Wateja Wa Embe Aina Ya Apple Karibuni Sana

MzaramoTz

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2017
Posts
1,873
Reaction score
3,096
Habari zenu wakuu.

Natumai mnaendelea vyema kabisa na ujenzi wa Taifa letu pendwa.

Tunakaribisha wateja wa embe aina ya apple kwa kiwango kikubwa. Kama una hoteli au mgahawa hizi embe zinafaa sana kwa juice.

Tunazo embe mbivu na mbichi itategemea na mahitaji ya mteja. Embe ni kubwa na nzuri kabisa, pia tunampelekea mteja mahali alipo bila ya kulipia gharama ya usafiri ila kuanzia idadi ya embe 50.

-Embe mbichi bei ni 800 tukimpelekea mteja alipo. Ila akija kuchukua shambani/ofisini bei inapungua na kuwa 700 kwa embe moja.

-Embe mbivu bei ni 700 tukimpelekea mteja alipo. Ila akija kuchukua shambani/ofisini bei inapungua na kuwa 600 kwa embe moja.

Delivery tunafanya kuanzia embe 100 na kuendelea. Na hii ni kwa wakazi wa Dar-es-salaam pekee.

Karibuni Sana.







 
Mmmhhhhh,
Yaani Tshs 700/= kwa embe moja??
Tena hapo ndio Bei ya Jumla??
Ngoja waje

Mkuu, usihofu kuhusu bei kiongozi wangu bei inapungua tu kulingana na idadi ya embe anazohitaji mteja kiongozi.

Mawasiliano yapo hapo juu, tupe idadi ya embe unazohitaji then tuelewane ili tufanye biashara mkuu wangu.

Thanks.
 
Kuna mtu anatafuta dodo kwa wingi sana

Karibu sana spray.

Unaweza kunitumia message humu au kwa namba yangu whatsapp. Au hata ukini-beep ntakupigia usjali ili niweze kuskiliza hitaji lako kiongozi.

Karibu sana mkuu.
 
kweli dar maisha magumu hizo embe ni mia saba??wakati huku kwetu hadi tunalishia ng'ombe
Unachosema kinaweza kuwa ni sawa au sio sawa ndugu.

Na ndio mana utakuta kuna sehemu watu wanavaa nguo zilizochanika na zisizofaa lakini wengine nguo nzima kabisa anapigia deki kiongozi.

That's the way life goes mkuu. Karibu.
 
Biashara ya embe ni nzuri Japan.
Hapa tunanunua ¥500 / $5 kwa dodo moja. Maembe yanatoka Ufilipino, Peru na Mexico.

Nakushauri uweke contact zako na picha kama ulizoziweka hapa katika site ya alibaba.com.

Pia, wasiliana na JETRO JETRO | Japan External Trade Organization ili wakupe mwanga zaidi namna ya kuuza embe zako huku.

Pengine wana ofisi zao Tanzania au katika ubalozi wao.

Good luck.
 
kweli dar maisha magumu hizo embe ni mia saba??wakati huku kwetu hadi tunalishia ng'ombe
Kwa hiyo kulisha ng'ombe ni sawa? Nakumbuka juzi juzi wakulima wa korosho mikoa ya kusini walipata bei nzuri wakawa wananunulia mbuzi soda na kuzinywesha. Akili zetu tunazijua wenyewe
 
Thanks a lot mkuu.

Watu kama hao wanahitaji majibu mazuri na ya kiungwana kabisa mkuu na wala sio harsh words.

Kwa sababu kiuhalisia a coin has two sides. And each side is distinct mkuu.

Thanks a lot kiongozi.
i love the way you behave! you deserve many thanks!
 
Thanks a lot mkuu.

Watu kama hao wanahitaji majibu mazuri na ya kiungwana kabisa mkuu na wala sio harsh words.

Kwa sababu kiuhalisia a coin has two sides. And each side is distinct mkuu.

Thanks a lot kiongozi.
Unajua biashara, piga kazi kiongozi
 
Sie wa mikoani mzigo unafikaje
Karibu mkuu.

Kwa walio mikoani tunatuma mzigo kwa kutumia mabasi yanayoenda mkoa husika mkuu.

Malipo, Kama una mtu hapa Dar Es Salaam unaweza kuongea nae kwa ajili ya kufanya malipo kwetu ili kurahisisha zoezi kikamilifu.

Kisha sisi tunachofanya tunakupelekea mzigo wako mpaka kwenye ofisi za basi utakalotumia kusafirisha mzigo wako bila ya gharama yoyote ile ya usafiri.

Karibu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…