Watoto wote hawa wa nini?

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Posts
3,344
Reaction score
2,537
Wasalamu
Kuna binamu yangu yupo Dar jana alinipigia simu kunisalimia, hajaoa, ila ana miaka 33 sasa, na bado hajapata kazi lakini anaishi Dar, na amepanga, usiniulize anaishije kwani hata miye sijui.


Sasa jumla ya watoto wake ninaowajua kabla ya jana walikuwa ni 14 hawa amezaa na mabinti mbali mbali toka akiwa Sekondari huko mkoani Mara, Jana namuuliza hali ya watoto, si ndo ananiambia tena kuwa hadi sasa amefikisha 17, wa mwisho kuzaa naye ni mdada mmoja anafanya kazi tigo Dar, kwa kweli nilimgombeza sana, kwani kuna jambo aliniambia eti "Jiandae kunisaidia kusomesha" weeeeeeee!!! nilimtukana sana, na nikamwambia starehe zake zisinisumbe, kila mmoja abebe msalaba wake.

Sasa nikamwambia kwa nini asioe mmoja wapo? akasema hataki ana mwingine eti mkerewe! nikamwambia kila la kheri.

Sasa kwa nini starehe zako ziwape wengine shida? kuzaa uzae wewe, halafu mzigo uwape mwingine? sitakubali, kwani kila mmoja ana maisha yake na familia yake.
 
Huyo ni sperm donor maana hana sifa ya ubaba. Akihamia majuu atapata pesa nyinga sana maana itakuwa ajira kamili
 
Reactions: kui
Hahahahhaha duh huyu anafata nyao za Bob Marley hahahaha
 
Mwambie yeye sio BABA ni UBWABWA kutia mimba sio kazi kazi kulea,anahesabu watoto inaekea anaisikilizia sana utamu wake, mwambie akapime kwanza halafu ndio muongee ......
 
Mmmh! Hata kama ni kusaka nafasi Guiness Book of Records, sio kihivyo.
 
Aisee watoto 3 wanatosha
 
17 wengi sana aisee halafu bado hajaoa
 
Hahahaaa dude is a genetic jackhammer.

He should consider getting nipped.
 
wadada wa tigo wakarimu ... wanatoa huduma vizuri
 
Halafu mshauri ahakikishe anazaa na wadada wenye kazi zao ambao hawatamsumbua kulea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…