Watoto sio miradi yenu

Watoto sio miradi yenu

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
745
Reaction score
1,504
Na. Robert Heriel.

Haya ni majibu kwa Mhe. Jumanne Kishimba Mbunge wa Kahama na Wazazi wote wenye mtizamo kama wake.

Nilimsikia Mbunge huyo siku nyingi zilizopita akitoa hoja zake bungeni kuwa iundwe sheria mahususi kwa ajili ya kuwashinikiza watoto kuwasaidia Wazazi wao waliowalea. Kwa kweli nilishangaa kumsikia mheshimiwa akiongea mambo hayo. Hata hivyo naheshimu maoni yake lakini siungani naye hata kwa chembe.

Wazazi wote wenye mtizamo kama huu waachane nao tuu maana ni mtizamo finyu na haulisaidii taifa zaidi ya kulilemaza.

Mzazi bora kamwe hawezi fikiri jambo kama hilo hata kwa kuota. Yaani unazaa watoto ili wakusaidie baadae? Hawa ndio wale wazazi ambao wanawanyanyasa watoto wao kila kukicha.

Mara utasikia Mimi nimekuzaa. Kwani nani alikutuma uzae. Si wewe mwenyewe kwa utashi wako umeonelea uzae na utaweza kuwatunza? Sasa kutishia watoto wako kuwa umewazaa wakati hawajakutuma ndio nini.

Wewe kama mzazi lazima ujue kuwa ukiamua kuzaa basi ni jukumu lako kumlea mtoto wako mpaka atakapojitegemea. Na wala mtoto wako halazimiki kukulipa fadhila ikiwa ataona hivyo.

Mhe. Kishimba ni wale Wazazi wanaonyanyasa watoto wao. Kila kitu mimi ndio nimekuzaa. Mimi ndio nimekusomesha. Nani alikutuma uzae. Huyo ndiye unapaswa uingie naye mikataba. Sio mtoto ambaye hakukutuma umzae.

Nafahamu pia mimi ni mzazi wa Badae. Na wote sisi tuwazazi wabadae. Lakini mimi mtoto wangu hakunituma nimzae. Wala hakunitaka nimzae. Kwa hiyo endapo nitamzaa ninalojukumu la kumtunza mtoto kulingana na mahitaji ya dunia kwa wakati niliokuwapo.

Sio nimsomeshe au nimfanyie jambo lolote kutegemea malipo kwa mtoto. Huo si ndio wendawazimu wenyewe.

Sikuzai ili nipate fadhila au malipo yoyote. Nakudhaa kwa sababu nataka uendeleze kizazi changu. Nataka uendeleze jamii ya wanadamu. Mungu kaagiza tuzaliane. Natimiza agizo la Mungu

Agizo la Mungu ni pamoja na kuwalea watoto katika njia iwapasayo. Kuwasomesha, kuwafundisha kazi, kuwafundisha habari za Mungu, Kuwafundisha tabia njema na mambo mengine.

Kuzaa sio biashara. Yaani uzae mtoto ili akulipe kwa mambo uliyomfanyia. Sasa heshima yako ni ipi kama mzazi.

Kusubiri malipo kwa mtoto ni kujishushia heshima kama mzazi. Yaani kwa akili ya kawaida mtoto unamuambia kabisa nakusomesha ili unisaidie badae ilhali mtoto mwenyewe hata muelekeo wa maisha bado wewe kama sio kichaa unadhani ni nani.

Hakuna upendo wa mzazi kwenda kwa mtoto kwa faida. Hakuna upendo wa biashara. Hakuna nasema hicho kitu hakuna. Mimi kama mzazi wangu akisema hivyo basi kuanzia siku hiyo hiyo tunaanza biashara ya upendo.

Wazazi wa siku hizi ndio wanaharibu watoto. Embu fikiria mzazi anaongea vitu vya ajabu kama hivyo bado kuna heshima hapo. Mzazi anajishushia heshima bila kificho.

Sishangai kwa nini watoto wa siku hizi hawawasaidii wazazi wao. Hii ni kutokana na jinsi walivyolelewa. Hawakulelewa kwa upendo. Unakuta mzazi anajitutumua kumsomesha mtoto huku akimsimanga na kulalamika. Mara unaona ninavyohangaika kwa ajili yako. Unaona ninavyokopa kwa ajili yako ili usome. Unaona ninavyopigana kwa ajili yako. Sasa unamuambia hivyo kwani yeye haoni. Yeye hana akili ya kuona unavyomjali.

Mwisho unamwambia nakusomesha hapa alafu kumbe napoteza pesa zangu. Hautanisaidia. Hakuna upendo wa kutegemea malipo.

Ndugu zangu ukiona mzazi anategemea malipo ya aliyokufanyia ujue hakupendi wala hakuwa anakupenda. Hakuna upendo wa kurudisha malipo. Hiyo ni biashara hapo.

Hata biblia inaeleza ni yapi majukumu ya mzazi kwa mtoto. Biblia inaeleza wazi kabisa kuwa Haimpasi mtoto kuweka akiba kwa ajili ya wazazi wake. Bali wazazi ndio wanapaswa kuweka akiba kwa watoto wao. Ni jukumu la mzazi kuweka akiba kwa watoto wake. Mtoto hana wajibu huo.

Wazazi wenye tabia hii muache mara moja. Ni tabia ambayo hata wanyama hawawezi kuwa nayo. Ni tabia ya hovyo na unyonyaji uliotukuka. Huwezi mzaa mtoto alafu uje umfanyie uhuni kama huo.

Mlee mtoto kwa upendo sio ufanye ujasiriamali kwa watoto. Sio ugeuze watoto miradi ya kukupa fedha.

Vijana ambao tunaenda kuwa wazazi tuachane na tabia hizi za hovyo. Kama unazaa kwa ajili ya biashara ya watoto tegemea mawili. Kupata faida au hasara. Lakini kama unazaa kwa kutimizia matakwa ya Mungu lazima upate faida.


Kama ulikuwa unamlea mtoto wako bila manung'uniko basi naye atakuheshimu kama mzazi bila manung'uniko. Lakini kama ndio wale ooh! Nimekuzaa! Ooh! Nimekusomesha! Yaani unalalamika basi tegemea malalamiko kwa mtoto.

Binafsi Mzazi akinambia maneno kama hayo. Huwaga namjibu kabisa kwamba hukutumwa unizae. Nashukuru Mungu wazazi wangu hawajawahi nambia hivyo. Ila wakinambia hivyo wategemee jibu kama hilo.

Kuna watu wataniona sina adabu lakini kitu cha pekee wasichokijua ni kuwa mimi sina unafiki. Kama mtoto hatakujibu kwa sauti basi atakujibu moyoni. Ipo hivyo.

Haya ndio yale ya mahari. Unaenda kuoa unasikia mahari milioni Sita sijui kumi. Mtoto kageuka mradi.

Haya mtoto anataka kuoa unamuwekea vikwazo sijui usioe huyo. Yupo hivi au vile. Wakati huo huo hujamsaidia mtoto kutoa mahari. Hivi hii ni akili au matope. Mzazi anao uamuzi wa kukataa mtoto asioe ikiwa yeye ndiye anatoa mahari na sio vinginevyo.

Sishangai kuona watoto wa siku hizi wakiwa hawana adabu kwa wazazi wao. Sishangai kuona watoto wa siku hizi wakiwa hawawasaidii wazazi wao. Hii yote inatokana na baadhi ya wazazi kuwalea watoto wao katika hali ya manyanyaso. Wazazi wanalalamika kutwa. Umefeli kidogo mara utalipa pesa yangu. Yaani mzazi kusema hivyo ni kumfanya ajione kama sio sehemu ya familia.

Wazazi wanaolea watoto wao kwa upendo na bila malalamiko hupewa fadhila za upendo zisizo na malalamiko.

Lakini wazazi waliolea watoto wao kwa upendo wenye faida na malalamiko hupewa fadhila za chuki huku wakilalamika.

Hujawahi kuona Mtoto akiambiwa na mama yake nitumie elfu kumi tuu jinsi anavyovuta mdomo. Basi atatuma hiyo pesa lakini atalalamika siku nzima. Utasikia Mama naye, au Baba naye kila siku kuniomba pesa. Kwani hakuna watoto wengine. Kila siku mimi. Wapo wengine wanaosema kabisa ila wengi hulalamika chini chini.

