Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,627
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuhusu watu wanaoitwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania, ni kina nani? (human right defenders). Haki za binaadamu ni jambo la kikatiba na kisheria, hivyo watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, walipaswa kuwa ni wanasheria, lakini kwa upande wa Tanzania, jee wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa malipo ya uwakili kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?. Ili wakili uwe ni mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu, inakubidi utetee bure. Jee mawakili wetu wanatetea haki za binaadamu bure?.

Nimepandisha uzi huu baada ya kuguswa na tukio la mawakili wa Arusha, kuandamana kutetea haki za wakili mwenzao, aliyezuiliwa kule Loliondo. Mawakili hao, wamejiita ni watetezi wa haki za binaadamu, swali ni jee ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, au utetezi huu umekuja kwa vile tuu wakili mwenzao ameguswa?, hivyo wanachopigania mawakili hao ni haki za binaadamu, au wanapigania haki za wakili mwenzao aendelee kuvuta malipo ya uwakili kwa ajili ya matumbo yao?.

Naungana na mawakili wasomi wote ambao hutetea haki za binaadamu wote bure bila malipo na bila ubaguzi, kikiwemo kitengo cha msaada wa kisheria cha chuo kikuu cha Dar es Salaam lakini siungi mkono utetezi wa haki za binaadamu kwa sababu tuu aliyeguswa ni wakili mwenzao, hivyo siungi mkono maandamano ya mawakili Arusha, kumtetea wakili mwenzao as if huyo wakili haki zake zikivunjwa, ndio aandamaniwe, lakini kila siku haki za wananchi wengine wengi wa kawaida, zinavunjwa kila siku, sijawahi kuwasikia mawakili hawa hata wakikohoa tuu, achilia wakiandamana!. Hivyo kuandamana kule, mimi nakuchukulia ni kuandamana kwa kupeleka machozi ya mamba (crocodile tears), kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu, ila kinachoandamaniwa ni matumbo yao kwa malipo ya uwakili na sii haki za binaadamu!.
Mifano hiyo na mingine mingi ni ushahidi tosha kuwa wengi wa wanaojiita ni watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania , kiukweli sio watetezi halisi wa haki za binaadamu, bali ni wapigania matumbo yao kwa mwamvuli wa haki za binaadamu, wakiishashibishwa fedha za wafadhili, hupaaza sauti zao sana tuu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu ili tuu wafadhili wawasikie, lakini ndani ya mioyo yao, ndani ya nafsi zao na ndani ya dhamira zao, hakuna utetezi wowote wa kweli wa haki za binaadamu zaidi ya kupigania matumbo yao!, kwa sababu mawakili au wanaharakati, wengi wao ni watu wa mshahara!.

Lakini miongoni mwa watetezi wa kweli kabisa na wa dhati wa haki za binaadamu nchini Tanzania, ni huu mtandao wetu wa JamiiForums au jf, watu humu wanapaaza sauti zao kutetea haki za binaadamu bila kutegemea kulipwa chochote na yeyote, na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, zinawaponza, na zitaendelea kuwaponza, uhuru wao, haki zao, hadi maisha yao, na wengine zikiwaponza wasikamate ulaji for being too vocal or too critical to the current regime, imewa cost kwa sababu tuu ya kusema ukweli!, katika utetezi wa kweli wa haki za binaadamu, mimi naamini ipo siku iso jina, hawa unsung heroes wa JF wakiongozwa na Maxence Melo, Mike na wana jf wengine wote, na jf yetu, italipwa kwa mema yote inayo watendea Watanzania, na itakumbukwa na kuja kupewa tuzo, na hawa baadhi ya mawakili wanaojinasibu ni watetezi wa haki za binaadamu ilhali kiukweli ni watetezi tuu wa matumbo yao, nao pia watalipwa kwa utetezi wao!.

Kwa maoni yangu, nadhani JF wakiongozwa na Maxence Melo na Mike ni miongoni mwa vinara watetezi wa kweli kabisa wa haki za binaadam nchini Tanzania, angalia kila uchao wanavyohangaika na kukabiliwa na mlolongo wa kesi mahakamani zisizo na kichwa wala miguu.

Nasi JF kwa ujumla wake, tunastahili pongezi na hongera za dhati kwa utetezi huu, hizi kelele tunazopiga humu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu, haki za kisiasa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari, haki ya kupata habari, haziendi bure. Hivyo swali linabaki, kwa mawazo yako, jee JF tunastahili kuwamo kwenye list ya watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, nchini Tanzania au jf ni wachafuzi tuu kwa kupinga kila kitu cha awamu hii?.

