Watanzania walalahoi 'wanazikwa' bungeni dodoma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania walalahoi 'wanazikwa' bungeni dodoma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamakabuzi, Jun 23, 2011.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ubaguzi
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sehemu ya tatu kwenye haki na usawa; kifungu cha 13(2) kinasema:

  “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.”

  Na kifungu kidogo cha (5) yaani 13(5) inafafanua maana ya ubaguzi kama ifuatavyo:

  “Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au wanahesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno “kubagua” halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia serikali kuchukua hatua za maksudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika jamii”

  Je Bunge linapotunga sheria ya posho ambayo inabagua watanzania katika kulipa kodi, tena kibaya zaidi inawakandamiza baadhi ya watanzania, halikiuki ibara hii ya Katiba?
  Kwa sheria ya fedha iliyopitishwa na bunge:
  Mtu yeyote anayefanya kazi serikalini au kwenye taasisi au shirika linalopata ruzuku ya serikali hatalipa kodi ya mapato kwenye posho atakazopewa. Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba mtu yeyote asiyefanya kazi serikalini,au anayefanya kazi katika taasisi au shirika lisilopata ruzuku ya serikali atalipa kodi ya mapato katika posho atakazopewa.
  Mfano:
  Ndugu Musa ameajiriwa na serikali na ndugu Mbonde ameajiriwa na Kampuni ya Mohamed; wote wawili wanahudhuria warsha ya siku 5 iliyoandaliwa na TGNP na wanapewa posho ya kikao (sitting allowance) ya Tshs 50,000 kwa siku. Wote ni watanzania wanaoishi Mbagala DSM na wanapanga nyumba moja.
  Kwa sheria hii ya fedha, Musa hatalipa kodi kwenye posho hiyo lakini Mbonde posho hiyo inajumuishwa na mshahara wake na kukatwa kodi ya mapato!
  Je sheria hii haina ubaguzi wa dhahiri? na kama siyo wa dhahiri, basi si ubaguzi kwa taathira?
  Je haijengi matabaka hapa?

  Misamaha ya kodi:
  Bunge limepitisha sheria juu ya misamaha ya kodi ambapo mwekezaji akiwekeza dola 100,000 atapata msamaha wa kutolipa kodi (hata akipata faida) kwa miaka 10; lakini Mtanzania aliyekwisha wekeza mtaji wa kiasi hicho analipa kodi zote zinazostahili. Kisingizio eti uwekezaji maalum na project cycle inaonyesha kuwa kurudisha mtaji inachukua miaka 8. Hii ni ajabu – kuna mjinga gani anaweza kuwekeza dola 100,000 (Tshs 150,000,000) halafu asubiri miaka minane kurudisha fedha zake. Hivi basi moja la abiria linagharimu kiasi gani? Hivi semi-trailler moja Iveco inagharimu kiasi gain? Je hawa wamesamehewa kodi?
  Ikumbukwe pia kuwa kwa uwekezaji unaolenga kilimo, maeneo makubwa ya vijiji yanayofaa kwa kilimo yatachuliwa na kama kuna fidia yoyote, itakuwa ndogo sana.
  Kuna kitu kimefichika ndani; Wabunge wengi wanataka kuchukua maeneo makubwa kwa ajili ya kilimo ndiyo maana wameziba maskio na akili zao na kupitisha misamaha hiyo wakijua kuwa wao ndio watanufaika zaidi!

  Kisingizio cha misamaha ya kodi kusaidia kuchochea uchumi Tundu Lisu alinukuu ripoti mbalimbali za nje na ndani zinazoonyesha kuwa misamaha hiyo haisaidii sana. Naibu waziri akajikita kwenye ripoti moja tu ya benki ya dunia. Kumbuka hii ni benki – lazima itoe mikopo ili iweze kuishi hivyo sera yoyote itakayowezesha ipate wateja wa kukopa, itapigiwa debe. Ndiyo maana si sahihi sana kuzingatia ripoti ya benki kuu. Ebu ona Benjamin William Mkapa alivyojuta:
  Ex-president of Tanzania Benjamin Mkapa nicely summed up his experience and that of many other countries: “We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us.”

  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]Written by Roberto Savio / Inter Press Service
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]Wednesday, 19 August 2009 21:16
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Hayo ni machozi ya mamba ya Mkapa!
  Halafu nyuma ya naibu waziri wa viwanda na biashara alikaa mbunge mmoja sijui ni wa wapi –kazi yake kupiga meza tu! Sijui hiyo ndiyo kazi waliyomtuma wapiga kura wake – aibu tupu!

  Pamoja na hoja zote zinazotolewa na ushahidi wake, bunge linaishia kupitisha mambo mazito yatakayoendelea kumdidimiza mwananchi wa kawaida kwa kusema ndiyoooooo!!! Tena ndiyo yenye kubwagiza ndiyoooooiiOOOOOooooOOOOoooiioo! (ningekuwa najua kuandika mziki ningeweka zile alama za muziki wa namna wabunge wanavyopitisha sheria)
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Maumivu ya kichwa
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Yule Mbunge anaitwa Gosbert Balndes ni kutoka moja ya majombo moani Kagera alitangzwa mshindi kwa kutumia mabomu ya FFFu na kisha kubebwa na garu kutoka jimboni kwake na gari chini ya ulinzi mkali hadi Mwanza kutokana na kiwango cha wizi wa kura kilichofanyika.
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kama ni huyo, ni mbunge wa Karagwe. Masikini wana karagwe, walimuacha yule kijana Kahangwa!
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Oooooh.....umenifumbua macho
   
Loading...