Watoto wa wenye nyumba VS Wapangaji

Watoto wa wenye nyumba VS Wapangaji

Kontelo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
571
Reaction score
161
Heshima zenu wakuu,

Kuna hili swala la baadhi ya wenye nyumba kuishi na watoto zao nyumba moja au hata wenye nyumba watupu kuishi na wapangaji imekuwa kero sana kwa baadhi ya wapangaji.

Nimeshuhudia baadhi ya wapangaji wengi kunyanyaswa na watoto wa wenye nyumba au hata nyumba wenyewe katika baadhi ya nyumba hapa mjin, hata inafikia ili mpangaji kuhama nyumba kwa mdomo au manyanyaso.

Baadhi ya wapangaji/waliowahi kupanga hili wanalifaham.

Unadhan baadhi ya wapangaji kunyanyaswa kwa either kupandiahiwa kodi bila maelezo, kupandishiwa hela ya umeme, maji na hata kupangiwa mda wa kurudi nyumbani husababishwa na nini?
 
Ni umaskini tu, unadhani yule anayepanha nyumba nzima yenye geti kilakitu self, mwenye nyumba atamnyanyasa hivyo, thubutuuu....

Hata kumwendea mpangaji tu inabidi mwenye nyumba apange appointment, tatizo ni kupanga chumba kimoja tena uswazini choo half kilometre.....watoto wanatoka ndani wanakimbilia chooni wamejishika nyumba utafikiri mbwa kafyata mkia wanakutana na baba nae amefyata mkono katikati ya miguu hivyo hivyo mbio chooni, hapo heshima itoke wapi!

Kati ya vitu vilivyonihamasisha kujenga nyumba katika umri wa ujana kabisa ni manyanyaso kutoka kwa watu ambao ukiwaangalia kiuchumi hawajakuacha kihivyo kama si kuwa sawa au hata kuwazidi.
 
nyumba zenyewe za urithi. lakini pia kuna wapangaji wakorofi
 
Jenga Yako...ili kodi umeme maji taka na usafi visipandeee as long upo kwa watu....Tuliaaaa kimyaaaa
 
Suala la kunyimana kugegedena linaingia hapa
 
Mambo ya choo passport size heshima itoke wapi, fanya kazi kwa bidii weka hicho kidogo unachopata utafute heshima mkuu. Familia lukuki kuishi nyumba moja lazima kutakuwa na matatizo kila siku, jenga yako hata kama mbali na mjini, lakini afadhali kuliko hizo tabu za uswahilini.
 
Huwa wananishangaza tu wale wamama wenye nyumba wasiotaka kijana mpangaji kuwa na mchumba au kumkaribisha mpenzi/mchumba...
 
Wenye nyumbaa wengine ni wanokoo sanaa utakuta ashapata mtu anayetaka chumbaa kwa bei ya juu so anakuwekeaa visangaaa uamee kwakeee.
 
Shida zinazotajwa kwa namna fulani ni baraka, kwa vile zinatoa hamasa kubwa kwa watu kujijengea nyumba zao.
 
Huwa wananishangaza tu wale wamama wenye nyumba wasiotaka kijana mpangaji kuwa na mchumba au kumkaribisha mpenzi/mchumba...

Kwa upeo wangu mfupi nahisi km wanaogopa watoto wao kuharibika kisaikolojia kwa kuhisi kubadilisha wanake/wanaume kila siku huo ndo mfumo wa maisha. Ndio maana wanaweka misimamo ya kuingiza mmoja tu ili usiharibu vichwa vya watoto wao
 
Wenye nyumbaa wengine ni wanokoo sanaa utakuta ashapata mtu anayetaka chumbaa kwa bei ya juu so anakuwekeaa visangaaa uamee kwakeee.

Nadhan madalali nao huchangia ktk hili. Anamfata mwenye nyumba na kumuahidi mpangaji mwenye dau nono.....hapo ndo mshikemshike unapoanza
 
Shida zinazotajwa kwa namna fulani ni baraka, kwa vile zinatoa hamasa kubwa kwa watu kujijengea nyumba zao.

Shida zikizidi sana huwa kero, hata maji ya mvua yakiwa mengi huitwa mafuriko....
 
Mtaoa mada hapa ana matatizo ya kisaikolojia... labda nimuulize bei ya cement .....pili anunue kiwanja aanze kazi... tatu... siku zote mpangaji huna haki... mwenye nyumba ni mali yake kwa hiyo anayo haki ya kuandaa mkataba yani makubaliano na mpangaj.. ukiona ni magumu sepa au kajenge yako....
 
Back
Top Bottom