Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Mimi kampuni yangu ya gesi ni moja tu Oryx hizo kampuni nyingine sijawai kuziamini kabisa na sijawai kusikia kuwa kampuni ya oryx wanachakachua miaka mianane nipo na oryx yangu nyingi endeleeni na uzalendo wa kutumia magesi mengine
 
KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika zaidi ya kuteua na kutengua tu.pole yetu
 
Kampuni zote Zina ubabaifu nakumbuka nlikuwa natumia Mihan gas mara ya kwanza ikawa inadumu ila kadiri siku zinavyoenda siku zikawa zinapungua ! Nikamwambia wife hizi gesi watakuwa hawaweki kilo SAHIHI
Mihan gas ndio hawahawa Taifa Gas mkuu, walibadilisha jina tu! Kumbe ujanja-ujanja walianza zamani.

Vv
 
Awamu imessbabisha matepeli na wezi Kila kona
 
Pole Kwa kuchelewa kujua,Kwa taarifa yako hata oryx wanapiga.
 
Pia hio mizani huwa inachezewa, inakuonesha kilo nyingi kumbe imesogezwa mbele
 
Pia hio mizani huwa inachezewa, inakuonesha kilo nyingi kumbe imesogezwa mbele
Hicho ni kitu kingine, muhimu ni kuwa unaponunua gesi ipime, kama ni kilo 15, pima na uchukue mtungi ambao una-tally na mzani.

Vv
 
, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.

Vv
Cheap Brand Wars
 
Rostam hajawahi kuwa rahisi hivyo lazima kashirikiana na juha yule kutuumiza
 
Hakuna Nia ovu Wala Nini yeye anapoiba Huwa ana Nia njema? Kikubwa awe amesema ukweli tu basi.

Shida ya wabongo hawaridhiki na huenda hata hiyo mizani nayo imekeketwa vilevile yaani Kila kona tunabinywa.

Mimi Huwa natumia oryx. Mwanzo nilikuwa na kale ka mtungi kadogo ka taifa sikulijua hili. Leo Leo naenda kubadirisha nikikuta Hivi naleta uzii mrefu mnoo.

Wizi wowote upingwe na kila aliye hai na akiri sawa
 
Shida ya wabongo hawaridhiki na huenda hata hiyo mizani nayo imekeketwa vilevile yaani Kila kona tunabinywa
Wale wanaokamua pump za Mafuta kwenye vituo vya mafuta....unakuta bodaboda mida ya saa 6 mpaka 8 usiku wanavizia hayo yaliyokamuliwa na yakiwa yamewekwa kwenye chupa za Maji zilizotumika? Tunawaweka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…