Watanzania wamkimbilie nani zaidi?

Watanzania wamkimbilie nani zaidi?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,622
Reaction score
3,144
Bila shaka kila Mtanzania anajua madudu yanayofanyika na viongozi wengi katika Nchi hii.
Kuna mambo ya Rushwa, ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, uzembe makazini, wizi wa mali za umma nk.

Kwa awamu hii, vitendo hivyo vyote vinafanyika bila kificho. Yaani wanaofanya hayo hawaogopi mtu isipokuwa wao ndo wanaoogopwa.

Kwa kifupi kabisa ni kwamba:-
•Wabunge(isipokuwa wachache wao) wamewekwa mfukoni na Genge hilo, hivyo hawawezi kuchukua hatua madhubuti.

•WATU WA HAKI ZA BINADAMU wamewekwa mfukoni na Genge hilo, hivyo hawawezi kupaza sauti zao kukemea uovu huo.

•Bad enough, inaonekana hata MHIMILI MKUU umepigwa mfukoni na Genge hilo, ndo maana huwezi kuona unachukua hatua kali na za wazi kwa wahujumu hao.

Je, Watanzania wamwamini nani anayeweza kuwasaidia/kuwapigania?
 
Hivi ukiambia uthibitishe madai yako utaweza? Free speech ina mipaka yake.Au unafikiri kujificha chini ya identity uliyonayo ndio kinga?

Kusema usichoweza kuthibitisha na kuwataja watu ni kosa la jinai. Njoo na uthibitisho.
 
Hivi ukiambia uthibitishe madai yako utaweza?Free speech ina mipaka yake.Au unafikiri kujificha chini ya identity uliyonayo ndio kinga?
Kusema usichoweza kuthibitisha na kuwataja watu ni kosa la jinai.Njoo na uthibitisho.
Kama awachukuliwi hatua kwann tusidhani hivyo
 
Si kipindi wapinzani wanang'olewa bungeni mlishangilia eti wanatumika na mabeberu alafu Leo mnalialia Nini?! Kama hamuwezi kuandamana kudai haki zenu kama Kenya au Misri basi kaeni kimya nchi iendelee kuliwa. Haiwezekani muwape nchi nzima CCM alafu muanze kulalamikia watu ambao hamkuwapa hata Jimbo Moja.

Shame on you
 
Hivi ukiambia uthibitishe madai yako utaweza? Free speech ina mipaka yake.Au unafikiri kujificha chini ya identity uliyonayo ndio kinga?

Kusema usichoweza kuthibitisha na kuwataja watu ni kosa la jinai. Njoo na uthibitisho.
Mtu kutojua tarehe yake ya kuzaliwa haina maana kwamba hakuzaliwa.

Wewe hujamsikia CAG akitoa taarifa na mapendekezo yake dhidi ya ufisadi?
Mpaka sasa, niambie ni nani kati ya waliohusika kuiba mabilioni ya Watanzania amechukuliwa hatua madhubuti?
 
Si kipindi wapinzani wanang'olewa bungeni mlishangilia eti wanatumika na mabeberu alafu Leo mnalialia Nini?! Kama hamuwezi kuandamana kudai haki zenu kama Kenya au Misri basi kaeni kimya nchi iendelee kuliwa. Haiwezekani muwape nchi nzima CCM alafu muanze kulalamikia watu ambao hamkuwapa hata Jimbo Moja.

Shame on you
Wewe unachanganya mafaili.
 
Hivi ukiambia uthibitishe madai yako utaweza? Free speech ina mipaka yake.Au unafikiri kujificha chini ya identity uliyonayo ndio kinga?

Kusema usichoweza kuthibitisha na kuwataja watu ni kosa la jinai. Njoo na uthibitisho.
Unataka aprove nini sasa hapa.Are you trying to defend someone here? sio mtu wa kufuatilia mambo kiundani lakini ulisikia au kusoma ripoti ya mkaguzi wa serikali(kumbuka hii ni formal document sio kelele za watu wa mtaa) nini kaeleza?si rushwa au matumizi mabaya na wahusika si wametajwa au?
 
Ninachomtahadharisha ni kudai kwamba wanalindwa na Mhimili mkuu.Anaweza kuthibitisha kulindwa huko?
 
Yeah concern yako nimeipata lakini hapa theme ya ujumbe wake ni haya mauza uza tunayoshuhudia Tanzania.Ndio anaweza kuwa kakosea katika hiyo sentensi lakini angalia hapa sio kwenye formal gathering kwamba kila protocol lazima izingatiwe so forget about mihimili kulinda wezi(hiki ni kipengele kidogo sana kwenye ujumbe wake)

Again ata hii kauli yake anaweza kuitetea hapa(japo sijui ikifika kwenye vyombo vya sheria kama anaweza).Hoja ni kwamba,why does the president take so long to decide on every single madness that is revealed?
 
Kuna utawala wa sheria Nchi hii.CAG ameeleza yake tuache vyombo vinavyohusika vifanye kazi yake.Au mnataka Kangaroo Courts?
Mkipata utawala unaojaribu kufuata utawala wa sheria mnalalamika, mkipata anayejirundikia madaraka na kuamua anavyoona yeye bila kujali utawala wa sheria mnalalamika. Which is which lazima mchague.Watu wakituhumiwa ni lazima process ipite ushahidi utakao hold in a court of law upatikane sio mob justice.
 
Bila shaka kila Mtanzania anajua madudu yanayofanyika na viongozi wengi katika Nchi hii.
Kuna mambo ya Rushwa, ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, uzembe makazini, wizi wa mali za umma nk.

