Watanzania tuwe macho

Watanzania tuwe macho

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
WATANZANIA TUWE MACHO
Jumatatu, 25 Febr, 2019

Nimemsikiliza Dk. Suleiman Kisango Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza sababu za kuanguka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani ambapo katika siku za karibuni Dola moja ya Marekani imebadilishwa kwa hadi shilingi 2,415 za Tanzania. Hiki ni kiwango kikubwa kuwahi kutokea.

Moja ya sababu zilizotajwa kusababisha kuanguka kwa shilingi yetu ni maneno yanayosemwa na wanasiasa yanayoashiria kuwa Tanzania kuna hali mbaya inayochagizwa na mauaji ya watu yanayofanywa na Serikali, kuanguka kwa uchumi, unyanyasaji mkubwa dhidi ya wawekezaji, utawala wa kidikteta nakadhalika.

Kama kweli hii ni sababu muhimu kuna kila sababu za sisi Watanzania kujiuliza kama wanaomwaga sumu hii wanatusaidia ama wanatuangamiza?

Wanasiasa wa upinzania akina Tundu Lissu na Zitto Kabwe ambao kwa sasa wameacha majukuku yao ya kuhudumia wananchi na badala yake wanafanya kampeni ya kumwaga sumu dhidi ya Rais Magufuli na kuichafua nchi. Bila shaka wanahusika na kuanguka kwa thamani ya shilingi yetu.

Na ndio hao hao wanapoona mbao za viwango vya kubadilisha fedha zinaonesha kuanguka kwa shilingi wanashangilia na kupanga ziara za kupita kwa mabeberu kutangaza mafanikio ya kampeni yao ya kuidhohofisha Serikali ya Tanzania.

Halafu wanaongea upuuzi kabisa kuwa wao hawaichafui nchi bali wanashughulika na Serikali iliyopo madarakani. Swali dogo tu anayehudumia wananchi ni nchi au ni Serikali iliyopo madarakani?

Kama kweli tunakubaliana na hoja kwamba Rais ni kioo cha nchi, hivi kioo cha nchi kikichafuka nchi itakuwa salama?

Ndio maana nasema Watanzania tuwe macho, hawa watu wanaofanya kampeni hizi leo tupo baadhi tunawashangilia lakini ipo siku tutalia na wakati huo tutakuwa tumefikia mahali ambapo ni pagumu zaidi.

Naipongeza Serikali kwa jinsi inavyochukua hatua dhidi ya wanasiasa wanaotaka kuvuruga nchi, wanaodhani wanashika madaraka kwa kuharibu nchi. Kwenye suala la kulinda maslahi ya nchi hatupaswi kucheka na nyani.

Navipongeza vyombo vya dola kwa hatua vinazochukua dhidi ya wavunja sheria. Waendelee kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria na wakikutwa na hatia wapate adhabu.

Na sisi Watanzania tuwakatae watu hawa na kampeni yao chafu dhidi ya nchi yetu. Leo hii shilingi inaanguka kwa namna yoyote bei ya bidhaa inapanda mwisho wa siku mnunuzi wa bidhaa ambaye ni mtanzania wa kawaida ndio anayeumia.

Nawapongeza Watanzania ambao wamekuwa wakiwapinga wanasiasa hawa wanaofanya kampeni ya kuichafua nchi yetu na Rais wetu. Maana kila Zitto Kabwe anapoweka upuuzi wake kwenye mitandao ya kijamii au anapofanya mahojiano kama aliyoyafanya juzi na Sudi Mlete wa DW wapo wengi waliompinga kwa kumueleza ukwei kuwa anatumiwa na mabeberu kumiuliza Tanzania. Halikadhalika wapo ambao wameendelea kumshambulia Tundu Lissu kila kampeni yake inaporushwa kwenye mitandao ya kijamii. Huku ndio kujitambua kwenyewe.

Nawapongeza waandishi wa habari ambao wamekataa kuwa njia ya kueneza upuuzi wa akina Zitto Kabwe na wenzao. Ukiangalia kwa umakini utagundua ni vyombo vya habari vya nje ya nchi tu ndivyo vinatumiwa na wanasiasa.

