Watoto watano kila mtoto na baba yake

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,181
5,429
Hakika dunia tambarabovu!Anasimulia dada mmoja maksio miaka 40 hivi. Ujue kaka (Jimmy) si jina halisi. Mimi nilipomaliza shule tu sikubahatika kuendelea na shule. Nikawa na mahusiano na kijana mmoja pale mtaani kwetu. Katika mahusiano yale nikabeba mimba ndiyo huyu mtoto wangu(anamtaja jina).
Nilipozaa tu hakunitaka ndipo kaondoka na pale kijijini. Mtoto alipokuwa na miaka mitatu nilienda mjini kwa shangazi ili nimsaidie kazi baada ya kujifungua. Nilipofika to nikiwa na mwanangu niliishi vizuri naye. Nikiwa huko alitokea mwanaume akanipenda na kutaka tuishi wote.

Katika neno ninalokumbuka alisema wanawake waliozaa wana nidhamu yaani hata sielewi ilikuwaje nikakubali akanitoa kwa shangazi tukawa tunaishi wote nikabeba mimba nikazaa mtoto wa pili. Mtoto alipofikisha miaka mitatu aliniaga kuwa anaenda chunya kutafuta maisha tukaagana vyema. Miezi mitano tu kupita alinitumia ujumbe kuwa nikipata mwanaume niolewe tu kwani yeye hatorudi na amepata mwingine. Nilihisi dunia ya moto.

Ukweli kutokana na hali ya kuzoea maisha ya mume na mke nikajikuta nami napata mwanaume tuliyekuwa tunapeana tu maana alikuwa mme wa mtu. Katika mahusiano hayo nilikuwa natumia dawa za uzazi wa mpango bahati mbaya kumbe nilipochoma ile sindano tayari nishabeba mimba. Nilipoona mabadiliko tofauti nilijikuta nina mimba ina miezi mitano.

Nilikubali yaishe nikazaa mtoto nikalea akakua. Pamoja na wanaume hao wote niliozaa nao huyu wa now alininasa kutokana na ugumu wa maisha maana watoto walifika umri wa kwenda shule nikawa sina pesa akatokea huyo baba ambaye alikuwa fundi ujenzi hivyo nilifuatana naye kufanya kazi nikapata riziki yangu. Alinisaidia kupeleka watoto shule na hakunidai chochote na huduma za watoto alinisaidia karibia miaka mitatu bila kudai kitu.

Ikumbukwe kipindi chote hicho niliwaona wanaume kama takataka. Ilikuwa siku moja akaniomba nikaandae chakula nimpelekee kazini tulipokuwa tunajenga nami nikafanya hivyo baadaye nilirudi nyumbani nikamwacha naendelea na vibarua wengine kutokana na dharula niliyopata. Nilipofika nyumbani nilipopanga nikaendelea na kazi zangu mpaka ilipofika muda wa kulala nikaenda kulala. Mnamo saa tano usiku nilisikia mlango unagongwa basi nikauliza wewe nani akajibu mimi Fundi basi nikajifunga kitenge nikatoka. Nilipofungua mlango baada ya kuwasha taa akaingia ndani akakaa. Akasema samahani mimi nasafiri kesho nimekuletea posho yako ya kazi ya leo, nikapokea pesa kama elfu saba. Baada ya hapo nikaingia ndani nikaweka hela na kurudi kukaa. Ukweli neno moja ninalokumbuka alisema njoo nikwambie kitu nilipomsogelea tu alinigusa kifuani akanikamata mkono kwa nguvu kanisogeza kifuani akasema unaogopa nini jamani mimi sikujua kilichoendelea zaidi ya kuendelea na mchezo na niliwaza mwenyewe bila kuombwa nikaona nimzalie naye kamoja kutokana na aliyonitendea kweli nikazaa mtoto. Alipofikisha miaka minne yule baba alirudi kwao ghafla mkoa mmoja Nyanda za kati na sikupata mawasiliano naye hadi leo.

Mwisho nilikukutana na huyu aliyekuwa mtumishi wa serikali yeye kila mshahara ulipotoka pesa yote aliniachia na hata alipotaka kutoka aliniomba pesa yeye ama kweli hata nilpobaki ndani niliinua mikono juu nikasema ee Mungu ulimchelewesha wapi huyu. Sikuchelewa naye nikamzalia mtoto maana kwanza dawa za uzazi wa mpango sikutumia kabisa. Mwisho wa siku alipigiwa simu aende msibani kwao alifiwa na mzazi wake na aliporudi alikuja na mke na watoto kumbe kule kwao aliacha mke. Nilipomwambia basi tuwe wote wawili aligoma na hakunielewa kamwe.

Niliinama nikakumbuka nilivyozaa watoto wote hadi huyu wa tano nikaona mbinu zote ni zilezile ila zimetofautiana padogo. Hadi naongea na wewe sasa(anataja jina Langu) wanaume wote nyinyi baba yenu na mama yenu ni mmoja. Sitaki tena sitaki kabisa. Nina watoto watano kila mmoja ana baba yake.

Je wanawake mna kumbukumbu ya kudumu kwelikweli vichwani ama ni nini kinawasibu hadi msiwe na tahadhari katika mapenzi maana hili si kwa waliosoma ama wasiosoma ni karibia wengi yamewakuta. Je nini sababu ya hili?.
 
Mmh ivi hii inakuaje???
Au akishazaa tuu anasahau...... Lakini ucjali hao watoto huko mbeleni wanaweza wakawa msaada mkubwa tu kwako
 


Usemalo wala si uongooo. TRUE STORY siku hizi ukikuta mkaka ana kauwezoooo, yaani hata sio uwezo mkubwaaaa wa maana, kauwezo tu, kajumba na gari tena kajumba kenyewe Kibamba usipomkuta wanawake wamezalia watoto 4 basi unue wa 5. Chinekeeeeeeee! Heeeeeeey!

Yani mwanaume akikwambia yupo single muulize ana watoto wangapi. Maana utafurahi ukijua
 
Duuuuuh!!!! Hii kweli kufyatua.
Huyu inabidi atafute suluhisho la kidini!!! Sio kawaida aisee... Kila mwanaume anaemzalisha anatokomea? Shetani katika kazi yake.
 
Back
Top Bottom