Watanzania wavunja rekodi ya uzalendo Afrika: Utafiti umeonyesha

Kapwani

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
672
110
Imeandikwa na Na Joseph Lugendo;
Tarehe: 28th November 2009

TANZANIA imeweka rekodi ya aina yake barani Afrika kwa kuibuka nchi pekee yenye wananchi wenye mapenzi makubwa kwa taifa lao kuliko jambo au mfumo wowote wa kitamaduni, kiuchumi au kijamii unaowagawa katika makundi mbalimbali na matabaka.

Rekodi hiyo ambayo ni moja ya kigezo cha nchi iliyo na ulinzi imara, imepatikana baada ya wananchi wa nchi za Afrika, wakiwemo Watanzania, kufanyiwa mahojiano maalumu kuhusu jambo la fahari wanalodhani ni muhimu kujitambulisha nalo kati ya mambo kadha wa kadha yanayotumika kumtambulisha mwanadamu.

Vigezo vingine vinavyoifanya nchi kuwa na ulinzi imara na madhubuti licha ya uzalendo wa wananchi wake kulipenda taifa lao ni teknolojia ya vita, ushirikiano mzuri na nchi marafiki zikiwemo nchi jirani, wingi wa wanajeshi, bajeti inayotumika kwa ajili ya ulinzi na usalama na idadi ya watu.

Katika mahojiano hayo yaliyohusisha wananchi kati ya 1,200 na 2,400 katika kila nchi kati ya nchi 16 zilizochaguliwa kufanya utafiti kuhusu ujenzi wa taifa katika nchi za Afrika, wananchi waliulizwa maswali ili kubaini iwapo wanajisikia fahari zaidi kutambulishwa kwa jina la taifa lao kwa mfano Mtanzania, au kwa jina la kitu kingine haswa kabila.

Kwa mujibu wa maoni ya utafiti huo uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya utafiti ya Afro Barometer yenye makao makuu nchini Ghana na kuongozwa na Amanda Lea Robinson wa Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani ulionesha kuwa waliojisikia fahari kutambuliwa kwa mataifa yao zaidi ya kitu kingine ilikuwa asilimia 42 ya wahojiwa wote wanaofikia 22,765.

Tanzania ni ya pekee, ambapo asilimia 88 wanaelezea kulipenda zaidi taifa lao, hata wale ambao kabila lao lilikuwepo katika orodha asilimia 87 walisema wanajisikia fahari kutambulishwa kwa taifa lao,” alieleza msomi huyo katika utafiti wake huo.

Robinson ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Idara ya Sayansi ya Siasa ya Stanford University anasema katika utafiti huo uliotolewa Septemba mwaka huu kwamba wakati wastani wa wanaopenda mataifa yao katika nchi hizo ni asilimia 42 ya wahojiwa, kwa Tanzania wanaolipenda taifa lao ni asilimia 88 ya wahojiwa wote
.

Alifafanua kuwa mapenzi hayo kwa taifa yanaweka mazingira mazuri ya kukua kwa demokrasia kwa kuwa mtu hatazuiwa haki yake ya kuchaguliwa kwa kigezo cha kuwepo katika kikundi fulani ambayo pia itachangia kukua kwa uchumi na maendeleo ya watu.

Hii nimeipenda zaidi. Jamani kumbe sisi ni wazalendo kiasi hiki sasa kwanini tunaendelea kuwa maskini? uzalendo huu ungesaidia sana kuliweka taifa katika maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni. Mbona wazalendo sisi ni mafisadi, au wanaohusika na ufisadi si WATANZANIA?

Je asilimia 88 ya watu waliohojiwa hawa hawamo katika wimbi la ufisadi kuanzia ofisi za wevyeviti wa vijiji, kata,tarafa etc? je hakukuwa na hawa manesi wanaotuzalisha baada ya kuwapa 5000 kinyume cha hapo unazaa mwenyewe yeye anakunywa chai yake akisoma gazeti?

Je hawa hawajahusika na kashfa za kugawa mashamba ya wanakijiji wenzao kwa wageni? Je hawa 88 wamo pia wahanga wa mabomu mbagala? je wamachinga na wa vibaka pia wamo? bila kusahau trafiki na madereva wa daladala! je wamo viongozi waandamizi wa serikali, je wamo wahadhiri wa vyuo ambao baadhi yao hupenda kutoa digrii za ch..i? wawakilishi watu je?

Kama hawa wote na wengine walikuwepo katika sample hii Je wali respond uongo tu kwenye mahojiano au ndio dhamira zao za kweli?

K
ama ni dhamira za kweli jamani kwanini sisi ni maskini sasa? wazalendo wenzangu nisaidieni maana nafahamu kuwa hata kuwa JF tumesukumwa na uzalendo wetu pia
 
Kapwani niongezee swali lingine, hivi hao 88% wanaolipenda taifa lao mbona hawakujiandikisha kupiga kura kwny uchaguzi wa serikali za mitaa? au utafiti ulifanyika kabla watu hawajaamua kutokuwa wazalendo? Mmmmmh
 
he! makubwa? labda! lakini hata mimi naipenda nchi yangu ila nahisi kila siku upendo unapungua.
 
