Watoto wa mitaani na wanavyotumika

mutant gene

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
876
Reaction score
326
Habari zenu wakuu,

Siku ya juma tatu pale ubungo mataa time za sita usiku na nusu hivi nilikuta mtoto mmoja (umri miaka nane)anakimbia huku nyuma akifuatwa na kundi la wahuni wanne. katika kumhami yule mtoto nikafanikiwa kuondoka nacho. katika kukihoji akanieleza yeye ni mchaga na amekimbia huko Kilimanjaro kutokana na manyanyaso ya mama wa kambo.

Nikamuuliza sababu ya wale wahuni kumkimbiza akasema walikuwa wakitaka kumuingilia kinyume na maumbile. nikamuliza kama alishawahi kufanya hicho kitendo akajibu " huwa wananifanyia hivyo mara kwa mara" aisee nilisikitika sana maana ni katoto kazuri ambacho hapo baadae anatarajia kuwa baba wa familia lakini kutokana na huu mchezo anaofanyiwa tena akiwa katika umri mdogo sidhani kama atakuja kuwa hivyo kama ninavyofikiria.

Basi nikakaa naye huyu mtoto siku ya jumanne nikitegemea siku inayofuata ambayo ni jumatano nimpeleke kituo cha polisi. siku hiyo hiyo ya jumanne jioni nikapigiwa simu kutoka nyumbani kuwa mtoto haonekani wamemtafuta maeneo ya nyumbani bila mafanikio.

Nikaona isiwe tabu usiku wake time zile zile nikapita tena bahati nzuri nikamuona yule mtoto maeneo yale yale. wakati nikiwa katika mazunguzo naye aligoma kabisa kurudi nyumbani. mara vijanawawili wa kihuni wakatokea wakawa wanamvuta yule mtoto. yule mtoto akawa anapiga kelele " uncle nichukue wanaenda kunibaka hawa" basi nilipambana nao nikafanikiwa kumchukua yule mtoto ila waliniumiza maeneo ya kichwani baada ya mmoja wao kurusha jiwe na kuvunja kioo.

Kitu ambacho kinanishangaza hivi wanaume wezangu inakuwaje ukampenda mkeo/ hawara yako kiasi kwamba akamnyanyasa mtoto wako hadi ikafika hatua ya mtoto wako kutoweka hapo nyumbani na wewe unaridhika kabisa kwa sababu ya K tu!!! jamani tuache ujinga hawa watoto wananyanyasika sana huku mitaani na kufanyiwa vitendo vya ajabu na vya kikatili! tuwalee watoto zetu tuache kusikiliza maneno ya hawa wa mama wa kufikia sio wazuri wengi wao ni waongo waongo sana.

Kinachosikitisha zaidi sijui huyu mtoto atakuwa ameingiliwa mara ngapi kinyume na maumbile na hawa wahuni??!! inasikitisha sana!!

Vilevile hii inaonesha kuwa jinsi gani hawa watoto wanaozagaa huku mitaani wanavyonyanyasika kijinsia tena na watu wazima!
 
Mungu akujalie kwa wema uliomfanyia huyo mtoto! Waziri mwenye dhamana ya hiyo wizara yupo saluni anajikoboa sura awe mzungu usoni!
 
1. roho za wake zetu wanazijua wao wenyewe na Mungu wao.
2. hivi mwanaume unasimamishaje dudu lako ukimuona mwanaume mwenzio? ina maana hata ukiona gari la maji taka unalisimamishia?
 
Kwanza hongera sana kwa roho yako nzuri kwa wema uliomtendea huyo mtoto....
Je,huyo mtoto yuko wapi sasa hivi?
 
Kitendo alichofanyiwa huyu mtoto, ni unyama uliopitiliza kabisa. Wazazi tunapaswa kuwalea vema watoto wetu. Pia nampa pongezi huyu bwana, kwa kujali na kutetea haki za watoto. Wote tunapaswa kuuiga mfano huu!
 
Swali la kizushi, why mtoto alitoroka nyumbani kwako na ulipomfuata akagoma kurudi.? Na kwa mujibu wa maelezo akakubali alipoona wahuni wanamfuata.?
 
Waganga wanawadanganya sana, mie huwa sishangai mtu kufanya hivyo kwa mtoto
 
Serikali ni kama mzazi inatakiwa kuwajali hawa watoto na pia kuwachukua hatua kali wananyanysaji wote. Ni laana kuwaacha watoto wanatesa hivi.
 
Hao watoto wadogo wa Ubungo wanalawitiwa Sana'a....Wanalawitiwa wao kwa wao au na Yale majamaa majitu mazima pale Ubungo.
Niliwahi kujifanya na Mimi ni teja na kibaka kwa siku kadhaa pale Ubungo...ili tu nijue hali iliyopa pale,Kiukweli kuna mengi sana yanayoendelea kwa wale watoto.
Kwa kweli wale watoto wengi kula yao inategemea kulawitiwa...Lakini Waziri husika yupo Saloon kujikoboa ili vijana wadogo wamapigie mruzi
 
Mungu Akubariki Kwa Moyo Wako...Ila Ukirudi Usiste Kujibu Maswali Ya Wenzangu Hapo Juu Kwan Ninashauku Ya Kujua Alipo Huyo Mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…