Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Hapa ninaponunu ni home boy wangu, niliposikia agizo la serikali kuwataka wauza gesi waweke mizani ya kupimia nilimtahadharisha na akalifanyia kazi.

Vv
 
Alete ushahidi gani wakati ni wengi wanalalamikia huu wizi? Mamlaka husika ndizo zenye jukumu la kufuatailia na kupata ushahidi. Hata mwenye kampuni anatakiwa afuatilie na siyo mteja. Kama anasubiri apelekewe ushahidi aendelee kusubiri tu lakini ajue wateja atawapoteza.
 
TBS na Watu wa taasisi ya vipimo na mizani waingie kazini haraka

Waende na mizani yao kila kona ya nchi kwa kuvamia maduka ghafla wapime
Kwa serikali ipi mkuu?
 

Yeye kahimiza watu watumie mizani wakati wanainunua. Hamna conflict of interest hapo. Wewe yule au mm tunaweza thibitisha asemacho popote tulipo kwa kutumia mzani kwa kila nunuzi
 
TBS na Watu wa taasisi ya vipimo na mizani waingie kazini haraka

Waende na mizani yao kila kona ya nchi kwa kuvamia maduka ghafla wapime
Yaani wamdhibiti mfuasi, mwanamikakati na mfadhili wa CCM? Mmiliki ana wajibu wa kimaadili kwa wateja wake, atimize wajibu vinginevyo tutamkimbia na kampuni itakufa.

Vv
 
Mkuu mbona nimeleta ushahidi kuwa ninatumia, nimefanya utafiti na nimeshapima mara kadhaa? Unataka nikuletee ushahidi nyumbani kwako? Wewe unayepinga ushahidi wangu una jukumu la kukanusha kwa kufanya utafiti pia. Nenda kwa muuzaji na chukua mitungi mitatu uipime uone kama tuhuma zangu ni uongo.

BTW bado natumia Taifa Gas, nachofanya ni lazima niipime na kuchukua mtungi wenye ujazo sahihi.

Vv
 
.... NDIYO HABARI YA MJINI. KATAA UTAPELI WA .....
Ninachokiona hapa nimeisha kieleza lakini hutaki kukuelewa.

Umetoa mfano wa ufisadi. Kama Kuna ufisadi mahali; ninachojua hatua zinachukuliwa ni mtuhumiwa ama kusimamishwa kazi na wakuu wake wa kazi ili uchunguzi ufanyike ( uchunguzi wa kupata ushahidi, msisitizo ushahidi)ama ukamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande kisha polisi ukusanya ushahidi; ushahidi ukitimia mtuhumiwa upelekwa Mahakamani kwa mashtaka.

Vivyo hivyo, na kwa yule aliyesimamishwa kupisha uchunguzi ripoti ya uchunguzi ikitoka na ikawa na ushahidi wa kutosha basi upelekwa Mahakamani kwa mashtaka.

Sasa mkanganyiko wa ninyi Wakuu kukataa kutoa ushahidi ili hawa wahujumu wateja kwenye huduma mnautoa wapi???

Umenipata lakini, Mkuu.
 
Siku hizi Wana mtindo mmoja ukihitaji kubadilisha wanakuletea mtungi wa gesi mpaka unapoishi na ni free of charge ww ni kupiga simu tu sasa hapo lazima Kuna upigaji tu.

Naomba kufaamishwa vizur unajuaje mtungi wa gesi kwamba umechakachuliwa?
Hii mbinu ni nzuri sana.
 
Yeye kahimiza watu watumie mizani wakati wanainunua. Hamna conflict of interest hapo. Wewe yule au mm tunaweza thibitisha asemacho popote tulipo kwa kutumia mzani kwa kila nunuzi
Asante sana mkuu, wewe umesoma vizuri kwa utuo na kituo, hujakurupuka kunijibu.

Vv
 
Mamlaka husika ndizo zenye jukumu la kufuatailia na kupata ushahidi.
Unajua Mkuu nipo upande wako sema haujanipata. Yaani hapa, kama tumedhamilia kuondoa hujuma hii dhidi ya haki ya Huduma kwa mTeja, tunatakiwa kutoa ushahidi usiotiliwa shaka wa uwepo wa hujuma hii ikiwezekana kwa Mamlaka ama mtoa huduma ili hujuma hii ikomeshwe.

Mamlaka, ndiyo ni wajibu wake, lakini kwa nini tujicheleweshe kisubiri Mamlaka ijekukusanya ushindi yenyewe wakati sisi tunaweza kufanya kazi hii kwa haraka?

Nadhani hapa umenielewa.
 
Kuna mawili, ama uandishi wangu mbovu, ama umesoma bandiko langu kwa hasira baada ya kusoma Aya ya kwanza ya bandiko inayohoji kama una mgongano wa kimaslahi katika Biashara hii ya gesi.

Kama utatulia, ukasoma vizuri bandiko langu, endapo tu ulilisoma kwa hasira mara ya kwanza, basi utapata maelezo ya kutosha juu ya ni ushahidi wa namna gani nimependekeza uulete hapa jukwaani.

Asante Jioni njema.
 
Tutumie oryx tu kwa kweli
 

Taifa gas ni wahuni
 
Kampuni zote Zina ubabaifu nakumbuka nlikuwa natumia Mihan gas mara ya kwanza ikawa inadumu ila kadiri siku zinavyoenda siku zikawa zinapungua ! Nikamwambia wife hizi gesi watakuwa hawaweki kilo SAHIHI
 

Acha hizo , hutaki watu waongee kisa kila mtu muhuni?
 
Ni kweli aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…