Watanzania wamkimbilie nani zaidi?

Watanzania wamkimbilie nani zaidi?

Nashukuru, umenielewa vizuri. Sina maana kwamba mhimili unawalinda wezi, ninachojaribu kuzungumzia ni pale ambapo wizi wa wazi kabisa umetokea, wezi wanafahamika lakini aliyepaswa kuwachukulia hatua kali kabisa ili iwe fundisho kwa wengine, naye amekaa kimya.
Kwa mfano, wewe ni mlinzi halafu wezi wanakuja kuiba mali unazozilinda, wanafanikiwa kuondoka na hizo mali, wakati huo wezi wamekuja na Mapanga lakini wewe kama mlinzi una AK-47. Mwishowe unaanza kulalamika eti umeibiwa. Mbaya zaidi ni kwamba, wezi wanafahamika, uwezo wa kuwachukulia hatua kali unao, lakini huchukui hatua.
Je, katika hali ya kawaida, wewe kama mlinzi sisi tutakutafsiri vipi?
Kauli yake ya kuonyesha kwamba kaplay role kama leader imebaki kuwa na hili mkalichunguze.Swali ni kwamba nani akalichunguze?
 
Kuna utawala wa sheria Nchi hii.CAG ameeleza yake tuache vyombo vinavyohusika vifanye kazi yake.Au mnataka Kangaroo Courts?
Mkipata utawala unaojaribu kufuata utawala wa sheria mnalalamika, mkipata anayejirundikia madaraka na kuamua anavyoona yeye bila kujali utawala wa sheria mnalalamika. Which is which lazima mchague.Watu wakituhumiwa ni lazima process ipite ushahidi utakao hold in a court of law upatikane sio mob justice.
Kangaroo court inaweza kutumika accordingly.
Kuna baadhi ya mambo yanapaswa kushughulikiwa kulingana na mazingira yake yalivyo.

Wakati mwingine kitu kinachoitwa UTAWALA WA SHERIA kinaweza kutumika kama KICHAKA cha wezi na waovu wengine.
 
Back
Top Bottom