Mambodia ridhaa wanne wa Kitanzania wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja nchini Mauritius baada kupatikana na makosa ya kuingiza nchini humo madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo nne.
Wanandodi hao waliiambia mahakama kuwa waliingiza madawa hayo kwa sababu walikuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya matunzo ya familia zao. Walikamatwa mwaka 2008 walipokwenda nchini humo kwa ajili ya mashindano ndondi ridhaa ya Afrika (African Cup of Boxing).
Wanandondi hao wanajulikana kwa majina ya Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa and Petro Charles Mtagwa. Inasemekana wote walikuwa na future nzuri sana ya kuwa mabondia wa kimataiafa mpaka pale walipokamatwa Juni 2008 baada ya polisi kuvamia hoteli kwenye mji wa Quatre Bornes, uliopo kilomita 15 kutoka mji mkuu wa Port Louis, baada ya kikosi cha madawa ya kulevya nchini humo kupata habari za kinteligensia.
Wakijitetea mahakamani hapo, wanandodi hao waliomba radhi kwa taifa la Mauritius na pia kudai kuwa wao ni maskini na wana majukumu mazito ya kifamilia, watoto na wazee wanaowategemea nyumbani. Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepokea kiasi cha Dola za Kimarekani 5,200.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Marie Joseph alisema kuwa pamoja na majukumu yao ya kifamilia, kukubali makosa yao na kusaidia kukamatwa kwa mwenyeji wao, kosa walilotenda ni kubwa sana kustahili hukumu ya miaka 15. Hata hivyo, Jaji amesema kuwa siku 1,722, ambazo wamekaa gerezani, zitapunguzwa katika vifungo vyao.
Hapo kwenye red, ni kweli dola 5,200 au umekosea kuquote!?
Hizo ni ndogo sana kwa kilo nne, jamaa wanameza gramu mia kadhaa na wakirudi bongo mtaani hatukai kwa raha! Mikoko kadhaa na mpaka kununu nyumba so ukiniambia kilo 4 ni USD 5,200 ambayo haizidi hata Tsh 10 milioni sio kweli!Kamanda Limbani ,inaelekea unajua bei za bidhaa hizi walizokamatwa nazo hawa mburula!!!Je hizo $5,200 kwa kilo nne ni ndogo?
Vipi ni nyingi sana? Basi ngoja ni-convert kwa sarafu ya Kitanzania.
Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepokea kiasi cha Sh. 8,504,556.74
Mtuhumiwa halisi mahakama zetu zimemwachia huru....
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachia huru aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaj Shaban Mintanga aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya nchini Mauritius baada kumuona hana kesi ya kujibu.
Interesting. Ina maana kesi yake ilikuwa na connection na hii ya waliohukumiwa Mauritius baada ya kukubali makosa yao?
Ushahidi huo wa mazingira ambao upande wa mashtaka uliuegemea ni namba za simu zilizodaiwa kukutwa kwenye tiketi za watu wanaodaiwa kukutwa na dawa hizo nchini Mauritius.
Hizo ni ndogo sana kwa kilo nne, jamaa wanameza gramu mia kadhaa na wakirudi bongo mtaani hatukai kwa raha! Mikoko kadhaa na mpaka kununu nyumba so ukiniambia kilo 4 ni USD 5,200 ambayo haizidi hata Tsh 10 milioni sio kweli!
Huyu ndie aliyewatuma na kuwabebesha unga, jamaa wa Mauritius walimtaka sana apelekwe kule kuunganishwa na hawa jamaa lakini kama unavyojua bongo yetu ilipigwa danadana mwisho akaachiwa huru. Kilo moja ya unga ni around Tsh 100ml kwa soko nzuri, hiyo USD 5200 ni bei ya Colombia "shambani"
Huyu ndie aliyewatuma na kuwabebesha unga, jamaa wa Mauritius walimtaka sana apelekwe kule kuunganishwa na hawa jamaa lakini kama unavyojua bongo yetu ilipigwa danadana mwisho akaachiwa huru. Kilo moja ya unga ni around Tsh 100ml kwa soko nzuri, hiyo USD 5200 ni bei ya Colombia "shambani"
Halafu hawa jamaa walikuwa amateurs.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
Kifuko kimoja kinaweza kuwa bei gani?
Haijalishi ni wazo lao au wazo la mtu mwengine, tanzania tunatia aibu nchi yetu sasa, kila kukiwa na mashindano ya kimichezo ndani na nje ya nchi lazima wachezaji wabebe madawa ya kulevya!! sikuzote michezo inahamasisha vijana kuwa na tabia njema, sasa mwana michezo kuuza unga ni sawa na mchungaji au ustadh kufungua danguro.... hivi hapa kwenye uwanja wetu wa taifa hakuna ving'amuzi vya haya madudu..????Halafu hawa jamaa walikuwa amateurs.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
Kifuko kimoja kinaweza kuwa bei gani?