Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
Tumekuwa tunasikia malalamiko mengi sana kutoka kwa wadau wanaotumia huduma za ttcl mobile na broadband kwamba pesa zao zinaenda sana wakitumia mtandao haswa wale waliounganishwa moja kwa moja angalau hawa wenye kudial .
Wengi wa watu hawa wakienda ttcl kwenyewe nafikiri wanashindwa kupewa msaada wa uhakika jinsi ya kutumia computer zao uzuri ili wasipoteze pesa nyingi zaidi .
Kama wewe ni mmoja wa wadau na unasikitika kwa kutumia hela nyingi kwa ajili ya kutumia mtandao tu , fuata hatua nitakazosema hapo chini nina uhakika itapunguza gharama hizo kwa kiasi kikubwa .
AUTOMATIC UPDATES .
Kila siku katika mtandao kuna kuwa na maongezeko ya patches kadhaa zinazotakiwa kuwekwa katika computer yako , sasa unapojiunga tu kama unatumia windows basi itajiunga moja kwa moja na mtandao wa Microsoft ili kupata hizi updates .
Unachotakiwa ni kudisable automatic updates
1- Right Click My Computer
Ondoa hiyo tiki halafu apply ok , wakati mwingine unaweza kutumia programu ya autopatcher ambayo inakuwa na update hizi au unakuwa na programu maalumu kwa ajili ya updates .
Kumbuka sio update zote ni muhimu kwa ajili ya matumizi yako ya kila siku ya computer .
ANTIVIRUS UPDATE
Antivirus nyingi zinahitaji updates za moja kwa moja mfano Norton definition yake kwa sasa ni mb 18 mcafee ni mb 23 na zinazidi kuongezeka kila kukicha ili kuweka computer yako salama zaidi , sasa ufanye nini ?
Kama unataka updates za antivirus ni bora uende katika internet cafes , watoa huduma wengi wanakuwa na hizi updates au wanajua njia za kuzichukulia , unabeba na flash kisha unaenda kuweka katika computer yako .
Ukisema utumie hiyo ttcl kudownload unakazi kubwa kwa sababu spidi yake ni ndogo sana pesa zako zote zitaisha na hautapata hiyo update unayoitaka .
Mfano mb 1 unalipa shilingi 70 sasa unataka mb 23 x 70 = 1670 , ukichanganya na mwendo wa kudownload utaona unatumia zaidi ya alfu 4 hapo bila kupata kitu .
Hiyo ni vitu viwili vinavyomaliza pesa zaidi ingiwa kuna programu zingine ambazo nazo zinahitaji updates za mara kwa mara kwahiyo wewe kama mtumiaji unatakiwa uweke zile programu unazofanyia kazi tu katika computer yako zile ambazo hazihusiani na shuguli zako unatakiwa uzifute .
Au unaweza kudisable zisiwe zinafanya kazi mpaka pale unapoamua wewe kuzitumia
1 Start Run andika msconfig
Kuna kitu kama hichi kitakuja system configuration utility
Programu zinazoonekana zote ziko katika taskbar kwahiyo ondoa pata katika programu zote ambazo hupendi zifanye kazi kama huna kazi nazo kama acrobat reader , nero , na programu zingine ambazo huwa zinastart moja kwa moja .
TTCL MOBILE WENYEWE
Ni vizuri ttcl mobile wenyewe waweke mirror katika tovuti zao au link maalumu ambazo wateja wao wanaweza kudownload baadhi ya hizo updates kwa urahisi zaidi ili kuwapunguzia wateja hawa gharama kubwa na ufanyaji kazi wao uwe rahisi zaidi .
Huo ni ushauri wangu tu , wewe kama mtumiaji una haki ya kutokufuata ushauri na mawazo yangu kama unaona hauna manufaa au hauwezi kubadilisha gharama katika matumizi yako ya mtandao .
ONYO :
Unatakiwa uonane na mtaalamu wa mambo hayo anaweza kukusaidia zaidi usijaribi kitu ambacho hujui au huna uhakika nacho haswa katika hatua ya pili ya startup unaweza kuleta madhara kwa programu zingine katika utendaji wake wa kazi .
Nakaribisha maswali zaidi kutoka kwa wadau mbali mbali , naamini tunaweza kuboresha huduma hizi kama tukiamua kushirikiana na kupashana habari hizi kwa uwazi zaidi
Andika kwa email hapo juu au simu +255 784 360204 lakini kumbuka sifanyi kazi TTCL wala sina uhusiano wowote ule na TTCL mimi ni mdau kama wadau wengine wengi .