Kwa takribani wiki nzima wakazi wa Nyegezi, Mwanza wamelazimika kuchota maji mitaroni baada ya huduma ya maji kukosekana kabisa bila taarifa yoyote kutolewa.
Cha kushangaza, ni baada ya malalamiko ya wananchi kuibuka ndipo Mwauwasa walitoa tangazo kupitia akaunti yao ya mitandao ya kijamii, wakidai kuwa kuna matengenezo yanayoendelea kwenye chanzo cha maji ambacho Mheshimiwa Rais alizindua miezi michache tu
Hali hii inaleta maswali makubwa:
Je, mitambo mipya hii tayari imeharibika au ilikuwa chakavu tangu mwanzo?
Kwa nini wananchi hawapewi taarifa mapema bali wanateseka kwa siku nyingi?
Wananchi wanalipa kodi na wanastahili huduma bora. Hii ni dharau kubwa na ishara ya uzembe wa kiutendaji.Mwauwasa imekuwa ikilalamikiwa mara nyingi na sasa tatizo limeonekana kuwa sugu.
Kwa sababu hiyo, watendaji wa Mwauwasa mnapaswa kujiuzulu mara moja.