Niwasalimu wana bodi..
Ni w'kend hii ambapo nilikuwa na mazungumzo na rafiki yangu mmoja ambae tumemaliza nae chuo mwaka jana.
Jamaa bado hajapata ajira na haoni ayo matumaini kwani anatumia partial ya semista tano kuombea ajira kwa case ya full hawezi kupata kutokana na kudaiwa malimbikizo ya ada (kwa wale waliokuwa wanategemea boom il aishi ataona ilivyo ngumu kugawa boom ilo ilo kama ada na matumizi).
Imefikia mahali ametamani kurudi kijjni kwao akalime ila hata huko anahitaj mtaji angalau wa kuanzia kufanya kilimo hicho (aliniweka wazi kuwa anahitaji angalau mashine ya umwagiliaji akafanye kilimo cha mboga mboga).
Nafahamu kuwa kuna viongozi mbali mbali wa serikali wanaingia humu na probably wataisoma hii thread...ningeomba walione tatizo hilo na angalau waje na plan za kuwasaidia hawa graduate ambao karibu wanamaliza mwaka mtaani (najua pia kuna wengine wengi wana miaka kibao mtaani wanatafuta ajira bila ajira).
Naomba kuwasilisha.
kama bado kuna mtu anaamini viongozi watamsaidia, anahitaji msaada zaidi ya anavyofikiria! Wale viongozi wa kujali shida za watu wanaowaongoza waliondoka na zama yao. Zamani zile hata kiongozi angekuwa dhalimu vipi lakini bado alitakiwa kujali japo kinafiki.
Lakini tatizo likawa ni system inayowalea viongozi. Ilitengenezwa kihuni. Na walizoea kuona uhuni ukifanywa na waandamizi huku ukipakwa mafuta, wakakulia humo. Na wakati ule viongozi walikuwa na uwezo adimu sana wa wao kufanya uhuni huku wakijaribu bila haya kuwakemea wengine wasijaribu!
Kinachotokea sasa ni mabadiliko ya zama. (zama hi inaitwa zama ya advancement ya uhuni wa viongozi). Watu wameacha unafiki wa kujificha. Wanafanya waziwazi. Na wengine wasiofanya wanasema waziwazi. Siku hizi ukifanya uhuni ukaupaka mafuta hawanyamazi, watakwambia au kama hawawezi watakuchora magazetini. Na wanaofanya hawawakemei wengine, na kwa kuwa wengine nao hawhitaji kunyoosha vidole, na wao wanafanya. Kwa hiyo wanafanya bila aibu, hawajifichi tena, na wanaziba masikio yao.
Kwa hiyo niseme wazi hakuna anayejali. Siku hizi uongozi ni ajira siyo utumishi. Na kama ambavyo kila mwajiriwa atataka ajira imnufaishe, the same kwao. Kwa hiyo ushauri wangu kwa huyu mpendwa pamoja na wengine ni kuanza na chochote ulicho nacho na unachoweza! Unataka mbogamboga? Kaanze kwa mikono, maji beba kichwani. Kuna siku italipa, utanunua mashine ya maji, na huenda trekta. Who knows, kuna siku utakomboa vyeti vyako!
Naona niseme hivi kwa kuwa is better you know that nobody is coming to your rescue and you are on your own. Kuliko kusubiria msaada amabo hautakuja. Guys, they don't care.
.!?..,mbona maandiko yako yamefanana na mtoa mada
Kama bado kuna mtu anaamini viongozi watamsaidia, anahitaji msaada zaidi ya anavyofikiria! Wale viongozi wa kujali shida za watu wanaowaongoza waliondoka na zama yao. Zamani zile hata kiongozi angekuwa dhalimu vipi lakini bado alitakiwa kujali japo kinafiki.
Lakini tatizo likawa ni system inayowalea viongozi. Ilitengenezwa kihuni. Na walizoea kuona uhuni ukifanywa na waandamizi huku ukipakwa mafuta, wakakulia humo. Na wakati ule viongozi walikuwa na uwezo adimu sana wa wao kufanya uhuni huku wakijaribu bila haya kuwakemea wengine wasijaribu!
Kinachotokea sasa ni mabadiliko ya zama. (Zama hi inaitwa zama ya advancement ya uhuni wa viongozi). Watu wameacha unafiki wa kujificha. Wanafanya waziwazi. Na wengine wasiofanya wanasema waziwazi. Siku hizi ukifanya uhuni ukaupaka mafuta hawanyamazi, watakwambia au kama hawawezi watakuchora magazetini. Na wanaofanya hawawakemei wengine, na kwa kuwa wengine nao hawhitaji kunyoosha vidole, na wao wanafanya. Kwa hiyo wanafanya bila aibu, hawajifichi tena, na wanaziba masikio yao.