mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Utamaduni wa kutokusoma vitabu umetapakaa sana miongoni mwetu. Nimewahi kujiunga na makundi zaidi ya matatu ya kusoma lakini yalikufa na mengine kudumaa na hata kusinyaa. Kuna kipindi nikiwa kidato cha kwanza nilikuwa na hamasa kubwa ya kusoma vitabu kiasi kwamba nilifunga safari kwenda maktaba ya mkoa na kusoma siku nzima. Kipindi kifupi nilikuwa na uelewa mkubwa shule haikuwa tatizo kwangu lakini baadae utamaduni huu mzuri ukazimika.
Pamoja na kujua hayo, wazazi nao wameshindwa kuhamasisha watoto wao utamaduni huu chanya baada ya kugundua unafaida.
Mafuriko ya Social Media yamekuja yamekuta hatujaandaliwa wala kujiandaa kuyakwepo kama wakazi wa jangwani, wengi wa watanzania tumesombwa tunaelea kwenye mitandao huku tukitupa lulu hii ya thamani.
Vyanzo vya taarifa za wasomi,wanafunzi hata wanasiasa ni Google wakati asilimia karibu 70% ya taarifa hizo huwa sio za sahihi sana. Taarifa na maoni mengi rasmi huwekwa vitabuni.
Wakristo tunasoma "Daniel kwa Kuvisoma vitabu, alielewa siku na miaka ambayo jerusalem Itabomolewa"
UTAMADUNI WA KUSOMA SIO WA MZUNGU
Utamaduni wa kusoma sio wa mzungu, bali mzungu alitambua umuhimu wake na kuukumbatia, ukamfanya aendelee. Wazungu(wamagharibi) kilichochochea maendeleo yao ilikuwa ni kusoma na kuandika Ideas and concepts. Utamaduni wa Kusoma ni wa MWANADAMU. Ndio maana hata sisi wakati hatuna cha kusoma Tulikuwa Tunahadidhiwa mambo ya msingi na wazee wetu.
Dini zote zinahamasisha kusoma na kuweka vitu kichwani(Memorize).
Watu wakubwa, Viongozi wakubwa duniani, Mabillionea, Watu wenye ushawishi waliwekeza na wamewekeza kwenye kusoma vitu sahihi. Kama umeshindwa wewe basi anza na Mtoto wako.
Unadhani tulikosea wapi na nini kifanyike...