Namalizia kwa lile swali la msingi, jee watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania ni kina nani?, Jee jf tumo?, Jee hawa wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?.

Wasalaam

Paskali
 
Namshukuru walau Mzee wa Upako kwa kujitokeza na kukemea yanayoendelea katika hii serikali maana watu wengine wakiwemo wasomi kama hao mawakili,viongozi wa dini,viongozi wa vyama vya wafanyakazi,viongozi wastaafu na hata waandishi wa habari kwa kiasi fulani wote wako kimya kwenye swala zima la kukosoa hii serikali.

Wazalendo wa nchi hii wako JamiiForums na kwenye vyama vya upinzani.
 
Mkuu Pasco ,

Sikubaliani na wewe Dikteta(Uchwara) kumpa hadhi ya Dikteta(Mzalendo)

Tuanzie hapo tu kwanza hayo mengine tutawekana sawa

Ila nimecheka sana kwa jinsi ulivyopanga mtiririko huu
Mkuu Ben Saanane, kwenye hili la udikiteta mzalendo, bora tukubaliane kutokukubaliana, kwa sababu, wengi wanaangalia tuu, rais Magufuli anafanya udikiteta gani, lakini ni wachache tunaoangalia the motive behind udikiteta huu!, kwa kumsikiliza Magufuli kwa kauli na matendo, he is very genuine, anayafanya hayo yote kwa nia njema na moyo safi, wa kuikomboa Tanzania, kwa sababu, haki, utawala wa sheria, utawala bora ndio vimetufikisha hapa tulipo, usimwite ni dikiteta uchwala, Magufuli ni dikiteta kweli ila ni mzalendo!, kitu ninachokubaliana na wewe, ni the dividing line between dikiteta kweli na dikiteta mzalendo ni very thin!, na madikiteta wote duniani walianza hivi hivi, kwanza kwa kuwa populist leaders, kisha dikiteta mzalendo na mwisho wa siku kugeuka kuwa a real dictator!.

Pasco
 
Mkuu chukua like za kutosha!!!
 
Mm nmeshangazwa na sheria za Utumishi wa Umma kuvunjwa na ikulu....kada kuwa DAS!! Na maadhi ya watumishi wa CCM kuwa na cheque number za utumish yaani mishahara yao inatoka utumishi.
 
Jf imekuwa sehemu ya watetezi Wa haki za binadamu kusemea watanzania wengi wazalendo imekuwa sehemu ya kusemea jf ni watetezi Wa haki za binadamu wengi tunapaza sauti kupitia jf
 
Kinachonipa furaha na matumaini mema ni kuwa, kwa sasa hatuongelei tena au kulalamika kuhusu wizi wa mali za asili za taifa au ufisadi ndani ya serikali ambao serikali inaufumbia macho.

Hatuongei na kulalamika kuhusu udhaifu wa serikali wakati mali za asili zinaibwa.

Kwa sasa tumebaki kwenye hoja kama udikteta ambazo mtazamo wake unatofautiana kati ya mtu na mtu au nchi na nchi.

Wengine wanadai udikteta uchwara, wengine wakidai udikteta uzalendo huku wengine wakisema hakuna udikteta bali ni usimamizi madhubuti wa sheria zilizotungwa na chombo halali ambazo zinajenga mazingira ya kidikteta.

Haya ni mafanikio makubwa sana kwa kipindi kifupi.
 
Magufulu sio dictector bali ana walk tha talk, hajawai kuvunja sheria za nchi yote anayoyafanya ndio watanzania tumekuwa tukililia kwa muda mrefu sasa yy kaamua kutenda so kwa vile ww umpendi ndo umuite dictator at the end utajua tu unapoteza muda
 

Pasco umeandika vizuri, mawakili siku zote ni wavhumia tumbo.wabadirike
 

Pasco stop that! Hakuna dikiteita mwema. Mpaka hapa watu wanaumia kwa kukosa haki zao bila kusikilizwa. Hilo tu linatosha. Please Pasco stop that
 
Nimemkumbuka Ben.

Paskali
Paskali umepotea. Tunataka kusikia kaulu yako kuhusu kupotea kwa Ben. Hatujui kapoteaje lakini kuna hisia nyingi. Nadhani umezisikia. Ebu tupe philosophical analysis of those rumors!
Leo kapotea huyu , hayanihusu, kesho itakuwa wewe maana wewe ni mwandishi hujui kesho ukiandika utamuudhi nani? Ni vitu vya kukemea.
 
Mkuu Retired, kuhusu kutoonekana kwa Ben, sio tuu kwamba tumeisha sema humu, bali pía we don't rule out, the possibility of an inside job.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…