Zoezi linaweza kuonyesha tu kwamba Watanzania wanajua kukuambia kile ambacho wanafikiri unataka kusikia.

Which is not a bad thing entirely, cause it shows smarts.

Uzalendo my foot, watu hawana chakula wala malazi watakuwa na uzalendo gani?
 
mmm. mi nashangazwa na ripoti zao na ninawasiwasina data zao kwani ukiangalia in real sense, watanzania si wazalendo wavitendo tena toka siku nyingi na ndo maana ujamaa ulitushinda ubinafsi ulichukua nafsi yake, mpaka sasa ubinafsi ndo mwakemwake, utaifa unakuja baadae. au labda mi sijui maana halisi ya huo uzalendo wanaouzungumzia.
 
Itakuwa hakukutana na wazenji...isingelifika asimilimia 88%.Wote wangelisema hawataki kuitwa watanzania....:rolleyes:
 
kuna tofauti gani kati ya UZALENDO na UZAWA?.........................nikijibiwa hili naweza kuwa kwenye position nzuri ya kujibu
 
Serikali ikiogopa wananchi, nchi itaendelea, lakini wananchi wakiogopa serikali, the virce versa is true. Ni majibu ya uoga haya. Hauwezi kuipenda nchi yako wakati unakufa njaa.
 
Ili kuwa mzalendo wa kweli, inabidi uwe na ilmu ya uelewa, uelewe uraia, uelewe nchi yako na uongozi wake, kisha hapo unaweza kufanya maamuzi yako uwe mzalendo au la.

Sasa watu hawana hata elimu, wengine wanafikiri Nyerere bado rais, wengine wanafikiri Malecela bado Waziri Mkuu, unataka kuniambia wana uzalendo hawa?

Ukondoo labda, Uzalendo? Nabisha.
 
Zoezi linaweza kuonyesha tu kwamba Watanzania wanajua kukuambia kile ambacho wanafikiri unataka kusikia.

Which is not a bad thing entirely, cause it shows smarts.

Uzalendo my foot, watu hawana chakula wala malazi watakuwa na uzalendo gani?

Hii nimeipenda kwa iyo haishangazi kwa nini Ben alipata tuzo la uongozi bora yawezekana hizi tuzo zinatolewa baada ya kusoma tafiti kama hizi.

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Kuna wakati inabidi tuwe tunaangalia na mazuri tuliyo nayo. Na tuweze kutofautisha kuipenda nchi na kuwapenda viongozi na yale yanayofanywa na kundi fulani. Mimi nafikiri kama huu utafiti umefanyika objectively inawezekana kabisa kuja na majibu hayo. Hasa ukijaribu kulinganisha na majirani zetu ambao kwao utambulisho wa kwanza ni kabila. nadhani watanzania wengi wanajivunia Utanzania wao kabla ya kusema anatoka upande upi wa Tanzania. Hili swali la kabila nimeshuhudia mara nyingi sana mtua akiulizwa na yeye anauliza "kwani ni unataka kujua?"
 
Nimeiukubali hii JF maana zikiletwa research za hao hao zikiiponda TZ ambao leo watu wana question credibility zao watu wanazikubali ila zikija za kuisifia kidogo watu wanageuka na kuanza kuponda data!!
 
Nimeiukubali hii JF maana zikiletwa research za hao hao zikiiponda TZ ambao leo watu wana question credibility zao watu wanazikubali ila zikija za kuisifia kidogo watu wanageuka na kuanza
kuponda data!!

you might be correct mkuu
Ila mimi nimeshangaa sana hawa wa tz ninaowafahamu kuanzia ngazi ya kijiji walivyopagawa na roho za ufisadi leo ndio wanatamka wanaipenda nchi yao? na wanajivunia kutambulishwa nayo hata baada ya kuivua nguo nchi yenye maliasili hivi kuwa maskini?
Hapana hili limenishangaza sana, hata kama data iko biased kwanini tuongoze africa? ina maana watu wame respond uongo, hayakutoka mioyoni katu...maana muungwana ni vitendo sio porojo
 
Eti unapenda taifa lako na unapenda kutambulishwa nalo!
Sidhani kama mtu yeyote angependa kutambulishwa na taifa ambalo bado a)wanafunzi wake wa shule ya msingi wanakaa chini wakisoma kwa karne hii
b)Taifa ambalo wanawake wanajifungulia chini sakafuni na hakuna
anayeonekana kujali sana labda naomi campbel ambaye nadhani hakuhusishwa katika utafiti huu
c) Taifa ambalo wanafunzi wa shule za kata wanalazimika kutembea kilometa nyingi kufika shule, na wakifika wamechoka, lakini kama hiyo haitoshi wakifika huko hakuna walimu wa kutosha maana walimu wazalendo hawa wote wanapenda kukaa mijini!
d) Taifa ambalo vifo vya watoto wadogo under five bado ni threat, manutrition bado ipo pamoja na maliasili yote inayotuzunguka
e) Taifa ambalo ku wakati linaingia gizani !!!!
d) Taifa ambalo baadhi ya walimu wako tayari kukufelisha kwa sababu binafsi...hawa wazalendo

