Wateja kununua vifaa kwa kampuni zinazotoa huduma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wateja kununua vifaa kwa kampuni zinazotoa huduma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zero, Feb 3, 2009.

 1. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Hii sijui kama inafit kwenye jukwaa la siasa, lakini naona imekaa kisiasa zaidi na inagusa maslahi ya umma.

  Kuna huu utaratibu wa kampuni nyingi za umma kuwauzia wananchi vifaa ambavyo vinahusiana na huduma wanayotoa na vile vile kuwatoza malipo kwa huduma yenyewe.

  Nitatumia mfano wa kampuni za simu, shirika la umeme (TANESCO) na upande wa maji ni DAWASCO. Mimi naamini, nikiwa kama mteja wa kampuni fulani ya simu, nisingepaswa kuuziwa simcard, maana hiyo ni nyenzo yao wao ya kuniwezesha mimi kutumia huduma yao na kuilipia kila ninapoitumia. Hapa sioni hoja ya mimi kununua simcard. Maana mwisho siku nikiichoka kampuni yao, sina pa kuipeleka simcard zaidi ya kuitupa.

  Vivyo hivyo kwenye upande wa umeme. Ni kwanini mteja alipishwe gharama za nguzo, waya na meter pale anapotaka kuwekewa umeme kwenye jengo lake ilhali mteja huyu atakuwa analipia gharama za umeme kila anapotumia? Hapa pia mimi sioni hoja.

  Napongeza upande wa DAWASCO kwa kutoa meter zao bure. Kwa upande wao, kama mteja hudai ankara yoyote ya nyuma, basi unapewa meter ya maji bure pamoja na fundi wa kufanya installation bure. Makampuni mengine yaige mfano huu.

  Najua mifano wa huduma za aina hii ni nyingi, na wadau mnaweza kutoa mifano mingi zaidi na zaidi. Hoja hii inagusa maslahi ya watanzania wengi maana bei za huduma hizi ni ghali sana. Kwa upande wa TANESCO, gharama za kufunga umeme ni ghali mno. Wananchi wengi vijijini wanashindwa kupata huduma hii muhimu kutokana na ughali wake. Mimi nadhani TANESCO wangeliangalia hili na kuona kama changamoto kwao ya kuongeza mapato kwa kuwafikishia watanzania wengi huduma hii kwa gharama nafuu.
   
 2. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naomba maoni yenu wadau!
   
 3. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kufanya biashara kibiashara ni pamoja na kuhakikisha kila kitu unachompa mteja unakiuza tena kwa faida.

  Kampuni za simu hazitengenezi simu za mkononi wala hizo sim card za namba wao huzinunua toka kwa wazalishaji ambao ni makampuni mengine.Hawawezi kumpa mteja bure.Ndio maana wanaziuza.

  Tanesco pia Nguzo na nyaya na vifaa wanavyofunga kwa wateja hawazalishi wao.Wao hununua toka kwa wengine.Ndio maana nao huwauzia wateja wanapowafungia ili warudishe gharama walizonunulia waweze kuendelea kufungia wateja wengine.

  Kusema watoe bure sababu unalipia kila mwezi si sahihi mfano wametumia shilingi milioni moja kuleta nguzo za umeme na nyaya na vifaa kwenye nyumba ya mtu ambaye amefunga balbu mbili tu za umeme nyumbani mwake kubana matumizi ambaye analipa shilingi 1000 kwa mwezi kama bili yake ina maana Tanesco watachukua miezi elfu moja au miaka 83 kurudisha ghara zao za kumfungia umeme huyo mtu bila faida.Hiyo itakuwa ni biashara kichaa ambayo hata kichaa hawezi kuifanya.Ndio maana wanapofunga umeme wanakudai hapo hapo ulipie kila kitu mmalizane hazta kama utafunga balbu mbili au utaacha kutumia umeme wao wao wasiwe na hasara yoyote.Kama kuna unaosema wanatoa bure si kweli.Wafanyabiashara ni wajanja mno yawezekana wanakubambika kwenye bili yako ya kila mwezi utajijua huko siko.
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Netanyahu, Salute bro!

  Hapa hoja ya msingi sio kwenye uchangiaji wa gharama. Hoja hapa ni ule mzigo anaobebeshwa mteja katika hatua za awali tu za kutaka kujipatia huduma. Nitakupa mfano rahisi. Kwenye biashara ya daladala au mabasi ya abiria kwa ujumla, watu wanalipa nauli kulingana na umbali wa safari zao. Mmiliki wa basi anakusanya kidogo kidogo kwa miaka kadhaa mpaka kufikia kurudisha mtaji wake na kuanza kupata faida. Hapa utaona kwamba mmiliki wa daladala sio mtengenezaji wa daladala, mafuta wala vipuri vya daladala. Tulitaka na TANESCO na haya makampuni mengine kuondoa hizi gharama za "installation" na kuziingiza kidogo kidogo kwenye monthly charges ili kuondoa mzigo kwa wateja.

  Sio kweli kwamba kila mteja mmoja anatumia nguzo moja na nyaya pekee yake. Ukiangalia katika maeneo mengi, hivi vitu ni shared. Utakuta nguzo moja inatumiwa na wateja hata mpaka kumi. Kwenye maeneo ya "slums" nguzo hii yaweza kutumiwa na idadi zaidi ya hapo. Kwahiyo suala la kwamba wao hawatengenezi nguzo na nyaya, sio hoja ya msingi. Wao waweke gharama zao za ankara katika hali ambayo mteja atalipia kidogo kidogo hizo gharama za installation without feeling the pinch.

  Tunasema tunataka maendeleo vijijini ilhali wananchi huko hawawezi kupata huduma muhimu kama umeme nk. Imefika sehemu sasa serikali kuona hali hii na kuitafutia ufumbuzi. Hili sio kwa TANESCO tu, bali kwa makampuni yote yanayotoa huduma na kuwatoza installation charges wateja wake.
   
 5. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ok Zero kuhusu kupeleka huduma kama za umeme na simu bila kuchaji gharama kubwa TTCL waweza toa data nzuri sana.Nakumbuka kipindi fulani Msuya akiwa waziri alipigania sana simu ziwekwe hadi vijijini kule Upareni Kwenye jimbo lake la uchagguzi.Na kweli nguzo na nyaya na simu zikafungwa kwa maelezo kama hayo yako uliyotoa kuwa watalipia kidogo kidogo hadi kurudisha gharama za kufungiwa huduma hizo.

  Wazee wengi wa upareni wenye watoto wafanyao kazi sehemu nyingi za Tanzania wakafunga simu kwenye nyumba zao.Matokeo yake simu zile zilikuwa wakizitumia tu kwa kupokelea simu zinazopigwa na watoto walioko Dar es salaam na mikoa mingine.Sehemu kubwa ya simu zilikuwa hazitumiki kupiga bali kupokea tu.Shirika lilipata hasara kubwa.Sidhani kama walili-cover cost zao za ku -install miundo mbinu ya simu hadi leo.Waweza tueleza uzoefu wao wa vijijini.

  Anyway sipingi wazo lako Zero cha msingi tuangalie maslahi si ya wananchi tu lakini pia ya mtoa huduma ili aendelee kuitoa kwa ufanisi.Tuhakikishe kunakuwa na balance .Na kila upande uridhike.

  Wazo lako zuri ila linataka wataalamu wa CBA (COST-BENEFIT ANALYSIS) wakae wafanye mahesabu na analyisis zao kujua kama hilo wazo ni viable na linafaa kibiashara na kiuchumi na katika kuhakisha utoaji huduma bora endelevu.Mimi hilo si eneo langu labda wataalamu wa fani hiyo kama wapo humu watusaidie.Na mimi hapa naongea tu kama muwazaji fikirika.

  Vinginevyo I salute you Zero wewe ni mtetetezi mzuri wa wananchi wanyonge wakiwemo wa vijijini wenye kipato cha chini wanaohitaji huduma bora zikiwemo za maji,umeme na simu.KEEP IT UP.
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Kuna mantiki ya hoja yako lakini umeharibu hapo ulipowasifu DAWASCO kwani sielewi wanafanyaje kazi zao, maji siku hizi sio zamani Dar imekuwa Chalinze na Chalinze imekuwa Dar, je tunakwenda mbele au tunarudi nyuma? nyumbani kwangu ujenzi wa barabara wamenikatia maji huu mwezi wa nane hawajaunga bomba langu lakini kila mwezi wanatuma bill ya matumizi ya maji, Zero futa usemi wako mara moja la sivyo nitachomokea kwenye screen yako
   
 7. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Thanks Netanyahu,

  Kama kumbukumbu zangu ziko sawa nakumbuka kuna gharama huwa zinaitwa "service charges" ambazo mteja wa TTCL huwa anawekewa kwenye ankara yake hata kama hajatumia huduma yao. Kwa upande wa TANESCO hili pia liko hata pale unaponunua LUKU. Kuna mwezi utakwenda kununua umeme na utapata "units" kidogo, eti wanakuambia ulikuwa hujakatwa "service charges" kwa muda mrefu. Sijui kama wenzangu hili limeshawakumba, lakini mimi nimeshakumbana nalo.

  Kwenye suala la ulilotaja hapo la CBA, nadhani uko sahihi kabisa. Sisemi kwamba hawa watoa huduma wapeleke huduma pale ambapo haina wateja au wateja wataitumia katika hali ya chini (japo ni haki ya kila mtanzania kupelekewa huduma za kimaendeleo). Kila kampuni ina haki ya kufanya CBA, lakini isiwe ni katika hali ya kuwaumiza wananchi wa Tanzania wenye kipato cha chini. Nilitembelea kijiji kimoja huko mkoani Shinyanga ambapo TANESCO walifanya CBA na kujua kwamba wananchi wanahitaji huduma ya umeme. Wakapeleka nguzo na nyaya, lakini ilipofika kwenye gharama za "installation" wananchi wakashtuka. Maana waliambiwa ni zaidi ya shilingi laki tano kwa kila nyumba. Kwa maisha ya kijijini mtu kupata laki tano kwa mkupuo sio suala rahisi.
   
 8. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa nazungumzia ufanisi wao kwenye suala la meter. Hayo ya kukatiwa maji na miundo mbinu yao mibovu ni suala jingine kabisa. Nimetoa tu kama mfano utaratibu wao kuwapa wateja wa maji meter za maji bure.
   
Loading...