"Wateja hawaji kwa bahati mbaya, wanatafutwa"

"Wateja hawaji kwa bahati mbaya, wanatafutwa"

Max Marketer

Member
Joined
Oct 13, 2020
Posts
46
Reaction score
50
Habari za leo wakuu, natumai mu wazima na kila mtu anaendelea vizuri ktk harakati zake za biashara & ujasiriamali.

Leo ikiwa jumapili tulivu kabisa, baada ya mihangaiko ya wiki, appointments , nilitaka kuja kuendelea na mada yetu kuhusu kujifunza Facebook & Instagram ads,

Na jinsi unavyoweza kuzitumia kuongeza mauzo & wateja wa biashara yako

Lakini naomba leo nisiweke mada, Bali nishee kitu ambacho nimejifunza jana, nilivyokua napiga Story na mfanyabiashara mmoja apa Town, ana duka lake zuri maeneo ya sinza.

Tukiachana na story za hapa na pale, mada kubwa ilikua kuhusu maduka makali around the area

Yaani ukicheki watu wamefungua businesses, maduka mbali mbali,wamefanya investments za maana, wanalipa million kadhaa ktk kodi.

Lakini mbona hatuoni movements za wateja? , tukasema maybe wanauza online.

Lakini kuna sehem zingine mimi ni shahidi kabisa, kuna mdada alikua na bonge la duka la nguo, liko very classic.

Lkn wateja kuonekana ilikua nadra sana, mpaka mwisho naona frem inafungwa.

Jamaa akaongezea akasema biashara ya sasa hivi aiseeh, inabidi uwe umejipanga vzr ktk suala la kupata wateja..

HASA PALE unapofungua biashara mpya na haujatengeneza customer base yako.

Akatoa mfano yeye ana mteja wake huyo alimfata toka kigamboni mpaka sinza, for a very simple product ambayo hata feri tu kabla hajavuka angeipata.

Na hapo ni kwa sababu tu walijuana kupitia Instagram,..I was like aiseeh, kweli hii mitandao iko very powerful ktk biashara.

Tukakubaliana kama tayari unajulikana, ni rahisi kupata wateja zaidi, especially through refferals, unaambiwa tu "ukitaka kitu flani,nenda kwa fulani"

SIMPLE TU

Lakini kama ndo unaingia sokoni,.....hujajulikana,...mauzo yapo chini,
Huna wateja wa kutosha,bado online unahangaika,.....biashara haikui

Aiseeh usikubali hii hali, pambana kutafuta wateja na kujulikana within your target market, ili hata mtu akihitaji huduma akufikirie wewe kwanza, na si mtu mwingine.

Na hapa ndipo nikaona kumbe niendelee kufundisha & kusaidia watu about Social Media Marketing and Advertising,..

Sababu Ukifahamu vizuri kuimarket na kuitangaza biashara yako kupitia social media, you have a bright future...kitendo cha kupata wateja hakikupi changamoto tena.

Juzi nilikua na appointment na Mzee mmoja, amefanya investment kubwa, lakini as we all know wengi hawana ufahamu bado na ishu za social media marketing and advertising... Nikampa ABCs pale, tukafungua account na akaweza kurun ads, alifurahi kweli..

Nkasema doh, kweli ukiwa willing to succeed.. Nothing can stop you,.. Sasa Mzee nampa support and guidance, tunaenda bega kwa bega mpaka lengo litimie.

Tumeshafanya kazi kadhaa za matangazo, and more are on the way

Recently,nimeongea na wafanyabiashara tofauti tofauti walionicheki,.... Kuna umuhimu wa kufahamu hivi vitu kwa kweli

Ukishapima ROI (return on investment ) unayoweza kuipata kwa kuwekeza ktk matangazo.....na sio kwa kubahatisha, bali ukifata strategies zote muhimu, you should give this a try .

Guys strategies za kupata wateja ni nyingi, social media marketing, matangazo ya kulipia, Influencers,Content marketing, Traditional marketing, word of mouth marketing etc

DON'T SETTLE... do something for your business

Mimi niko ktk Social Media Marketing and Advertising.. Ukihitaji msaada hapo, nitafute whatsapp/call 0752226475,

Nitakusaidia pale ulipokwama,au kama unaanza na ungependa kupata mafunzo and knowledge.

*Tuendelee kuwa pamoja, lessons and tips za Jinsi ya kufanya ads zenye impact ktk Facebook and Instagram zitaendelea from kesho

TUAMBIZANE PIA, WEWE UNATUMIA NJIA GANI KUPATA WATEJA au WATEJA WENGI ZAIDI?

---------------

By: MAX MARKETER TZ

"Ideas that spread Win"

- Social media marketing | Facebook ads | Graphics design | Simple Web Design | Content Creation
 
Kuna biashara wateja watakuja tuu so iko hivyo in nature.

Mfano biashara ya kuuza jeneza wateja watakuja tuu.
 
Back
Top Bottom