Watanzania wavunja rekodi ya uzalendo Afrika: Utafiti umeonyesha

hata mie naipenda sana nchi yangu ya TZ lakini watu wake loh hata hatupendani hata kidogo
 
Ni lazima kwa kila mtz na mtu mwingine yeyote kuwa mzalendo kwa nchi yake kwani ''MJENGA NCHI NI MWANANCHI NA MBOMOA NCHI NI MWANANCHI HUYOHUYO'' huwezi kujivua utaifa eti kwa sababu nchi yako ni masikini kwani wewe ni sehemu ya tatizo.....na kama wewe ni mtz na umeulizwa kuhusu uzalendo wako kwa taifa lako ukajibu unependa kuwa mmarekani utakuwa unachemka kwani wamarekani walijenga taifa lao kwa kuweka mbele uzalendo kipindi walipo kuwa masikini....hata nchi ambazo inaaminika wananchi wake sio wazalendo inawezekana wamejibu kuwafurahisha waulizaji lakini ukweli unabaki moyoni mwao kwamba hawawezi kuisaliti nchi yao.....hapa bado sijaamini..........utafiti ulifanyika kwa watz waishio ng'ambo ambao hawajui kinachoendelea hapa nchini.Lazima tufikie mahali tujiulize namna tulivyo saidia kuijenga nchi na tuende mbali zaidi kwa kujiuliza ''SISI TUMEIFANYIA NINI NCHI YETU KABLA YA NCHI YETU KUTUFANYIA KITU'' mmoja mmoja pale alipo ajielize alivyo shiriki kulijenga taifa................hizo takwimu ni ubabaishaji tu....

Sikumaanisha watu wajivue utaifa wao kwa sababu ya umaskini tulionao,la hasha! Nilikuwa natoa mwito wa imani bila matendo haina tija! uungwana ni vitendo si porojo. Kama tunaipenda Tanzania basi tufanye juhudi za pamoja kutatua matatizo yetu ili hata ukijitambulisha mahali kuwa naipenda tanzania basi matendo yetu yadhihirike na MATUNDA YA MATENDO YETU YANAONEKANA!
 
Watanzania wazalendo? Mmmhh! Can someone please eleborate?

Kuipenda nchi kwa maneno tu! Blah blah nyiiingi, vitendo vya kizalendo sifuri.
 
Asilimia kubwa ya Watanzania wana Uzalendo wa Kinafiki na Kifisadi, sidhani wengi wana uzalendo wa kweli ambapo wanaweza kujitoa mhanga kutetea na kulinda maslahi ya nchi na rasilimali zake. Uzalendo wa Watanzania wengi si uzalendo wa kweli.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom