Watawala wetu wanatengeneza chuki katika Jamii yetu

sasa hivi ni waziwazi kuhusu; ukanda, itikadi, ukabila nk
Yaani nchi inaendeshwa kwa ubaguzi wa waziwazi.

CCM kufanya mikutano ya kisiasa ya ndani, mikutano ya hadhara na hata maandamano ruksa....

Wakifanya Chadema, Polisi wanakuwa 'wapiga ramli' kuwa eti taarifa zao za kiintelejinsia zinawambia kutatokea uvunjifu wa amani!

Hawa Polisi kufanya kazi kama 'kitengo' cha CCM imesababisha wananchi wapoteze Imani yao kwa Jeshi hilo.
 
Hapa mimi naona chama tawala sehemu zote mapka 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini Katiba ya nchi ambayo Mkulu aliapa kuitii na kuilinda inatamka wazi kuwa nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi.

Sasa yeye Bwana Mkubwa anapata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati yeye na chama chake cha CCM wanafanya kampeni kila siku?
 
Hivi mkuu nani anatamfunga paka kengele walikuwa wa hawamaanishi paka na panya unaowajua wewe ila ndio kama mimi na wewe leo tunavyoona sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WALA HATUJARUDIA WANAJILAZIMISHIA TU ILA MAJANGA WANAYOYATENGENEZA NI YA KUDUMU HUU UTAWALA UTAFIKIA UKOMO LAKINI CHUKI ZETU HAZITATUTOKA KAMWE
 
WALA HATUJARUDIA WANAJILAZIMISHIA TU ILA MAJANGA WANAYOYATENGENEZA NI YA KUDUMU HUU UTAWALA UTAFIKIA UKOMO LAKINI CHUKI ZETU HAZITATUTOKA KAMWE
Very true.

Imagine na hiki kitendo cha leo cha Spika wa Bunge kuridhia kuwavua ubunge wabunge wanabe wa CUF kutokana na mapendekezo ya Mwenyekiti aliyejuzulu nafasi yake hiyo Profesa Lipumba nayo Inabidi kujenga chuki ndani ya jamii ya watanzania
 
Shida ni kwamba UVCCM wanakuwa wametumwa specifically kwenda kupiga wapinzani wakiwa kwenye mikutano au maandamano.Ni namna CCM ilivyolea vijana wake wamelelewa kwa kujenga chuki miongoni mwao na wapinzani
 
Kila uchwao wapinzani wanahakikisha wananchi hawaipendi serikali yao. wamesahau majukumu yao ya msingi katika majimbo yao wamehamia kuhakikisha kuwa nchi inavurugika kabisa.
 
Hivi mkuu nani anatamfunga paka kengele walikuwa wa hawamaanishi paka na panya unaowajua wewe ila ndio kama mimi na wewe leo tunavyoona sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii hali ya kumhofia Mkulu ndiyo inazidi kuiweka nchi hii kwenye hali mbaya zaidi.....
 
Kila uchwao wapinzani wanahakikisha wananchi hawaipendi serikali yao. wamesahau majukumu yao ya msingi katika majimbo yao wamehamia kuhakikisha kuwa nchi inavurugika kabisa.
Wewe mpiga debe wa Lumumba ngoja nikuulize swali moja, hivi wajibu wa vyama vya upinzani nchini ni nini?

Wajibu wao mkuu ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani ili ijisahihishe pale ilipokosea.

Lakini cha ajabu serikali hii ya awamu ya 5 wanajifanya miungu-watu wasiotaka kukosolewa kwa jambo lolote!

Wao wanajiona wako 100% perfect!
 
Sidhani ata kama tunafanana na mfumo wa chama kimoja kwa sasa.Nadhanj ni kama tupo katika ukoloni.
 
Mkuru anazngua xna bt finally awamu hii huenda ikapelekea kupotea kwa tunu yetu ya amani tunayojivunia daily.

Sent using Jamii Forums mobile app
It is true.

Kama wananchi tutaamua kukaa kimya kwa ukandamizwaji mkubwa wa demokrasia nchini, ambapo CCM kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano inakuwa halali wakati vyama vikuu vya siasa vya Chadema na CUF vinazuiwa hata kufanya mikutano ya ndani....

Hakika kama trend hii ya ubaguzi wa wazi unaoendelea nchini hautapigwa STOP, basi ni dhahiri amani yetu itakuwa ipo rehani....
 
Kamanda kama ni chuki labda uianzishe wewe. Unajua watanzania hatukuwa tumezoea utii wa sheria bila shuruti. Hapo ndio tatizo. Lakini pia unafananisha Magufuli na unamchanganya kuwa kama kiongozi wa chama tuu. Hivi unasahau yeye ni rais wa nchi.. ana uhuru usio na mipaka kama rais wa nchi. Anaweza simama popote akazungumzia masuala ya nchi. Na ndio maama amethubuhu hata kumtaja mbunge wa ccm kuwa arudishe viwanda ambavyo alibinafsishwa kwa manufaa ya taifa avirudishe.
 
Sidhani ata kama tunafanana na mfumo wa chama kimoja kwa sasa.Nadhanj ni kama tupo katika ukoloni.
Kwa sababu katika hali ya nchi yetu ilipofikia, hatupaswi tena kujiita tuko kwenye mfumo wa vyama vingi.....

Ni vyema tu serikali ya awamu ya 5 iutangazie Ulimwengu kuwa nchi yetu imerejea kwenye mfumo wa chama kimoja!
 
Badala ya kuzungumzia ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na baadhi ya vyama vya siasa mnavyovijua kwanza mnadandia gari kwa mbele kwa mambo ambayo hata ukiambiwa uthibitishe huwezi..kwenye vyama vile ukihoji kitu unafukuzwa. Ukihoji katiba unafukuzwa. Ukihoji matumizi ya ruzuku unafukuzwa. Ukihoji mapato na matumizi ya jumla unaambiwa msaliti umetumwa. Ukandamizaji huu hamuuoni au mmeamua kuziba masikio. Jengeni kwanza nyumbani kabla hamjaamia ugenini
 
Kwa sababu katika hali ya nchi yetu ilipofikia, hatupaswi tena kujiita tuko kwenye mfumo wa vyama vingi.....

Ni vyema tu serikali ya awamu ya 5 iutangazie Ulimwengu kuwa nchi yetu imerejea kwenye mfumo wa chama kimoja!
Hahahaha mmeshazoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi.. mmezoea siasa za kulelewa kama mayai, na kubembelezwa. Awamu hii msijidanganye. Itakula kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…