Watawala hutenda mambo ya hovyo mno!

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Hebu Great thinkers nisaidieni kuelewa Saikolojia ya Watawala ilivyo...nini huwa kinapita kwenye vichwa vyao wanapofikia hatua ya kufanya maamuzi mbalimbali;Je,ni woga?

1. Nilikuwa napitia historia ya South Africa,zile sheria za kipuuzi kabisa za kibaguzi(Apartheid),nikawa najiuliza ni kitu gani huwa kinaendelea kwenye vichwa vya watawala hata waamue kutenda mambo ya hovyo kiasi hicho; Kuna nyakati utawala wa makaburu wa South Africa uliwaanzishia Waafrika weusi tawala feki zinazojitegemea -Bantustans - na wakawa wanadai kwamba hao si raia wa South Afrika bali ni raia wa "mataifa" ya nje,yan kwa mfano sisi tunavyowaona Wakenya,au Wakenya wanavyotuona Watanzani.

2. Nimejiuliza kwanini Watawala hufikia hatua hizo?Kwa mfano,CCM na Dr.Shein wanawezaje kirahisi tu kuamua kupindua matokeo ya Urais Zanzibar?Hawasomi historia - kwamba hakuna utawala uliopata kushinda Umma? Makaburu wa South Afrika pamoja na maguvu yao yote hatimaye walishindwa na raia maskini wa South Afrika waliopambana kwa mishale na mawe tu.

3. Nimejiuliza inawezekanaje kirahisi tu watawala wakaamua kudhibiti Bunge, nalo Bunge kweli likaufyata?Inawezekanaje watawala kwa mfano,wakazuia vyama vya siasa kufanya mikutano yao ya nje popote nchini?Hivi hawa watawala si ni binadamu wa kawaida tu?

4. Inawezekanaje watawala wakaamua ku-control media na kufanya censorship,wakati wanafahamu kabisa kuwa hatua hiyo itazaa migogoro isiyo na tija kwa taifa?Why?
 

Attachments

  • 200px-ApartheidSignEnglishAfrikaans.jpg
    200px-ApartheidSignEnglishAfrikaans.jpg
    10 KB · Views: 25
Back
Top Bottom