Pia mzazi aliyeombwa pesa na mtoto wakati wa malezi. Akawa anamwambia si umuombe Baba yako, au Mama yako. Au nenda kwa ndugu zako. Au utasikia unachezea hiyo Tv Baba yakoau bibi yako anaweza kuinunua. Wazazi hawa hupata matokeo yale yale watoto wao wakikua. Utasikia mtoto anamjibu mzazi; Kwani nipo peke yangu si uwaombe na wengine. Kwani mama nawe si unadada au kaka zako. Kwa nini hawakusaidii.

Wewe badala ubebe jukumu la kumsaidia mtoto wako unamwambia awaombe wengine. Kwani hajawaona? Basi ndio unakuta litoto nalo linarudisha matokeo yale yale lilivyolelewa. Mtoto ukiona mama/Baba anakuomba wewe msaada sio kwamba wengine hajawaona. Bali ameona wewe ndiye msaada kwake.

Wazazi tunapaswa kuwalea watoto kwa upendo. Upendo haujivuni. Yaani nilikusomesha..Sijui nilifanya blah blah blah. Sasa ulitaka afanye nani. Upendo hautaki malipo.

Tufanye kazi. Tuweke akiba zitakazo tusaidia wakati tukiwa wazee. Akiba hizo hizo zitumike kusaidia watoto ambao hawana uwezo wa kukabiliana na maisha mpaka pale watakapo himili.

Watoto ni baraka halikadhalika na Wazazi. Sio unazaa watoto unaowaona mizigo alafu baadae nao wakuone mzigo. Ukiwaona watoto kama Baraka nao watakuona kama baraka. Ukiwaona mzigo nao badae watakuona mzigo.

Unachopanda ndicho utakachovuna. Usitegemee kuwalalamikia watoto wako alafu wao wakutukuze. Lazima nao wakulalamikie.

Zaa kama wanyama. Wale unaoweza kuwahudumia ndio uwazae. Sio unazaa watoto wengi alafu kulea inakuwa mtihani. Ati unamzalia Mungu. Kama unamzalia Mungu subiri Kuzeeka na Mungu. Kama kila mtoto anakuja na riziki yake basi hata kila mtu huzeeka na riziki yake.

Mwisho niseme; Huenda nimetumia lugha kali lakini hiyo ndio itakayoeleweka kwa wazazi na watu wenye mtizamo huo.

Watoto tuwalee wazazi wetu kwa upendo hata kama walitunyanyasa. Kwa wale tusionyanyaswa tuendelee kuwalea wazazi wetu.

Kwa sisi vijana ambao ni wazazi wa baadae. Tuondoe hiyo dhana mbaya ya kuwageuza watoto Miradi.

Tuijenga nchi yenye jamii bora isiyotegemezi.

Robert Heriel.
Taikon wa fasihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani".
 
Kweli jukumu la mzazi ni kumjengea misingi bora Mtoto na si kutegemea malipo.

Wazazi wengi hawajui tofauti kati ya zawadi na malipo.
 
Umeandika Sanaaa. Yaan bila hata Sheria kutungwa.

Ni upumbavu wa kiwango cha kimataifa, ikiwa wewe Kijana mwenye nguvu ,utaamua kutoshikilia wazazi wako ambao uzee na changamoto zake vinawaandama.

Alafu maajabu, wakati unawapuuza wazazi wako, Huko nje una vimada kama vinne, unavikipia kodi, chakula, mavazi, na matumizi makubwa makubwa na madogo madogo.

Ukisikia Fulani ni Tahira. Ndo utahira wenyewe huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika Sanaaa. Yaan bila hata Sheria kutungwa.

Ni upumbavu wa kiwango cha kimataifa, ikiwa wewe Kijana mwenye nguvu ,utaamua kutoshikilia wazazi wako ambao uzee na changamoto zake vinawaandama.

Alafu maajabu, wakati unawapuuza wazazi wako, Huko nje una vimada kama vinne, unavikipia kodi, chakula, mavazi, na matumizi makubwa makubwa na madogo madogo.

Ukisikia Fulani ni Tahira. Ndo utahira wenyewe huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipe muda wa kukujibu, maana umejibu kwa mihemko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani sana ifike hatua kila mzazi alitambue hili. Kwamba kumuwekea misingi mwanao huo ni wajibu wako na sio fadhila.
Kumuwekea misingi mwanangu na kuweza kujitegemea hiyo kwangu inatosha sana kujivunia.