Nilikuwa namuangalia Sudi Mlete akimhoji Zitto Kabwe na Zitto akawa anadanganya eti Serikali ya Tanzania ina mpango wa kutia saini Mkataba wa kinyonyaji na Jumuiya ya Ulaya uitwao EPA na kwamba yeye na wenzake wanapinga, wakati ukwei ni kwamba Serikali ya Tanzania ndio iliyokataa kutia saini mkataba huo wakati Kenya imekubali na Rwanda imeonesha kuwa tayari kutia saini. Na kwamba hadi sasa Umoja wa Ulaya umekasirishwa na kitendo cha Tanzania kukataa kutia saini mkataba huo ambao una madhara kwa mpango wa ujenzi wa viwanda.

Mwisho nawaomba Watanzania tuendelee kuwa macho na wanasiasa hawa ambao wakati nchi yetu inapambana kuingia katika uchumi wa kati, uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu, tunakomesha rushwa, tunakusanya kodi, tunahimizana kuzalisha mali kwa wingi na tunadhibiti matumizi ya hovyo, wao wanatukwamisha.

Nawatakia Jumatatu njema.

Joshua Salitoni
Dar es Salaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe hata Hapo ulipo umechangia kushusha thamani ya shilingi jaribu kua mkweli na usiegemee upande wowote unalaumu wapinzani kua hawahudumii wananchi wakati unajua wazi wamezuiliwa wasifanye shughuli za kisiasa kuhusu huyo TAL unamuonea bureee mtu katoka wodini juzi tu na je alichotendewa Ni sawa?ana makosa gani akilalamika kua hakutendewa haki Mimi niwaombe Watanzania tuwe wakweli tusiongee kwa kujipendekeza ili Hali unajua wazi unaongea kwa minajili ya kujionesha wewe Ni mwema mno tuwe wakweli

Kaa macho mwenyewe na jiwe wako. Sisi tunamtafuta Ben Saanane, waliomshambilia Lisu, waliomuua Gofrey Luena, Alphonce Mawazo, Azory na Daniel.
 
Mnalo safari hii. Endeleeni kukipaka mavi kioo chenu halafu mseme wengine ndio wanakichafua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye rushwa hapo na matumizi mabaya ya fedha umesema uongo...

Embu fanya kuwa mkweli trillion 1.5 zilifanya kazi gani? Mbona mmekuwa mkificha hili suala kila kukicha
 
Pia ungetufahamisha sababu za hao wanasiasa kuamua kuichafua nchi wanapokua huko kwa hao mabeberu. Iwapo mngeruhusu waongee na wafuasi wao kupitia mikutano yao ya kisiasa ambayo ipo kisheria na kutoa hizo nyongo zao, wangepata wapi huo muda?

Hii ni sawa na wewe kumwaga mboga na mwenzako nae akaamua kumwaga ugali. Haiwezekani wewe ufanye siasa muda wote halafu mshindani wako hutaki afanye! Sasa utajipima na kujisahihisha kwa kutumia chombo gani? Baadhi ya mambo hasa haya ya kisiasa, hamna budi kujifunza tu kwa JK.
 
WATANZANIA TUWE MACHO
Jumatatu, 25 Febr, 2019

Nimemsikiliza Dk. Suleiman Kisango Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza sababu za kuanguka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani ambapo katika siku za karibuni Dola moja ya Marekani imebadilishwa kwa hadi shilingi 2,415 za Tanzania. Hiki ni kiwango kikubwa kuwahi kutokea.

Moja ya sababu zilizotajwa kusababisha kuanguka kwa shilingi yetu ni maneno yanayosemwa na wanasiasa yanayoashiria kuwa Tanzania kuna hali mbaya inayochagizwa na mauaji ya watu yanayofanywa na Serikali, kuanguka kwa uchumi, unyanyasaji mkubwa dhidi ya wawekezaji, utawala wa kidikteta nakadhalika.

