Watch Lipumba Live on "Baragumu" la Channel Ten!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Wanabodi,

Wale wenye access, please watch Kipindi cha Baragumu now, kinachorushwa na Channel Ten, M/Kiti wa CUF yuko hewani Live akizungumzia issue mbali mbali ikiwemo kukemea vikali tuhuma za udini, ukabila na ukanda kwenye vyama vya siasa.

Endelea....
 
Amesema dhana ya udini, ukabila na ukanda zinaweza kuusambatatisha umoja wa kitaifa tulio nao Watanzania.
 
Ameulizwa CUF kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) inafuata ilani gani?. Prof. Lipumba hakujibu swali, amechenga chenge na watangazaji wetu hawa weupe weupe akaingizwa chaka bila kumsisitiza Prof. Lipumba hajajibu swali.

The fact is "CUF kwenye SUK inatekeleza Sera na Ilani ya CCM!"!.
 
Kuhusu Urais wa 2015, Prof. Lipumba amesema kila mwana CUF yuko huru kugombea urais kupitia CUF, akimaanisha yeye sio mgombea wa urais wa kudumu wa CUF, ila pia amebainisha kamwe hawezi kugombea ubunge, akisisitiza kugombea ubunge sio saizi yake!.
 
Prof. Lipumba alimalizia kwa kusisitiza utajiri wa mali asili za Tanzania, uwafaidie Watanzania wote!. Akasema licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa wa madini lakini utajiri huu hauwafaidii Watanzania kutokana na sera mbovu zilizopo zinazolindwa na sheria mbovu za mgawanyo wa rasilimali za taifa.

Akatoa msisitizo kuwa baada ya kupatikana kwa mafuta na gesi, Watanzania sasa tuamke, tuweke sera nzuri na kutunga sheria nzuri zitakazo fanya Watanzania wote wafaidike na rasilimali za Taifa!.
 
kielele tu!mapumba ni mapumba kila kukicha yeye tu mpaka watu tumemchoka na mauzo yake luningani!ccm B rest in peace
 
Back
Top Bottom