Wa tatu naye kanikataa! Nakosea wapi ndugu zanguni?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,215
56,855
Habari zenu watu?

Tukiachana na yule niliekuta kanisevu "KIBERENGE" nikapiga chini,nimeamua kusonga mbele japo bado nawasiliana nae kiaina ila hakomi kuacha kuniita hivyo akinitext tu utaona text "we kibe haujambo" inaniuma sana.. tuachane na hilo

Kuna pisi moja kali niliiandikia barua.. nilijipinda mtoto wakiume na mwandiko wangu wakulala nikijitahidi kuusimamisha lkn yote hayo hakuona binti yule!.. kwenye barua nikaweka na msimbazi mmoja ili kumshawishi kusoma muandiko wa komamanga mimi..! Lkn pamoja na yote hayo alinijibu kwa kuandika nyuma ya barua "SI DATE NA POSTA MIMI!" kilichoniuma zaidi pesa alichukua hakurudisha!.
Nikaachana nae japo sikulala siku tatu mpk mbu walinizira kuniuma nafikiri hata wao pia walikuwa wakinione huruma!..

Wapili huyu alikuwa mpole nikaona hapa nimepata toto moja zuri.. nikabadili mbinu nikaona nitumie face to face approaching nisijeitwa tena posta!,so nikaanza mazoezi ya kumtongoza nikaandika na essay kabisa nikaimeza kichwani.. nikaenda mcheki sasa asalaleee lile jicho lake tu lilitosha kunisahaulisha essay zote nilizokuwa nimemeza! nilikuwa nakumbuka kabisa baada ya kumwambia "Mambo mrembo? Then ningemwambia umependeza!"

Baada ya hapo ndo ningeanza tiririka lkn dah! Niliishia kumuuliza tu kwenye kampeni za CHAUMA utaenda kula ubwabwa!! Mpk alinishangaa.. sijui kichwa kilipata shida gani.. hilo likapita nikajipanga tena upya kumtokea mara hii nilimfata nimeandika kabisa essay nikaanza kumsomea mbele yake lkn asalaleee komamanga la watu nilianza kutetemeka mpk sauti nayo ilikuwa ikitetemeka!. Ndugu nilichekwa mimi.. ikabidi nihairishe zoezi sahivi nikikutana nae anacheka tu na ameshanipa jina Kaka wa mikaratasi na anajua ilikuwa ni joke kumbe nilikuwa namaanisha. Huyo nae nikaachana nae..

Watatu sasa huyu nae ndo wale wanaitaga black beauty.. Toto fulani hivi kama twiga aliesimama kwenye mlima Kilimanjaro!
Hizi ndo zile pisi wanaita mboga saba! Unaweza hata ombea zamana na ukapata!.. komamanga la watu nikaona hapa ndo pakujitosa nikaakti kama gentleman kumbe lamba mwiko fulani tu!.. huyu kwanza nilianza pata tabu kwenye kiingereza chake tu!.. Mi naskia katamka "LILO BIL" hapo nitahangaika kujua anamaanisha nini kumbe kasema little bit!!.. hapo tu nikaanza kujiuliza hivi nimekuja kutongoza ama kutafuta changamoto!!.. ikabidi nijipe moyo tu nitatongoza hivyohivyo.

Nikajipanga siku ya siku nikamtoa out,kula sana mazagazaga kunywa sana ma wine,wisky n.k sasa kabla sijamuambia dhamira yangu akanitaka tukaogelee kulikuwa na swimming pool!. Na kuogelea sijui lkn nikaona hapa nitaonekana boya! Wacha nichukue point za umahiri asalaleee.. laiti ningejua maji ni nini walahi nisingeenda kuogelea mule!,nikajitupa kwa kujifanya mbobezi na ile step ya kwanza yakutumbukia nilienda kama mshale na hapo ndipo nilipokosea!! Naomba nisiendelee tumshukuru tu aliejuu kuwa nilitoka mzima!.. so hapo sikumuambia dhamira yangu msala wa kutumbukia kama mshale na kunywa vikombe uliharibu!

Nilimtongoza kwa sms tu na niliandika li essay likubwa lkn alivyojibu sasa hapo ndo nilikata tamaa! Hata hakujisumbua aliandika hivi tu "UNIKOME KAMA ULIVYOKOMA KWENYE SWIMMING POOL!!".

Ndugu zanguni mi staki kuwa padri wala mtumishi.. hebu niambieni ati Nakosea wapi mbona nakataliwa hivi..??
 
Mkuu hata wewe essay yote hii unaona ni comedy!!! Hapa kweli sijaleta kuomba ushauri..
Mkuu kupitia maandish yako we ni zaidi ya comedian bt tukirudi kwenye swala lako shida kubwa we unatongoza pisi zilizo nje ya uwezo wako, chakufanya tongoza za kati or zakawaida ambazo utaweza kuzimudu, nadhani ndo itakua suluhu ya changamoto yako.
 
Rudi tena kwake, mpe ID yako ya JF ili aweze kusoma post yako hii. Hakika atakuelewa hata kama itakuwa hisani kwake, upande wako hesabu zitakuwa zimetumia.
 
Bora Hata wewe Mimi aliniita mbwa .
Nikamtumia picha ya mambwa mengi halfu nokamwambia
"Onesha babako yukwapi hapa kwenye hii picha yetu ya pamoja".
Sasa hivi ndo mke huyu black mamba
😂😂
 
Pole sana, huwa inatokea, mshukuru Mungu huenda anakuepushia makubwa zaidi, pole sana
 
Back
Top Bottom