Kama kweli hii ni sababu muhimu kuna kila sababu za sisi Watanzania kujiuliza kama wanaomwaga sumu hii wanatusaidia ama wanatuangamiza?

Wanasiasa wa upinzania akina Tundu Lissu na Zitto Kabwe ambao kwa sasa wameacha majukuku yao ya kuhudumia wananchi na badala yake wanafanya kampeni ya kumwaga sumu dhidi ya Rais Magufuli na kuichafua nchi. Bila shaka wanahusika na kuanguka kwa thamani ya shilingi yetu.

Na ndio hao hao wanapoona mbao za viwango vya kubadilisha fedha zinaonesha kuanguka kwa shilingi wanashangilia na kupanga ziara za kupita kwa mabeberu kutangaza mafanikio ya kampeni yao ya kuidhohofisha Serikali ya Tanzania.

Halafu wanaongea upuuzi kabisa kuwa wao hawaichafui nchi bali wanashughulika na Serikali iliyopo madarakani. Swali dogo tu anayehudumia wananchi ni nchi au ni Serikali iliyopo madarakani?

Kama kweli tunakubaliana na hoja kwamba Rais ni kioo cha nchi, hivi kioo cha nchi kikichafuka nchi itakuwa salama?

Ndio maana nasema Watanzania tuwe macho, hawa watu wanaofanya kampeni hizi leo tupo baadhi tunawashangilia lakini ipo siku tutalia na wakati huo tutakuwa tumefikia mahali ambapo ni pagumu zaidi.

Naipongeza Serikali kwa jinsi inavyochukua hatua dhidi ya wanasiasa wanaotaka kuvuruga nchi, wanaodhani wanashika madaraka kwa kuharibu nchi. Kwenye suala la kulinda maslahi ya nchi hatupaswi kucheka na nyani.

Navipongeza vyombo vya dola kwa hatua vinazochukua dhidi ya wavunja sheria. Waendelee kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria na wakikutwa na hatia wapate adhabu.

Na sisi Watanzania tuwakatae watu hawa na kampeni yao chafu dhidi ya nchi yetu. Leo hii shilingi inaanguka kwa namna yoyote bei ya bidhaa inapanda mwisho wa siku mnunuzi wa bidhaa ambaye ni mtanzania wa kawaida ndio anayeumia.

Nawapongeza Watanzania ambao wamekuwa wakiwapinga wanasiasa hawa wanaofanya kampeni ya kuichafua nchi yetu na Rais wetu. Maana kila Zitto Kabwe anapoweka upuuzi wake kwenye mitandao ya kijamii au anapofanya mahojiano kama aliyoyafanya juzi na Sudi Mlete wa DW wapo wengi waliompinga kwa kumueleza ukwei kuwa anatumiwa na mabeberu kumiuliza Tanzania. Halikadhalika wapo ambao wameendelea kumshambulia Tundu Lissu kila kampeni yake inaporushwa kwenye mitandao ya kijamii. Huku ndio kujitambua kwenyewe.

Nawapongeza waandishi wa habari ambao wamekataa kuwa njia ya kueneza upuuzi wa akina Zitto Kabwe na wenzao. Ukiangalia kwa umakini utagundua ni vyombo vya habari vya nje ya nchi tu ndivyo vinatumiwa na wanasiasa.

Nilikuwa namuangalia Sudi Mlete akimhoji Zitto Kabwe na Zitto akawa anadanganya eti Serikali ya Tanzania ina mpango wa kutia saini Mkataba wa kinyonyaji na Jumuiya ya Ulaya uitwao EPA na kwamba yeye na wenzake wanapinga, wakati ukwei ni kwamba Serikali ya Tanzania ndio iliyokataa kutia saini mkataba huo wakati Kenya imekubali na Rwanda imeonesha kuwa tayari kutia saini. Na kwamba hadi sasa Umoja wa Ulaya umekasirishwa na kitendo cha Tanzania kukataa kutia saini mkataba huo ambao una madhara kwa mpango wa ujenzi wa viwanda.

