Watoto waamini asili ya binadamu ni ipi?

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
28,827
Reaction score
45,349
Kwa wale mliopitia shule kuanzia ngazi ya msingi mtakuwa mlikutana na mada ya asili ya binadamu kuwa mwanzo wake ni nyani. Hoja ni kwamba ilikuaje nyani aendelee kuwa nyani hadi leo bila kubadilika asili yake?

Utata upo, Biblia na vitabu vya dini zingine kama Qur an vimeandika chanzo cha binadamu aliumbwa na Mungu kutoka kwenye udongo.

Hii inachanganya wanafunzi waamini upande gani, sayansi au dini? Charles Darwin alidai asili ya binadamu imetokana na nyani, ukweli ni upi?
 
Majibu ya swali hilo kwako ni yapi?
 
Asili ya mtu kama kiumbe chenye uhai haitofautiani sana na asili ya viumbe hai wengine, je unaweza kuniambia asili ya Ng'ombe ni ipi?
Basi inaposemwa asili ya mtu ni udongo hiyo itakuwa na maana ya kiroho zaidi (spiritual cannotation).
 
Asili ya Binadamu ni utata.

Binafsi napenda na nimeikubali asili ya mwanadamu kwa mujibu wa Biblia Takatifu.

Sina tatizo na wanaopinga asili hii ya Biblia.
 
Asili inayozungumzwa na Biblia ni ipi???
Ni ile ile dhana ya udongo ila utofauti wake ni udongo aliotumia mungu wa biblia haujaelezewa kama ulikua unatoa sauti kama ambavyo quran takatifu imefafanua
 
Kwahiyo Adam alioa mwanaye "aliyemzaa" kutoka mbavuni mwake na akazaa naye na kisha kupatikana watu wote tuliopo duniani??!!😒

Sio concept hii Pekee ya uumbaji. Concept nyingi za Imani zilizoandikwa kwenye Biblia kuzichambua kwa akili za kisomi hatutoboiii!

Mojawapo ni hii: Ndimi Bwana Mungu wako usiabudu mungu wengine. Hii pia ukihoji kisomi hutoboiiii.

Ndio maana mafarisayo na masadukayo walikuwa wajuzi sana wa agano la kale walipata shida sana kumuelewa Yesu. Ili kuepuka kero zake ambazo waliona zinaharibu agano la kale wakamuundia Kesi. Wakamuua.
 
unahitaji kujithibitishia na kuchunguza na nani anasema ukweli kisha hicho ndio ufundishe watoto wako la sivyo watadanganywa..
 
Sio concept hii Pekee ya uumbaji. Concept nyingi za Imani zilizoandikwa kwenye Biblia kuzichambua kwa akili za kisomi hatutoboiii!

Mojawapo ni hii: Ndimi Bwana Mungu wako usiabudu mungu wengine. Hii pia ukihoji kisomi hutoboiiii.

Ndio maana mafarisayo na masadukayo walikuwa wajuzi sana wa agano la kale walipata shida sana kumuelewa Yesu. Ili kuepuka kero zake ambazo waliona zinaharibu agano la kale wakamuundia Kesi. Wakamuua.

Haya, wewe chambua hiyo concept kwa akili isiyokuwa ya KISOMI tuone kama utatoboa huo ukuta!!

Nakusubiri.
 
Nikumegee siri mkuu, ukimwamini Mungu kwa Imani yako na kushika amri zake inalipa sana. Ninashuhudia binafsi!

Kumwamini Mungu na kumtegemea haina maana kwamba hutopata misukosuko ya Maisha. Yenyewe itakuja Ila utabaki imara mara zote.
 
Sio concept hii Pekee ya uumbaji. Concept nyingi za Imani zilizoandikwa kwenye Biblia kuzichambua kwa akili za kisomi hatutoboiii!

Mojawapo ni hii: Ndimi Bwana Mungu wako usiabudu mungu wengine. Hii pia ukihoji kisomi hutoboiiii.

Ndio maana mafarisayo na masadukayo walikuwa wajuzi sana wa agano la kale walipata shida sana kumuelewa Yesu. Ili kuepuka kero zake ambazo waliona zinaharibu agano la kale wakamuundia Kesi. Wakamuua.
wala hawakuwa na ujuzi wowote wa agano la kale walikuwa wanafiki tu na Yesu aliwasema waziwazi ...kama ukubali futilia maswali Yesu alikuwa anawauliza walikuwa weupe kabisa na mara nyingi hawakujibu
 
Waliamini kwamba wanajua.
Walijinasibu hivyo.
Hawa tunao hata sasa kwenye kizazi hiki.
 
Nikumegee siri mkuu, ukimwamini Mungu kwa Imani yako na kushika amri zake inalipa sana. Ninashuhudia binafsi!

Kumwamini Mungu na kumtegemea haina maana kwamba hutopata misukosuko ya Maisha. Yenyewe itakuja Ila utabaki imara mara zote.

Mkuu, hapa hatuzungumzii juu ya Imani kwa Mungu, tunazungumzia juu ya Eva kutolewa ubavuni mwa Adamu, in literal sense ni kwamba Adamu "alimzaa" Eva kupitia ubavuni mwake (sijui ilikuwa ni kwa operation?? ) na kisha baadaye kumuoa (ilipita miaka), sasa maswali ni haya, hiyo mimba ya Eva Adamu alipewa na nani?? (Mungu apishe mbali), na tukisema Adamu alioa mwanaye tutakuwa tumekosea??, je mtu kuoa bintiye ni sahihi??, kama sio sahihi je huoni kwamba sisi tunaosemwa tumetokana na uzao wa Adam na Eva ni uzao haramu ??,

Kwa concept yako Wewe huoni kwamba Adamu alioa bintiye Eva??

Nasubiri majibu yako yasiyo ya kisomi ili "utoboe" tundu katika hiyo ngome ya maswali.
 
Haya Masomo umefunguka hapa kwangu ni Masomo ya juu Sana. Sijafika kwenye hizi advanced studies!

Mimi nimeishia Masomo ya mungu mtenda muujiza. Akisema inatokea. Basi!

Pengine kwa Neema ya Mungu miaka ijayo nitazamia kwa kina ili tuwe na mjadala wenye afya.

c.c Scars
 
✔✔✔✔ nitakuja kukujuza maana ya Eva kutoka ubavuni mwa Adam, na Maana ya Adamu kuitwa Mtu wa kwanza, (sio mtu wa kwanza kuimbwa), nitakujulisha maana ya mtu kuumbwa kwa udongo kimwili na kiroho pia nitakujulisha watu tulitokea vipi duniani bali hata wanyama mimea nk,

Kifupi ni kwamba sio kila neno la Vitabu vya dini huwa na maana ya mojakwa moja.

Vita subira.
 
Back
Top Bottom