Watanzania Waliofariki Hijja Wafikia 8

Watanzania Waliofariki Hijja Wafikia 8

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Zuberi Ali amesema mpaka sasa ni watu 8 ndio wameripotiwa kufa katika tukio la mahujaji kukanyagana huko makka nchini Saudi Arabia wakati wa Swala ya hijja. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mufti Zuberi ameongeza kuwa juhudi zinaendelea kufanywa kwa pamoja kati ya balozi wa Tanzania na Serikali ya Saudi Arabia kujua idadi kamili ya Watanzania waliokwenda, waliofariki, waliopotea na waliofanikiwa kurudi.

Hata hivyo Mufti Zuberi amesema kuwa mwaka huu hakutakuwa na shamra shamra za kuwapokea mahujaji wanaorudi toka makka sababu ya kuomboleza msiba huo.

Aidha Mufti Zuberi amesema chanzo cha ajali ni baada ya kufungwa kwa njia moja ya kwenda katika eneo la jamarati ili kumpiga mawe shetani na hivyo kusababisha watu kuwa wengi zaidi ya uwezo wa njia.

Chanzo: EATV HOT MIX
 
mbona sababu iliotolewa na mufti inatofautiana na ile ilotolewa officials wa saudia
 
Umemsikia nani?

Soma vyombo vya habari vya Iran. Na ndo maana Saud Arabia wamekataa kutoa hata mwili mmoja ukazikwe kutoka kwenye nchi ya mahujaj walipotoka. Soon vita ya Iran na Saudia vinanukia. Maana mahujaj wengi waliokufa wanatokea Iran. Stay tuned
 
Huyu shetani ameleta Shida sana. Hivi wakuu nisaidieni pale ndio makao ya shetani?
 
Siyo hivyo, ni tendo la kuadhimisha yaliyotokea enzi hizo. Shetani yupo popote unapomtaja Mungu na Shetani pia hutajwa ndiyo maana hata kumpiga vinatumika vijiwe vidogovidogo.
 
Mkuu kwa hiyo unataka kuniambia huyo shetani hawezi kupigiwa mawe kwenye nchi zao mpaka waende pale??
 
Zuberi Ali amesema mpaka sasa ni watu 8 ndio wameripotiwa kufa katika tukio la mahujaji kukanyagana huko makka nchini Saudi Arabia wakati wa Swala ya hijja. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mufti Zuberi ameongeza kuwa juhudi zinaendelea kufanywa kwa pamoja kati ya balozi wa Tanzania na Serikali ya Saudi Arabia kujua idadi kamili ya Watanzania waliokwenda, waliofariki, waliopotea na waliofanikiwa kurudi.

Hata hivyo Mufti Zuberi amesema kuwa mwaka huu hakutakuwa na shamra shamra za kuwapokea mahujaji wanaorudi toka makka sababu ya kuomboleza msiba huo.

Aidha Mufti Zuberi amesema chanzo cha ajali ni baada ya kufungwa kwa njia moja ya kwenda katika eneo la jamarati ili kumpiga mawe shetani na hivyo kusababisha watu kuwa wengi zaidi ya uwezo wa njia.

Chanzo: EATV HOT MIX

Hivi Ismail Aden Rage amesharudi? Nauliza tu.
 
Huyu shetani ameleta Shida sana. Hivi wakuu nisaidieni pale ndio makao ya shetani?
Hiyo ndio Imani bana,ukiingia kiundani sana unaweza kufikia muafaka kuwa hawa jamaa ni machizii! ila ukweli ni kuwa uislamu unatakiwa uuamini na kuufuata bila kuhoji chochote na kama wangeruhusu kuhoji na kukosoa kwa wazi hii dini isinge enea kabisa. Kizuri ni kuwa ukihama uislam adhabu yake ni kifo na ukimkosoa Mtume au Allah basi adhabu yako pia ni kifo.
 
Uongo ulioje?? Ni heri ukae kimya tuu kama hujui.
 
Back
Top Bottom