Watanzania waibuka kidedea mbio za Olimpiki Marathon! - wafanikiwa kumaliza hadi mwisho kabisa

Bado hizi kauli zinatuchelewesha kufanya vitu vya maana, kila kitu serikali serikali ifanye hiki na kile, jua linachomoza jua linazama. Ni lini tutaanza kusema mmoja mmoja nahitaji kujitoa kwa ajili ya michezo ijayo ya olympic 2016 nchini brazil ili nirudi na medali ya dhahabu? Ni lini tutaanza kujiwekea malengo ya kutaka kuitangaza nchi yetu kupitia michezo na mambo mengine yanayojumuisha nchi nyingi? Ni lini basi, ni lini, ni lini ......? Kama watu wanajua umuhimu wa kujituma katika kazi zao na kujinyakulia zawadi kemu kemu kwa faida yao na familia zao basi taratibu hii mentality ya watu (pamoja na viongozi wetu) kudharau fani za michezo (siyo michezo tu) itakuwa ndo mwanzo wa watu wengi kukaa na kubweteka wakisubiri serikali iwafanyie kitu. Lets wake up and use any chances!! Watu wakianzia ndani kuvunja record za kitaifa, africa then tutakuwa tumepiga hatua kubwa.

Unadhani ingekuwa hawajitolei, hata hao wa kwenda Olympic wangepatikana?

Umesikiliza mahojiano ya waogeleaji wa Tanzania waliokwenda Olympic mwaka huu? Wanasema wameanza kujifunza wao wenyewe na familia zao bila ya msaada wowote wa serikali hadi hapo palipofika.

Kujitoa na kujitolea imo, lakini kipaji kitupu bila ya msaada wa kiufundi hautufikishi mbali. Ndio yale unayaona wanashindwa katika mchujo wa mwanzo.
 
Kama kukimbia kooote huko ni kuwania dhahabu wakimbiaji wetu naona wanaona hamna haja ya kusumbuka hivyo wakati pale Geita, Kakora na Buzwagi kuna dhahabu ya kutosha tunaweza hata kupata tani kumi, ni bora kuachana na hizo dhahabu zao tukaenda tu kuchimba na tusishindane tena olympic
 
Mkuu,
Wakijibu hivyo tuwaambie kabisa hatujaridhishwa na majibu kabisa na wala hatuziamini kazi za mikono yenu, watoke au siku wasipeleke wanamichezo kama hakuna maandalizi, kama maandalizi ya medali yanaanza leo hapo sawa!
ni kwa sababu tu hatuna nafasi ya kuwachapa viboko kwa sababu hawajijui kama hawajui na watalazimisha kubaki madarakani kwa hali yeyote ile.shame on them all, wakati mwingine wanaoqualify sio wanaopelekwa mashindanoni.
 
ni kwa sababu tu
hatuna nafasi ya kuwachapa viboko kwa sababu hawajijui kama hawajui na
watalazimisha kubaki madarakani kwa hali yeyote ile.shame on them all,
wakati mwingine wanaoqualify sio wanaopelekwa mashindanoni.

Lazima tuwape mitihani ya kupima walichofanikiwa kupata wanamichezo watakaoweza kuleta medali wote ili kuhakikisha kuzuia kupata aibu nyingine mpya, tusiwadekeze kabisa, hicho ndicho kilichobaki!
 
Back
Top Bottom