babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,398
- 3,243
Waziri wa ujenzi mh. Magufuli amebainisha ya kuwa mara nyingi akituma timu zake kufanya ukaguzi katika mizani huwa zinarudi bila majibu mazuri kufuatia kukutana na majina ya watoto wa vigogo na hivyo kutishika.
Alizidi kusema kuwa watoto hao walipenya eneo hilo la mizani kwa kuwa wataweza kula hela za Watanzania kwa rushwa hivyo akatoa agizo wote watakao bainika wafukuzwe hata kama ni 10 kwa siku ili kuwapunguza.
Pia aliwataka watumishi kuwajibika kila mtu kwa nafasi yake na kwa uaminifu. Aliyasema hayo mjini Dodoma.
Habari inapatikana ktk gazeti la habari leo.
Hawa watoto wakijadiliwa watu wengi huona kama wanaonewa kumbe wanapenyezwa au kubebwa tu.