WATAWALA vs VIONGOZI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WATAWALA vs VIONGOZI!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lizzy, Jan 31, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nilipoanza kusoma makala moja iliyochapishwa ndani ya gazeti la Tanzania Daima siku mbili nyuma https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/217438-chadema-ndio-wamesababisha-mgomo-wa-madaktari-4.html#post3238962 nilijikuta najiuliza kama aliyeandika alikua akimaanisha au la. Maana mwanzoni nilielewa/dhani kwamba kwamba makala yenyewe inalenga kutuhumu na kuchafua CHADEMA ila matokeo yake yalikua ni tofauti kabisa. Ililenga kuonyesha ni kwa kiasi gani chama tawala kisivyo shughulika na kuwajibika kufanya yale wanayohitajiwa na wananchi kuyafanya kisha kulaumu chama pinzani(CDM) kwa kushindwa kwao.

  Na kutokana na lawama za mara kwa mara zitolewazo na chama tawala zikielekezwa kwa CHADEMA ni wazi kwamba CHADEMA ina ushawishi mkubwa sana kwa wananchi, tofauti na chama tawala, na wahusika wanalijua hilo. Ndio maana hawaishi kulalamika kwamba CDM ndio chanzo cha migomo na migogoro kati ya serikali na taasis mbali mbali pia wananchi hata kama sio kweli ili kujaribu kuondoa imani wanayopata CDM toka kwa wananchi.

  Wanasahau kwamba "Kiongozi hufuatwa, husikilizwa na hukubaliwa kutokana na ushawishi wake na kwa mapenzi ya anaeongozwa. Mtawala hutawala kwa lazima kutokana na nguvu, nafasi au mali mpaka pale hiyo misingi yake itakapoanza kuyumba na kukosa nguvu."

  Bila ya kumung'unya maneno niseme wazi kwamba Tanzania kwa sasa haiendeshwi na VIONGOZI bali WATAWALA. Viongozi ni hawa wanaolalamikiwa na watawala kwamba wanasababisha utendaji wa serikali udorore kwa kuwafanya watu waone makosa na matatizo yao. Malalamiko na vitisho kama vinavyotolewa kwa madaktari kwa sasa ndio haswa hatua ambazo huchukuliwa na 'watawala' pale wanapoona watawaliwa wanakataa kutawalika. Kwasababu hawana nguvu ya ushawishi wala imani ya watu wake basi lawama huelekezwa pale yalipo hayo.

  Muda umefika kwa chama tawala kufahamu kwamba wao sio viongozi ni watawala, na kwa kujaribu kulaumu makosa na matatizo wanayosababisha wao kwa chama kingine kunasaidia kuonyesha mapungufu yao wenyewe badala ya kuwasaidia. Mpaka watakapoamua hata ku-ACT tu kama viongozi, wategemee kupoteza watawaliwa zaidi.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mbona waliacha kuea viongozi miaka mingi iliyopita?
   
Loading...