Watoa maamuzi serekalini mnatupeleka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoa maamuzi serekalini mnatupeleka wapi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Prodigal Son, Jan 19, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Inasikitisha na kukatisha taamaa kweli,mashirika mengi ya umaa kama TRC (Reli), ATC, ndege, Simu, viwanda tulitumia nguvu nyingi tena saana kuyaanzisha na mengine yalikuwa yanafanya vizuri saana, kinachoshangaza ni jinsi serekali ilivyoyagawa kwa wawekezaji uchwara na mengine kuyauwa kwa visingizio mbalimbali, nachojiuliza tutaendelea lini???
  Serekali ilipokuwa inawapa Wahindi Shirika la Reli inamaana haikuwa inajua kwamba hii kampuni hainauwezo kabisa wakuliendesha hili shirika? Mlikuwa hamna taarifa hawa hawa Wahindi walikuwa wanaendesha shirika la reli huko Angola na Msumbiji wakawa na migogoro lukuki? Pesa mlizotumia kuingiza TRC kwenye huu mkataba feki na Wahindi kuanzia kutangaza tenda, majadiliano mgezipeleka kwenye sekta ya afya mgeokoa roho za Watanzania wangapi? Ngenunua madawati, ni wanafunzi wangapipi wangenufaika?

  Nyie watendaji wa Serekali mnaogawa rasilimali za taifa bila uchungu wowote tuwatofautisheje na ile mikataba aliyosaini CHIEF MANGUNGA NA WAJERUMANI????, naangalia mwelekeo wa taifa sioni, TUTAENDELEA LINI?? Nikiamgalia kwa muelekeo Tanzania baada ya mika 50 ijayo itakuwa wapi? Naona giza kabisa, Mipango kibao utekelezaji zero kabisa, Mind set za watawala wetu ni kwamba hiki atatusaidia Mchina, Muingereza, nk, Mbona India, Malysia, Ghana, Rwanda, wameweza angalau kuonyesha mwelekeo?? Kwa miradi mbalimbali iliyoasisisiwa na wakolini serekal Ilihali kila kitu cha kutufanya tuendelee tunacho, nchi imegeuzwa kama sehemu ya kuchumia ukisha maliza unaenda lia Canada, US, UK, Dubai nk.

  Enyi watoa maamuzi serekalini mkumbuke Mtayajibu yote hayo mbele ya Mungu siku ikifika. Na ni laana mnajitakia nyie pamoja na uzao wenu wote, Ni vema sasa Watanzania wenzangu tuamke watawala wanatuona kama wajinga ndo maana wanafanya kama wanavyotaka.
   
 2. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ukisemacho kina mantiki kubwa sana, ila nachelea kuuliza hivi ni kweli tusubili mpaka mwisho wa ulimwengu ndo waadhibiwe. Je ni kweli hakuna namna nyingine yoyo ya kufanya kulisaidia taifa letu, hususani kwa sisi vijana. Bila shaka uwezo tunao, sababu tunayo, hofu yangu ni je nia tunayo?. kwa wale wenye kufuatilia historia ya vitabu vyote vya dini utakuta mitume walikuwa wanapata utume wao haliwakiwa vijana, je kuna hekima gani katika hilo?. Lai yangu kwa sisi wenye mapenzi na taifa letu hasa vijana especially graduates, tujalibu na kuthubutu kujikita katika uzalishaji mali hususani katika ujasiliamali hii itapelekea kuweza kusolve issue nyingi katika taifa letu, ila tukikaa na kulia lia tuu kila kukicha, itafikia wakati mwana tutakuta si wetu, hii ndiyo bashraf yangu kwa sasa.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  ".........Kill them before they grow..."Brenda Fassie!
   
 4. bona

  bona JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  unaitaji kua mwendawazimu kufikiria mapinduzi kama yale ya kule urusi au china kutoa mabepari barabarani na kuwashoot wote then kuanzisha serikali ya kijamaa baada ya kutaifisha kila kitu na kuacha kufuata maelekezo ya world bank! kama nilivyosema awali unaitaji kua mwendawazimu lakini amini nawaambia iyo ndio njia pekee, i.e ujamaa ndio msamaha pekee wa nchi masikini na raia wake! subirini mambo ya dual citizenship ndio mtapokuta kina bill gates wanakua raia wa tanzania na kununua ardhi yote yenye rutuba maana atakua na haki sawa kama mluguru wa kule matombo morogoro
   
 5. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ujamaa unaweza ukawa ni suluhisho lakini tulishakuwa nao kwa miaka zaidi ya 20, ndio waliweka kama msingi kwa kuanzisha vitu mbalimbali kama mashirika yaliyokuwa ya umma yote ndo wameyauwa na mengine kuwagawia Wahindi, ukiangalia sera nyingi za serekali hazitekelezeki, watumishi wa serekali ni kama Mungu watu,mind set za wanasiasa wetu karibia wote ni tegemezi si majuzi uulimsikia waziri Nagu akiwaomba wachina waisaidie TZ iwe kama Hongkong najiuliza yeye anamikakati gani kama waziri kuisaidia nchi ifike hapo,

  nimejaribu kuresearch saana kuangalia nchi kama South korea, Singapore malasia waliwezaje nikagundua kikubwa walikuwa na strong government, sera zinazootekelezeka, uadilifu na kujitoa. Leo hii ukiangalia wanasiasa wetu kila moja personal interst ndo priorities interst za taifa kwao sio kipaumbele

  wanatupeleka wapi??? solution tuamke tuwaambie basi
   
 6. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  HUYU nagu kweli akili zake fupi!Hongkong is what it is because of a British system.which was there for 100 years..,sasa anawaomba wachina wamsaidie kitu ambacho wao wenyewe wameletewa na waingereza?

  hii inaonyesha huyu waziri exposure yake iko chini ya uvungu.Again why would a chinese minister care about a TZ becoming the next hongkong while the chinese government is busy converting shanghai to Hongkong(a financial center).

  Huyu nagu anaelewa maana nzima ya system ya Hongkong?how can we be like Hongkong with a population of 40M.tutawezaje ishi bila kutoza kodi?!hatuna scientific research centers,education system yetu iko ******,kampuni tunazojivunia ni tigo na vodacom!!

  hii miwaziri ndio inatufanya tuendelee kupiga reverse za GDP kila siku!
   
Loading...