Mwisho nawaomba Watanzania tuendelee kuwa macho na wanasiasa hawa ambao wakati nchi yetu inapambana kuingia katika uchumi wa kati, uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu, tunakomesha rushwa, tunakusanya kodi, tunahimizana kuzalisha mali kwa wingi na tunadhibiti matumizi ya hovyo, wao wanatukwamisha.

Nawatakia Jumatatu njema.

Joshua Salitoni
Dar es Salaam

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipande tu iyo dola ili wanyonge tutie akili 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali la wewe kujiuliza kabla hauja post huu uzi ni je hayo mauaji na huo uminywaji wa democracy vipo/yapo au havipo
Kama jibu ni vipo/yapo basi hakuna sababu ya wewe kuwalalamikia hao wanasiasa ambao wanao yafichua hayo maovu ", kwa sababu wanaitakia nchi salama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ugaidi uliofanywa Kenya juzi haukutikisa shilingi ya Kenya ndio hiyo hard talk ya BBC iliyozungumza kaukweli kadogo juu ya Tz.

Uchumi unaporomoka kutokana na sera mbovu za ccm. Mzunguko wa hela umeminywa sana watu hawajengi tena, hawanywi, hawanunui unategemea nini? Bado bombardier hazijaanza kula uchumi wa nchi.
 
WATANZANIA TUWE MACHO
Jumatatu, 25 Febr, 2019

Nimemsikiliza Dk. Suleiman Kisango Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza sababu za kuanguka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani ambapo katika siku za karibuni Dola moja ya Marekani imebadilishwa kwa hadi shilingi 2,415 za Tanzania. Hiki ni kiwango kikubwa kuwahi kutokea.

Moja ya sababu zilizotajwa kusababisha kuanguka kwa shilingi yetu ni maneno yanayosemwa na wanasiasa yanayoashiria kuwa Tanzania kuna hali mbaya inayochagizwa na mauaji ya watu yanayofanywa na Serikali, kuanguka kwa uchumi, unyanyasaji mkubwa dhidi ya wawekezaji, utawala wa kidikteta nakadhalika.

Kama kweli hii ni sababu muhimu kuna kila sababu za sisi Watanzania kujiuliza kama wanaomwaga sumu hii wanatusaidia ama wanatuangamiza?

Wanasiasa wa upinzania akina Tundu Lissu na Zitto Kabwe ambao kwa sasa wameacha majukuku yao ya kuhudumia wananchi na badala yake wanafanya kampeni ya kumwaga sumu dhidi ya Rais Magufuli na kuichafua nchi. Bila shaka wanahusika na kuanguka kwa thamani ya shilingi yetu.

Na ndio hao hao wanapoona mbao za viwango vya kubadilisha fedha zinaonesha kuanguka kwa shilingi wanashangilia na kupanga ziara za kupita kwa mabeberu kutangaza mafanikio ya kampeni yao ya kuidhohofisha Serikali ya Tanzania.

Halafu wanaongea upuuzi kabisa kuwa wao hawaichafui nchi bali wanashughulika na Serikali iliyopo madarakani. Swali dogo tu anayehudumia wananchi ni nchi au ni Serikali iliyopo madarakani?

Kama kweli tunakubaliana na hoja kwamba Rais ni kioo cha nchi, hivi kioo cha nchi kikichafuka nchi itakuwa salama?

Ndio maana nasema Watanzania tuwe macho, hawa watu wanaofanya kampeni hizi leo tupo baadhi tunawashangilia lakini ipo siku tutalia na wakati huo tutakuwa tumefikia mahali ambapo ni pagumu zaidi.

Naipongeza Serikali kwa jinsi inavyochukua hatua dhidi ya wanasiasa wanaotaka kuvuruga nchi, wanaodhani wanashika madaraka kwa kuharibu nchi. Kwenye suala la kulinda maslahi ya nchi hatupaswi kucheka na nyani.

