informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 122
- 111
Inaelezwa kwamba muda mrefu, watetezi wa haki za watoto nchini Tanzania wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi katika juhudi zao za kuandaa na kutumia mifumo rasmi ya utetezi wa haki hizo. Ukosefu wa ujuzi wa kiufundi wa kuandaa ripoti mbadala, uelewa mdogo wa mifumo ya kimataifa ya haki za binadamu, pamoja na ukosefu wa ushirikiano wa karibu na serikali, vimekuwa vikiathiri uwezo wao wa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji na ufuatiliaji wa haki za watoto.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha mafunzo maalum yanayolenga kuwawezesha watetezi wa haki za watoto kuongeza maarifa, stadi na mbinu za kushiriki kikamilifu katika mifumo ya haki za binadamu. Mafunzo yamelenga pia kuwaunganisha zaidi na Serikali ili kuleta ushirikiano madhubuti katika kutekeleza mapendekezo ya kitaifa na kimataifa yanayohusu ustawi wa mtoto.
View: https://youtu.be/VuPA8ElIQoI?si=Ludo7vLJzImvI-_p
Mkuu wa Idara ya Utetezi wa THRDC,Wakili Paul Kisabo akifungua rasmi mafunzo hayo kwa kusisitiza kuwa ni sehemu ya mkakati endelevu wa kujenga uwezo wa watetezi hao ili waweze kuwa sehemu ya suluhisho badala ya kushindwa na mifumo isiyowajumuisha. Alieleza kuwa ushiriki wa watetezi katika majukwaa ya kimataifa ni muhimu kwa maendeleo ya haki za mtoto nchini.
Katika semina hii, washiriki wamepata nafasi ya kujadili changamoto walizokutana nazo, kuchambua mifumo ya ufuatiliaji wa haki za watoto, na kujifunza mbinu bora za kuandaa ripoti mbadala zenye ushahidi na ushawishi.
Kupitia nyenzo na mafunzo hayo, THRDC inalenga kuongeza ubora wa kazi ya utetezi, kukuza ushawishi katika utekelezaji wa sera na mapendekezo ya haki za watoto, na kuwafanya watetezi wawe sauti ya kweli ya watoto ndani ya Tanzania na kwenye muktadha wa kikanda na kimataifa.
Mpango huo wa mafunzo ni sehemu ya hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtoto nchini analindwa, anaheshimiwa na anapewa nafasi ya kustawi katika mazingira yenye haki, usawa .