Kwa awamu hii, vitendo hivyo vyote vinafanyika bila kificho. Yaani wanaofanya hayo hawaogopi mtu isipokuwa wao ndo wanaoogopwa.

Kwa kifupi kabisa ni kwamba:-
•Wabunge(isipokuwa wachache wao) wamewekwa mfukoni na Genge hilo, hivyo hawawezi kuchukua hatua madhubuti.

•WATU WA HAKI ZA BINADAMU wamewekwa mfukoni na Genge hilo, hivyo hawawezi kupaza sauti zao kukemea uovu huo.

•Bad enough, inaonekana hata MHIMILI MKUU umepigwa mfukoni na Genge hilo, ndo maana huwezi kuona unachukua hatua kali na za wazi kwa wahujumu hao.

Je, Watanzania wamwamini nani anayeweza kuwasaidia/kuwapigania?

Ni kuandamana kama Kenya tu.
 
Hii ndo awamu majizi yanapigiwa kelele za mwizi na CAG na wala hayashtuki ndo kwanza yanatafuta kwengine kwa kuiba.
 
Yeah concern yako nimeipata lakini hapa theme ya ujumbe wake ni haya mauza uza tunayoshuhudia Tanzania.Ndio anaweza kuwa kakosea katika hiyo sentensi lakini angalia hapa sio kwenye formal gathering kwamba kila protocol lazima izingatiwe so forget about mihimili kulinda wezi(hiki ni kipengele kidogo sana kwenye ujumbe wake)

Again ata hii kauli yake anaweza kuitetea hapa(japo sijui ikifika kwenye vyombo vya sheria kama anaweza).Hoja ni kwamba,why does the president take so long to decide on every single madness that is revealed?
Indeed.
 
Kuna utawala wa sheria Nchi hii.CAG ameeleza yake tuache vyombo vinavyohusika vifanye kazi yake.Au mnataka Kangaroo Courts?
Mkipata utawala unaojaribu kufuata utawala wa sheria mnalalamika, mkipata anayejirundikia madaraka na kuamua anavyoona yeye bila kujali utawala wa sheria mnalalamika. Which is which lazima mchague.Watu wakituhumiwa ni lazima process ipite ushahidi utakao hold in a court of law upatikane sio mob justice.
Naelewa kila kitu ndugu sema jambo moja tu ambalo ni implicit ni kwamba bongo president ndio kila kitu(forget about what is written in formal documents like the constitution and other legal documents)

Kwenye hizi document ndio explicitly wametaja vitu kama mahakama,bunge na blah! blah! kibao ila ukiweka hivi vitabu kando ambavyo kaviandika binadamu tena wa kitanzania,rais anabaki kuwe yeye ndio mwisho wa hesabu.Sasa huyu anacheza michezo ya kihuni sana yeye kila jambo ni kwamba likatazamwe(anajaribu kuonyesha power decentralization lakini hii ni hypocrisy ya kiwango cha juu).
 
Sipo hapa ku judge assumption yako.Ulitaka uchunguzi ufanyike siku ngapi au una prefer wale wa kamata weka ndani mara moja.Halafu hakuna kinachoendelea baada ya hapo.Tumelemazwa na mfumo wa one man show.Time will tell.Kwa sasa ni mapema sana kuja na hiyo conclusion yako.
 
Yeah concern yako nimeipata lakini hapa theme ya ujumbe wake ni haya mauza uza tunayoshuhudia Tanzania.Ndio anaweza kuwa kakosea katika hiyo sentensi lakini angalia hapa sio kwenye formal gathering kwamba kila protocol lazima izingatiwe so forget about mihimili kulinda wezi(hiki ni kipengele kidogo sana kwenye ujumbe wake)

Again ata hii kauli yake anaweza kuitetea hapa(japo sijui ikifika kwenye vyombo vya sheria kama anaweza).Hoja ni kwamba,why does the president take so long to decide on every single madness that is revealed?
Nashukuru, umenielewa vizuri. Sina maana kwamba mhimili unawalinda wezi, ninachojaribu kuzungumzia ni pale ambapo wizi wa wazi kabisa umetokea, wezi wanafahamika lakini aliyepaswa kuwachukulia hatua kali kabisa ili iwe fundisho kwa wengine, naye amekaa kimya.
Kwa mfano, wewe ni mlinzi halafu wezi wanakuja kuiba mali unazozilinda, wanafanikiwa kuondoka na hizo mali, wakati huo wezi wamekuja na Mapanga lakini wewe kama mlinzi una AK-47. Mwishowe unaanza kulalamika eti umeibiwa. Mbaya zaidi ni kwamba, wezi wanafahamika, uwezo wa kuwachukulia hatua kali unao, lakini huchukui hatua.
Je, katika hali ya kawaida, wewe kama mlinzi sisi tutakutafsiri vipi?
 
Sipo hapa ku judge assumption yako.Ulitaka uchunguzi ufanyike siku ngapi au una prefer wale wa kamata weka ndani mara moja.Halafu hakuna kinachoendelea baada ya hapo.Tumelemazwa na mfumo wa one man show.Time will tell.Kwa sasa ni mapema sana kuja na hiyo conclusion yako.
Binafsi sina power ya kuamua how long and when investigation shall begin.Power nliyonayo ni vote, and guess what! my vote doesn't count.Hivyo basi hatuna haja ya kufanya malumbano au kufanya mjadala uwe mkubwa.

Acha wenye kula wale,wenye kuiba waendelee kuiba labda kuna siku watakoma.
 
Back
Top Bottom