Navipongeza vyombo vya dola kwa hatua vinazochukua dhidi ya wavunja sheria. Waendelee kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria na wakikutwa na hatia wapate adhabu.

Na sisi Watanzania tuwakatae watu hawa na kampeni yao chafu dhidi ya nchi yetu. Leo hii shilingi inaanguka kwa namna yoyote bei ya bidhaa inapanda mwisho wa siku mnunuzi wa bidhaa ambaye ni mtanzania wa kawaida ndio anayeumia.

Nawapongeza Watanzania ambao wamekuwa wakiwapinga wanasiasa hawa wanaofanya kampeni ya kuichafua nchi yetu na Rais wetu. Maana kila Zitto Kabwe anapoweka upuuzi wake kwenye mitandao ya kijamii au anapofanya mahojiano kama aliyoyafanya juzi na Sudi Mlete wa DW wapo wengi waliompinga kwa kumueleza ukwei kuwa anatumiwa na mabeberu kumiuliza Tanzania. Halikadhalika wapo ambao wameendelea kumshambulia Tundu Lissu kila kampeni yake inaporushwa kwenye mitandao ya kijamii. Huku ndio kujitambua kwenyewe.

Nawapongeza waandishi wa habari ambao wamekataa kuwa njia ya kueneza upuuzi wa akina Zitto Kabwe na wenzao. Ukiangalia kwa umakini utagundua ni vyombo vya habari vya nje ya nchi tu ndivyo vinatumiwa na wanasiasa.

Nilikuwa namuangalia Sudi Mlete akimhoji Zitto Kabwe na Zitto akawa anadanganya eti Serikali ya Tanzania ina mpango wa kutia saini Mkataba wa kinyonyaji na Jumuiya ya Ulaya uitwao EPA na kwamba yeye na wenzake wanapinga, wakati ukwei ni kwamba Serikali ya Tanzania ndio iliyokataa kutia saini mkataba huo wakati Kenya imekubali na Rwanda imeonesha kuwa tayari kutia saini. Na kwamba hadi sasa Umoja wa Ulaya umekasirishwa na kitendo cha Tanzania kukataa kutia saini mkataba huo ambao una madhara kwa mpango wa ujenzi wa viwanda.

Mwisho nawaomba Watanzania tuendelee kuwa macho na wanasiasa hawa ambao wakati nchi yetu inapambana kuingia katika uchumi wa kati, uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu, tunakomesha rushwa, tunakusanya kodi, tunahimizana kuzalisha mali kwa wingi na tunadhibiti matumizi ya hovyo, wao wanatukwamisha.

Nawatakia Jumatatu njema.

Joshua Salitoni
Dar es Salaam

Sent using Jamii Forums mobile app
ndugu, risasi 16 ndani ya mwili wa binadamu ndiyo concern kubwa ya humankind.

huhitaji kuua watu eti ndiyo upate maendeleo.... ukifanya hivi hauko tofauti na mchawi anayeroga watu ili atajirike.
pia hauko tofauti na mkoloni aliyeleta unayoyaita "maendeleo" leo lakini alikandamiza wananchi. Nyerere & co wangekuwa na fikra kama hizi zenu Uhuru wa Tanganyika tungeusikia bombani tu!
 
Na wewe hata Hapo ulipo umechangia kushusha thamani ya shilingi jaribu kua mkweli na usiegemee upande wowote unalaumu wapinzani kua hawahudumii wananchi wakati unajua wazi wamezuiliwa wasifanye shughuli za kisiasa kuhusu huyo TAL unamuonea bureee mtu katoka wodini juzi tu na je alichotendewa Ni sawa?ana makosa gani akilalamika kua hakutendewa haki Mimi niwaombe Watanzania tuwe wakweli tusiongee kwa kujipendekeza ili Hali unajua wazi unaongea kwa minajili ya kujionesha wewe Ni mwema mno tuwe wakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli hakuna mwanasiasa aliezuiliwa kufanya siasa kilichoelekezwa ni kilwa mwanasiasa kufanya siasa jimboni kwake na sio kwingineko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom