Msifurahie hali hii, watesi wake bado wanamuwazia mabaya

Msifurahie hali hii, watesi wake bado wanamuwazia mabaya

Kigongoi kwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2018
Posts
554
Reaction score
660
Naomba niwakumbushe wafuasi wake kwamba wasifurahie mambo yaliyowasilishwa mbele ya hadhara kwa ajili ya mtuhumiwa, watesi wake bado wanamuwazia mabaya; kumbukeni ana risasi anatembea nayo, hii ilisababishwa na shambulio lililofanywa usiku kweusi kwenye makazi ya wachawi ambayo usiku kucha hakuna ulinzi kwa sababu watu wapo bize na kuroga.

Mpaka kesho uchunguzi wa aliyefanya tukio hilo au aliyepanga kumuongezea uhai haujafanyika na hawana hata mpango wa kufanya uchunguzi.

Yalitolewa matamko mbalimbali kulaani tukio hilo na wasio na mamlaka wakasema uchunguzi utafanyika kwa kuunda tume. Mpaka leo ububu ukatawala.

Leo akapatwa na dhoruba iliyotengenezwa na watesi wake; akapelekwa kwa Baraza ambapo wasimamizi wa hilo Baraza waliteuliwa na aliyewateua.

Kikao cha Baraza kilipoanza barazani wafuasi walifurahi kuona alivyokuwa hajibu hoja vizuri na wafuasi walihisi kwamba kikao kingeisha hatua za awali; lakini wapi.

Kikao kikapangwa kivingine na jinsi alivyokuwa hapangui haja, wafuasi wanadhani mchezo ungeisha huku wakifurahia utaalamu wa haja zilizowasilishwa pale kwa baraza.

Hili bado sana kwa sababu watesi wake hawataki kumuona na wapo tayari aning'inizwe kwa kamba kwa sababu ya hofu ya yafuatayo:

  1. Huyu amekuwa akiwapinga wachawi miaka yote na iwapo atafanikiwa kutoka atataka na kukomalia issue ya kuchaguana iliyosababisha watu wengi kuzaliwa mwezi Oktoba na kwa tabia yake atataka wahusika wasiwajibike😊
  2. Akitoka atataka mabadiliko ya kuchaguana na kwa sababu ana ushawishi kwa waliorogwa atawasumbua sana wachawi.
  3. Ufisadi mkubwa wa wachawi unaofanywa sasa hivi atakuja kuusanua. Wanamjua sana alivyo, atawatesa.
Rai yangu kwa wafuasi wake wasifurahi kudhani ataachwa hivi hivi, watesi wake wanatafuta jinsi ya kumzuia au kumaliza kwa sababu anaonekana ana roho ngumu kama ya paka, hashawishiki, hashawiriki akiamua kusonga mbele anasonga hata akiwa peke yake. Kikubwa wafuasi wake waombe Mungu ili yaishe; unaweza ukashangaa kutokana na shinikizo la watesi wake akaning'inizwa na hapo ikatengenezwa issue nyingine ya kuridhiana kwa sababu wale wa Baraza waliwahi kusema hawaangalii uzito wa ushahidi uliopelekwa Barazani.

Wasalaam.
 
Siku iyo watu wataingia barabarani na kufa zaidi ya siku ile
 
Da..., aluta kontinua!
Hii mada ikae jukwaa ipasayo kuwepo.
Kabla hawajamgusa, itabídi kwanza watuambie!
akina nani walimmiminia risasi zile. Hao ndio wahaini namba moja, mana waliitisha serikali kwa kutaka kuua kiongozi mbunge kwenye makazi yanayolindwa na serikali. Hii ndio uhaini wenyewe.
 
Back
Top Bottom