Watawala wetu wanatengeneza chuki katika Jamii yetu

Sidhani ata kama tunafanana na mfumo wa chama kimoja kwa sasa.Nadhanj ni kama tupo katika ukoloni.
Mnataka muachiwe kila mnalofanya. Mkitukana muachiwe na msiguswe
Mkitukana rais muachiwe msiguswe
Mkidhalilisha serikali mnataka muachiwe.
Hivi niulize hamuwezi kuendesha siasa za upinzani za kistaarabu mkajijenga mbele ya wananchi. Kwani ni lazima kuiga matabia ya ma nchi mengine ambayo amani kwao ni kama kitendawili.!? Tuache kuiga matabia ya kipumbaf.. kwa sababu hatujaweza kuwa na uthubutu wa kuyakabili matokeo yake yanapokuwa mabaya
 
Hivi wewe ni kipofu?

Hivi huoni namna hiyo mikutano ambayo Rais anayoiita ya kiserikali namna Rais Magufuli anavyoitumia kwa kampeni ya chama chake cha CCM kwa 'kuwananga' na kuwakejeli wapinzani?

Sasa ni kwanini wapinzani hawapewi fursa ya kujibu makombora yanayorushwa na JPM?

Nafananisha ushindani wa kisiasa wa CCM na wapinzani kwa sasa ni sawasawa ni kuwapandisha mabondia 2 kwenye jukwaa na bondia mmoja kumfunga na namba mikono yake yote miwili na k
Jibu hoja ni kwanini CCM kufanya mikutano ya kisiasa iwe halali na wapinzani kuwa haramu, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na vyama hivyo vinatakiwa kufanya shughuli zao bila kuingiliwa na chombo kingine chochote?
 
Kama kuna wakati wa kuiombea Tanzania basi ni sasa, kwani siasa ya nchi yetu inavyokwenda sipati picha kitakachotokea siku za usoni. Sidhani kama Tz mpya ya viwanda inayohubiriwa kwenye majukwaa tutaifikia kweli. Lakini ni aibu ilioje kurudi tuliko toka. Mungu atuepushie mbali na yanayo wakuta wenzetu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inashangaza mno watanzania wengi kuamua kukaa kimya wakati tunaona wazi namna Rais wetu anavyoamua kuisigina Katiba ya nchi yetu ambayo aliapa kuilinda na kuitii kwa kuzuia vyama vya upinzani visifanye shughuli zake za kisiasa wakati yeye na chama chake wanafanya shughuli zao za kisiasa bila kubughuziwa na vyombo vya usalama!
 

lakini tuwemakini na taifa letu pia ,kama mpinzani anaonekana ni adui i hatarii tena hatariiiiiiiiiiiii
 
with time people will find an alternative passively


siasa kwa yenyewe haina tatizo, tatizo kubwa ni watu kubadili siasa na kufanya yao kwa kisingizio cha siasa .kumbe wanasiasa ndo tatizo ,hasa wale wasioijua siasa wapolazimisha kisa tu wana nafasi flani hapo ndo shidaaaaaaaaaaaaa, siasa ni maelewano ,siasa halisi hujenga umoja ,siasa halisi hutokomeza visasi ,siasa halisi hujali utu wa mtu ...
 
Chuki ni kubwa sn,ashukuliwe mungu Ak47 hazipo mtaani vinginevyo ohooo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Bahati mbaya sana watawala wetu hawaioni hatari hiyo....

Badala yake kwa kuwa wanajiona ni kama 'wanavimiliki' vyombo vya dola, wanaviamrisha vyombo hivyo vya dola vinavyogharimiwa na wananchi kuwanyanyasa wananchi hao hao ambao kodi zao ndizo zinafanya vyombo hivyo vya dola kuwepo!
 
Si waliomba ridhaa wenyewe kututumikia?Hatukuwalazimisha kugombea.Ni kwa nini tusitumie haki yetu ya kikatiba kuhoji na kudadavua mambo ya mwenendo wa serikali yetu?
 
Si waliomba ridhaa wenyewe kututumikia?Hatukuwalazimisha kugombea.Ni kwa nini tusitumie haki yetu ya kikatiba kuhoji na kudadavua mambo ya mwenendo wa serikali yetu?
Kwenye mfumo wa kisiasa wa vyama vingi jinsi unavyofanya kazi ni kujibizana kwa hoja....

Ndiyo mfumo uliokuwa ukitumika kwenye serikali ya awamu ya 3 na 4

Sasa serikali hii ya awamu ya 5 imebadilisha mfumo kwa kujiona wao CCM ndiyo wenye haki ya kujibu hoja za upinzani.

Wapinzani nao wakijaribu tu kuzijibu hoja za CCM wanaitwa wachochezi na kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani na baadaye kufunguliwa mashitaka mahakamani!

Kama serikali hii ya awamu ya 5 haiutaki mfumo wa vyama vingi ni vyema ikapeleka muswada Bungeni wa kufuta mfumo wa vyama vingi na turejee kwenye mfumo wa chama kimoja, kuliko msteso na manyanyaso wanayopata wapinzani kila siku.
 
Sasa haya maneno siuwashauri Lumumba wenzako ??unawashauri upinzani ndo wanafanya huo ujinga ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Hii ndio comment yangu ya mwaka mkuu, upo sahihi kwa 10000000000000000000% mkuu
 
Hii ndio comment yangu ya mwaka mkuu, upo sahihi kwa 10000000000000000000% mkuu
Huo ndiyo ukweli.....

Kama kweli Mkulu anaamini Umma wa watanzania unampa full support na wapinzani wameishiwa Sera......

Ni kwanini basi ameingia woga wa kupitiliza kwa kutotaka kabisa wapinzani wafanye mikutano ya kisiasa?

Kwani yeye haujui ule msemo wa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?

Yeye aache vyama vyote vya kisiasa vinadi Sera zao kwa uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na wananchi wenyewe ndiyo wapambanue MCHELE ni upi na PUMBA ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…