kutishia kupasua taa/vioo
Wanatoza ushuru hadi usiku wa saa 3 kinyume na utaratibu wa serikali imbayo inamuda wa kazi
Hawaibia serikali pesa nyingi sana.

Hivyo kwa hali hii tunaviomba sana vyombo vyetu hivi muhimu vitusaidie kuokoa japo kilichosalia ili pesa itakayopatikana itumike kuboresha huduma. Vyombo hivi vitusaidie;
TRA
Polisi
Takukuru
Kuingilia kati kuhakikisha serikali inapata stahiki zake, wanatumia risiti na kuyafanyia kazi yote niliyosema hapo juu kwa faida ya wananchi. Wananchi wananyanyasika sana mwenge.

Nawasilisha
 
Hata mimi nimewaona,usipotoa hela upati parking na wanaweza kufanya lolotekwa gari yako
 
Back
Top Bottom