Ni mengi sana ya kushangaa katika ripoti hii! Nami naamini si serikali pekee au rais pekee au chama fulani kinaweza kubadilisha hali hii....ni watanzania wote kuamua kwa dhati kuipenda nchi na kufanya juhudi ya pamoja ili kuifanya iwe na sura ya kupendwa kutambulishwa nayo

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
you might be correct mkuu
Ila mimi nimeshangaa sana hawa wa tz ninaowafahamu kuanzia ngazi ya kijiji walivyopagawa na roho za ufisadi leo ndio wanatamka wanaipenda nchi yao? na wanajivunia kutambulishwa nayo hata baada ya kuivua nguo nchi yenye maliasili hivi kuwa maskini?
Hapana hili limenishangaza sana, hata kama data iko biased kwanini tuongoze africa? ina maana watu wame respond uongo, hayakutoka mioyoni katu...maana muungwana ni vitendo sio porojo
In any research lazima kuwe na objectives na methodology!! Nashangaa kwani hapa tumesoma tu results za hiyo reserch na ila watu hatufahamu ni methodology gani imetumika kupata data!! kinacho nishangaza kwa zile nchi ambazo zimeonekana kua hawana uzalendo na nchi zao sijaona hata mmoja akisema may be nao wamedanganya!!
 
Eti unapenda taifa lako na unapenda kutambulishwa nalo!
Sidhani kama mtu yeyote angependa kutambulishwa na taifa ambalo bado a)wanafunzi wake wa shule ya msingi wanakaa chini wakisoma kwa karne hii
b)Taifa ambalo wanawake wanajifungulia chini sakafuni na hakuna
anayeonekana kujali sana labda naomi campbel ambaye nadhani hakuhusishwa katika utafiti huu
c) Taifa ambalo wanafunzi wa shule za kata wanalazimika kutembea kilometa nyingi kufika shule, na wakifika wamechoka, lakini kama hiyo haitoshi wakifika huko hakuna walimu wa kutosha maana walimu wazalendo hawa wote wanapenda kukaa mijini!
d) Taifa ambalo vifo vya watoto wadogo under five bado ni threat, manutrition bado ipo pamoja na maliasili yote inayotuzunguka
e) Taifa ambalo ku wakati linaingia gizani !!!!
d) Taifa ambalo baadhi ya walimu wako tayari kukufelisha kwa sababu binafsi...hawa wazalendo

Ni mengi sana ya kushangaa katika ripoti hii! Nami naamini si serikali pekee au rais pekee au chama fulani kinaweza kubadilisha hali hii....ni watanzania wote kuamua kwa dhati kuipenda nchi na kufanya juhudi ya pamoja ili kuifanya iwe na sura ya kupendwa kutambulishwa nayo

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
Kwa jinsi ulivyo andika hapo inaonyesha unalipenda Taifa lako na una Uchungu wa nchi kutaka mabadiliko!!
 
Mawazo ya wengi humu yapo corrupted, ndio maana yanashindwa kuona umuhimu ya mtanzania kujitambulisha kama ni Mtanzania na sio Mgogo ama Mhaya ama Mmakuduchi!
 
Ni lazima kwa kila mtz na mtu mwingine yeyote kuwa mzalendo kwa nchi yake kwani ''MJENGA NCHI NI MWANANCHI NA MBOMOA NCHI NI MWANANCHI HUYOHUYO'' huwezi kujivua utaifa eti kwa sababu nchi yako ni masikini kwani wewe ni sehemu ya tatizo.....na kama wewe ni mtz na umeulizwa kuhusu uzalendo wako kwa taifa lako ukajibu unependa kuwa mmarekani utakuwa unachemka kwani wamarekani walijenga taifa lao kwa kuweka mbele uzalendo kipindi walipo kuwa masikini....hata nchi ambazo inaaminika wananchi wake sio wazalendo inawezekana wamejibu kuwafurahisha waulizaji lakini ukweli unabaki moyoni mwao kwamba hawawezi kuisaliti nchi yao.....hapa bado sijaamini..........utafiti ulifanyika kwa watz waishio ng'ambo ambao hawajui kinachoendelea hapa nchini.Lazima tufikie mahali tujiulize namna tulivyo saidia kuijenga nchi na tuende mbali zaidi kwa kujiuliza ''SISI TUMEIFANYIA NINI NCHI YETU KABLA YA NCHI YETU KUTUFANYIA KITU'' mmoja mmoja pale alipo ajielize alivyo shiriki kulijenga taifa................hizo takwimu ni ubabaishaji tu....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom