Watoto 93,000 wameuawa Syria

Watoto 93,000 wameuawa Syria

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
=
syriaDead_2230859b.jpg

=
syriaDead2_2230861b.jpg

=
Umoja wa Mataifa umesema takriban watoto elfu tisini na tatu wameuawa nchini Syria tangu kuanza kwa mapigano nchini humo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya elfu thelathini, tangu umoja huo ulipotoa takwimu zake Januari mwaka huu.
syria+houla.jpg

Ripoti hiyo imesema kuwa watu elfu tano hufa nchini Syria kila mwezi tangu Julai mwaka uliopita
Hata hivyo takwimu hizo huenda sio idadi kamili na Umoja wa Mataifa umesema huenda idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi, kwa kuwa vifo vingi havijaripotiwa.
Asilimia themanini ya waliouawa ni wanaume, lakini Umoja huo umeongeza kusema kuwa tayari umethibitisha kutokea kwa vifo vya zaidi ya watoto elfu moja mia saba ambao wako chini ya umri wa miaka kumi.
afg_dead_children_55.jpg

Vile vile, kuna ripoti kuwa watoto wengine waliteswa kabla ya kuuawa kinyama.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadam Navi Pilllay, amesema wamepokea ripoti ya kutokea kwa mauaji ya familia nyingi wakiwa na watoto wao, ishara kuwa vita vinavyoendelea nchini Syria vimegeuka kuwa janga kuu huku maelfu ya watu wakiendelea kuuawa kila siku.
Wakati huo huo, wanaharakati wa upinzani nchini Syria na shirika la habari la serikali wamesema kuwamakombora yaliyorushwa na wanajeshi wa waasi yameanguka katika uwanja mkuu wa ndege mjini Damascus.
Moja ya makombora hayo yaliyotengenezwa nyumbani, lilianguka karibu na barabara ya kurukia ndege na hivyo kulazimisha safari kadhaa za ndege kucheleweshwa kwa sababu za kiusalama.
Shambulio hilo ndilo la kwanza katika uwanja huo wa ndege ambao kwa sasa umezingirwa na wanajeshi wa serikali.
damascus_air_custom-f5805650bc2a80a192b2cc55478cf8eceffcd9cf-s6-c30.jpg


Source: bbc
 
Siamini na sitokaa niamini ila hizi ni propaganda ili tuwachukie viongozi wazalendo. Walianza na sadam then gaddafi na mugabe
 
Yeyote mwenye kuona picha hizi kama ni mwanadamu wa kawaida hana budi bali kuwaonyesha huruma na kuwaombea.

Sio kuleta malumbano ya siasa kwenye matukio kama haya!
Hii si desturi ya watanzania.
Sasa sijui huyu maxshimba ni kiumbe wa kwaida au ni devil!

Haonyeshi chembe ya imani hata kwa watoto wadogo.!

Unategeme huyu mtu ukikutana nae kwenye kona atakuacha huyu!
 
Syria said on Thursday a preliminary investigation showed that anti-government armed groups carried out a massacre last week in Houla region with the aim of encouraging foreign military intervention against the government.
Brigadier General Qassem Jamal Suleiman, head of the investigation committee formed by the government, said the victims were families "who refused to oppose the government and were at odds with the armed groups".

Syria: anti-government groups committed Houla massacre | Reuters

Eyewitness accounts and admissions from supposed collaborators say Sunni rebels tried to frame the Assad (gvt)regime.
link http://news.antiwar.com/2012/06/09/report-syrian-rebels-responsible-for-houla-massacre/
 
Rebels fighters in Syria have attacked a village in the country's east, killing dozens of Shiites. A Syrian government official denounced the attack, saying it was a "massacre" of civilians. An opposition group based in London, the Syrian Observatory for Human Rights, which relies on a network of thousands of sources inside Syria from both sides of the conflict, said many of those killed were pro-regime loyalists, but video posted online from the village revealed a much darker side to the war.

http://www.cbsnews.com/8301-202_162-57588904/syria-rebels-behind-alleged-massacre-of-shiites/
 
Mkuu Kahtaan

"Jadiliana nao(wenye imani,msimamo tofauti na wako) kwa lugha nzuri, nyepesi, laini na tamu."

Umekubali kuchokozeka? Wamekutoa nje ya ulingo(malengo)? Watakulamba "ban".

Mkuu nonda inauma sana kuona mtu anashangilia vifo vya watoto wadogo wasio na hatia yyt.
Halafu ana jiita "rafiki wa mungu!

Basi wanitukane mimi na imani yangu. Lkn sio kuleta utani na kejeli kwenye vifo vya hawa malaika.
Na hao Jf hawaoni hayo wanayo yafanya wengine ??

Lkn Yote kheri.!
 
Back
Top Bottom