Watesaji wa Kibanda, Ulimboka kitendawili

Watesaji wa Kibanda, Ulimboka kitendawili

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
WATEKAJI na watesaji wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka, na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, wanaendelea kuwa kitendawili baada ya Jeshi la Polisi kudai linaendelea na uchunguzi.
Wakata jeshi hilo likishindwa kuwatia mbaroni watesaji wa wanataaluma hao, limetamba kukamilisha uchunguzi wake kuhusu kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu, kwa waandishi wa habari jana, jalada hilo limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Licha ya matukio ya Ulimboka na Kibanda kutokea muda mrefu ikilinganishwa na lile la Lwakatare, Mungulu alishindwa kujibu maswali ya waandishi kuhusu suala ambalo linaonekana kupigwa danadana.

Dk. Ulimboka alitekwa na kuteswa vibaya kwa kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili na kung'olewa meno, kucha kisha kutelekezwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Juni 26, 2012.
Katika tukio linalofanana na hilo, Kibanda naye alivamiwa wakati akiingia nyumbani kwake na kupigwa kwa nondo kichwani, kutobolewa jicho la kushoto, kung'olewa kucha, meno mawili na kukatwa kidole.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na makao makuu limeunda timu za wataalamu kuchunguza matukio hayo lakini hadi leo zimekuwa zikipigwa danadana ya kuwakamata wahusika.
Katika mkutano wake na wanahabari, Mungulu aligusia matukio hayo kwa kifupi akisema uchunguzi bado unaendelea.

"Kuhusu kuvamiwa, kuteswa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk. Ulimboka, matukio yaliyotokea Zanzibar, uchunguzi bado unaendelea na uko katika hatua mbalimbali ambazo kwa sasa hakuna umuhimu wa kuziweka wazi kuepusha kuharibu upelelezi," alisema.
Alipoulizwa ni kwa nini hawajamkamata mtuhumiwa mwingine zaidi ya yule aliyejisalimisha katika kitubio kanisani, Joshua Mulundi, Mungulu alikwepa akiwataka waandishi wasome nakala ya tamko la jeshi hilo.

Hata hivyo nakala hiyo iliyogawiwa haikusema chochote kuhusu tume hiyo kupata watuhumiwa wengine kwa kesi ya Dk.Ulimboka.
Tukio la Ulimboka ni kama jeshi la polisi limeinua mikono kwani Inspekta Mkuu wa Polisi (IGP), Said Mwema, aliwahi kusema mbele ya wakuu wenzake wa mataifa mbalimbali kuwa ni siri ya taifa.

Dk. Ulimboka mwenyewe baada ya matibabu yake nje ya nchi, hajawahi kuhojiwa na jeshi la polisi licha ya kukaririwa na vyombo vya habari akimtaja mtumishi moja aliyedai ni wa Ikulu akidai alihusika kumteka na kumtesa.

Wakati huo huo, Mungulu alisema kuwa upelelezi wa kumwagiwa tindikali kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha, katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga mkoani Tabora September 2011, upo katika hatua za mwisho.
Alisema ingawa watuhumiwa wawili tayari wamefikishwa mahakamani, endapo watapatikana wengine zaidi nao watafikishwa huko.
 
Kuna uwezekano hao watekaji hawatakamatwa kama tutaendelea kulisubiri jeshi la Polisi kufanya hivyo. Ni miezi kumi toka kutekwa kwa Dr Ulimboka na mpaka leo watesi wake hawajatiwa mbaroni. Ni zaidi ya mwezi na nusu toka Kibanda kutekwa na kuumizwa hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa. Matukio mengine ya ujambazi wahalifu hukamatwa ndani ya siku tatu tu.
Niwasihi waandishi wa habari za uchunguzi wafanye uchunguzi wao huru ili kitendawili hiki kitegulkiwe. Ninaamini kuwa Investigative journalists tulionao wakiamua kuifanya shughuli hii seriously majambazi hawa watajulikana ndani ya muda mfupi tu. Kama Polisi wameshindwa au hawataki kutimiza wajibu wao, ni imani yangu kuwa Waandishi hawatashindwa wakiweka nia.
Najua it's an uphill task, lakini penye nia pana njia!
 
Hivi lile suala la yule Mkenya aliyekamatwa kwa tuhuma za kumteka Ulimboka limeendeje? Nakumbuka kumuona Kamanda Kova akielezea kwa kirefu kwenye TV jinsi walivyomkamata mtuhumiwa huyo.
 
Waliokamatwa na video ndio waliomtesa uli na kibanda...taarifa zinaonyesha hivyo
 
Mtuhumiwa wa ugaidi aliyekuwa anapokea maelekezo kwenye video ya lwakatare, baada ya kufanikisha utekaji wa kibanda, aliamua kujiteka ili kupoteza ushahidi...hadi sasa r.b aliyochukua kituo cha polisi imebainika kuwa ni magumash yaani feki
 
Ukiiangalia na kuisikiliza ile video kwa makini inasikitisha sana..yaani kumbe kuna watu humu nchini wana roho za kinyama sana
 
Sasa naanza kuamini kuwa kuteswa kwa Ulimboka na Kibanda ndiko kutakakoleta ukombozi wa Nchi , Dah ! Kweli nimeamini damu ya Mtu ni Hatari sana ! Maana kuna watu wanaishi kama Digidigi kwa sababu ya mambo haya ! Stay Tuned !
 
Hivi lile suala la yule Mkenya aliyekamatwa kwa tuhuma za kumteka Ulimboka limeendeje? Nakumbuka kumuona Kamanda Kova akielezea kwa kirefu kwenye TV jinsi walivyomkamata mtuhumiwa huyo.

Yalikuwa ni makosa ya kiufundi kwa upande wa Kamanda Kova. Nafikiri anajuta kwa nini alikwenda mbele ya Waandishi wa habari akiwa half-cocked!
 
Ninawasiwasi na umaahiri wa jeshi la polisi pamoja na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Utendaji wao unatia mashaka kutokana na kujihusisha sana na masuala ya kisiasa hasa kujaribu kutweza fikra mmbadala.
Wamekua wakiendekeza usanii na uongo uliopitiliza. Wameshindwa kufanyia kazi mambo ambayo yanaikera jamii na kujikita katika kujaribu kuwanusuru waovu waliopo katika kundi dogo linaloiharibu nchi yetu.
Kutekwa na kuteswa kwa Dkt Ulimboka ni miongoni mwa masuala ambayo jeshi la polisi halijaonyesha nia ya dhati ya kulishughulikia kitu kinachoshawishi kuwa hawa jamaa wanaujua mpango huu na hawataki aliyehusiaka afahamike hadharani. Gazetu la Mwanahalisi lilijitolea kutoa mwanga wa nani hasa anahusika lakini cha ajabu hawakupenda msaada huu na badala yake wakalifungia. hili linafanana sana na kutekwa na kuteswa kwa Kibanda.
Katika tukio la mauaji ya padri kule Zanzibar kumekuwa na maelezo yanayotia shaka sana kwa mtu mwenyeakili timamu kuyaamini. Mimi binafsi siamini yale maelezo ya kuwa FBI walihusishwa katika upelelezi wa muuaji wa padri kwani utendaji kazi wa FBI ninaufahamu na haufanani kabisa na ile FBI ya kisanii iliyopelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya padri.
Kama vyombo vya dola vitaendea hivi kuna hatari ya kuliingiza taifa letu katika janga kubwa zaidi ambalo itachukua muda mrefu na rasilimali nyingi sana katika kulishughulikia. Wako wapi viongozi wastaafu wazalendo katika kulikemea hili?
 
Back
Top Bottom