Ila hii isiwe ticket watoto kuwatelekeza wazazi. Unajisikiaje wewe unakula na kusaza kuku, huku mzazi wako analalia na kuamkia matembele?
 
Mtoa mada huja balance hoja yako

Mi mwenyewe siungi mkono kauli ama dhana ya kuwa nina deni kwa mzazi kwa kuwa tu amenizaa, kunizaa limua yeye, mzazi ana jukumu la kumtunza mtoto na kumpa mahitaji yake kwa uwezo wake wote äkishamzaa

Na mimi kama mtoto nina jukumu la kumtunza mzazi wangu na kumpa mahitaji kwa uwezo wangu kipindi akiwa hajiwezi kama mzazi nae aliniwajibikia vizuri, it goes both ways

mzazi akiwa mlevi au malaya na hajali mtoto kisha anategemea mtoto huyo aje kumlea akiwa mkubwa kwa sababu tu alimzaa, huyo anasthili kutoswa

na mtoto aliylelelewa na mzazi kwa upendo na kumpa mahitaji kadri ya uwezo wake, huyo mtoto ana jukumu (sio hiyari) la kumtunza huyo mzazi kipindi hajiwei ma anastahili laana aa kifungo kama asemavyo kishimba
 
Wanajua ila ufukara unawafanya wasahau.
Kweli jukumu la mzazi ni kumjengea misingi bora Mtoto na si kutegemea malipo.

Wazazi wengi hawajui tofauti kati ya zawadi na malipo.
 
Nini Ushauri wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuzai watoto kama mbwa anavyozaa! Tunazaa ili kupata social security wakati mzazi hujiwezi. Hivyo tunajinyima tunauza Tulichonacho ili tuwaendeleze mueze kujitegemea na cha ziada mtusaidie uzeeni au wakati wa shida kama corona nk. Ni dhana potofu kufikiria kuwa tuliwazaa kwa raha zetu za kwichikwichi, ungejua wengine unalazimishwa kuwa nahitaji sha hawa zako ili tupate mtoto. Ndiyo maana katika vitabu vitakatifu tunaelezwa kuwa kwichikwichi ni kitendo cha kutafuta mtoto na si kujifurahisha.

Kumbuka hakuna haki bila wajibu. Ni haki ya mzazi kutafuta mtoto na ni wajibu wa mtoto kutunzwa na kugharimiwa na mzazi. Vile vile ni haki kwa mtoto kutunzwa na kugharimikiwa na mzazi ila ana wajibu wa kumtunza baadaye.

Angalia hii videoclip na uone mantiki ya andiko langu ‘young man’
 

Attachments

  • IMG_2191.MP4
    7 MB
Hatuzai watoto kama mbwa anavyozaa! Tunazaa ili kupata social security wakati mzazi hujiwezi. Hivyo tunajinyima tunauza Tulichonacho ili tuwaendeleze mueze kujitegemea na cha ziada mtusaidie uzeeni au wakati wa shida kama corona nk. Ni dhana potofu kufikiria kuwa tuliwazaa kwa raha zetu za kwichikwichi, ungejua wengine unalazimishwa kuwa nahitaji sha hawa zako ili tupate mtoto. Ndiyo maana katika vitabu vitakatifu tunaelezwa kuwa kwichikwichi ni kitendo cha kutafuta mtoto na si kujifurahisha.

Kumbuka hakuna haki bila wajibu. Ni haki ya mzazi kutafuta mtoto na ni wajibu wa mtoto kutunzwa na kugharimiwa na mzazi. Vile vile ni haki kwa mtoto kutunzwa na kugharimikiwa na mzazi ila ana wajibu wa kumtunza baadaye.

Angalia hii videoclip na uone mantiki ya andiko langu ‘young man’
Nitaliangalia nikipata Muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani sana ifike hatua kila mzazi alitambue hili. Kwamba kumuwekea misingi mwanao huo ni wajibu wako na sio fadhila.
Kumuwekea misingi mwanangu na kuweza kujitegemea hiyo kwangu inatosha sana kujivunia.

Ila hii isiwe ticket watoto kuwatelekeza wazazi. Unajisikiaje wewe unakula na kusaza kuku, huku mzazi wako analalia na kuamkia matembele?
Haswaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom