Mikhail Tal
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 505
- 872
Hii inajidhihirisha pale kunapokuwa na IPOs unaanza kuona watu wananunua tu hisa bila hata kufanya utafiti. Angalia hisa za Voda ilivokuwa, watu walinunua tu kwa kufuata mkumbo matokeo yake sasa wanaziuza tu tena kwa bei ya hasara.
Utakuta pale pale DSE kuna makampuni yanafanya vizuri tu mfano Twiga Cement, DSE lakini watu hata hawatolei macho. Mfano tu kuna kampuni kama NICOL ambayo mwaka huu walitoa gawio la TZS 26 kwa hisa moja ambayo ni return ya karibu asilimia 10 kwa sababu hisa zao zilikuwa zinauzwa kati ya TZS 260 kwa hisa moja.
Ukienda kwenye soko la hisa utagundua watanzania wengi wamenunua hisa katika makampuni mabovu kwa kufuata mkumbo na kuwaachia wajanja tena raia wa kigeni wakikomba hisa kwenye makampuni mazuri.
Watu wengi sana wametupa pesa zao kwenye makampuni kama Swala, Voda kwa maamuzi ya kukurupuka na kuacha wajanja wakijilia hela za bure kwenye makampuni kama Twiga, TBL, Sigara, Nicol na baadhi ya mabenki kama CRDB.
Ni budi tuwekeze akili zetu na maarifa kwenye hii tasnia ya masoko ya fedha.