Watoto wa majuu na mchezo mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa majuu na mchezo mbaya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Timtim, Mar 27, 2009.

 1. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Source kutoka Nifahamishe.com zinaeleza kuwa

  Matokeo ya DNA yamethibitisha kuwa yule mtoto aliyetangazwa kuwa baba mdogo kuliko wote Uingereza akiwa na umri wa miaka 12, sio baba wa kweli kama ilivyotangazwa.

  Alfie Patten alitangazwa na vyombo vya habari vya Uingereza kuwa ndie baba mdogo kuliko wote Uingereza wakati huo akiwa na umri wa miaka 12 baada ya rafiki yake wa kike Chantelle Steadman mwenye umri wa miaka 15 kujifungua mtoto wa kike.

  Baada ya habari hizo kuwekwa hadharani vijana wengi walijitokeza wakidai Alfie sio baba halisi wa mtoto huyo kwani wao pia walitembea na msichana huyo na wengine wakisema kuwa msichana huyo alikuwa na wavulana wengi sana.

  Ingawa Chantelle alikanusha habari hizo na kusema kuwa Alfie ndio alikuwa mwanaume wake pekee, vijana hao walishinikiza vipimo vya DNA vifanyike ili kumjua baba halisi.

  Alfie alikubali kufanyiwa vipimo vya DNA ambavyo vimethibitisha kuwa Alfie sio baba halisi wa mtoto huyo.

  Matokeo hayo yanasemekana yatamuumiza roho sana Alfie ambaye alionekana kuhuzunishwa sana na madai ya vijana hao kabla hajakubali kufanyiwa majaribio hayo.

  Alfie alikuwa akijiamini kuwa ndiye baba halisi baada ya kufanya mapenzi bila kutumia kinga na Chantelle usiku mmoja.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mabalahau..
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sikukubali kabisa...yule mdada amemdanganya kabisa yue mtoto kiume....yule mdada anaonekana ameshakubuu....anajua sana wanaume tena wakubwa....yule dogo akacheze tu kidali po muda. Wake mbado sana atulizane...
   
 4. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Pengine familia ya kijana ni ya kimapesa ndipo kabinti kakapatia njia ya kujipenyeza kwa hiyo familia. Na mchezo wa hao watoto wadogo si mzuri inabidi wazazi wao kuwakemea maana inakuwa too much. Ni kweli kwetu Africa mchezo huo upo ila ni kwa sura tofauti, binti anakuwa mdogo na kajogoo anakuwa mkubwa kwa umri.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Mambo hayo sio majuu tuu, hufanyika hata hapa bongo. Watoto wetu hucheza sana mchezo wa 'baba na mama' na hayo hutookea ila hayaandikwi.
  I have a jirani, binti yake 13 years aliconceive akiwa class 7 hizi shule za kisasa za academy na baba na mama wakamtoa mimba kwa siri. The girl ni form three now, kicheche wa kutupwa na ndipo siri ikaleak amefanya abortion at 13!.
  This was supposed to be a police case, lakini wazazi waliizima kuepuka aibu na kumvurugia masomo binti wakiamini wanamsaidia, kumbe ndio wamempa go ahead ya kuhitimu mapema.
  Watoto wetu hawa hawa, huwezi amini.
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ya tunajifanya watu wa maadili sana hatutaki kuweka mambo hadharani ndio impact zake. Anyway turudi kwenye mada basi dogo anaweza kuclaim fidia kwa kusingiziwa na kuvunjiwa heshima.
   
Loading...