Watanzania tutathimini mienendo michango ya wabunge wetu bungeni

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Nakerwa sana na tabia za wabunge wa ccm wakati wa kuchangia mijadala bungeni. Hii fashion ya kutumia karibu robo ya muda wa kuchangia kumsifia rais naona ni waste of time. Kumbe kikao Cha budget kinaweza kufupishwa muda na kufanyika kwa mwezi 1½ tu.

Mbunge anapewa dk 15 achangie MASUALA ya msingi lakini yeye dk karibu 7....8 anatumia kumsifia rais. Ndio maana hawawezi kusimamia serikali na badala yake ni kujipendekeza pendekeza tu huku miradi ikipigwa Hela kiasi CAG Kila mwaka kirudi kubainisha hasara ya mabilioni kupotea.

Wabunge wetu Wana mizaha sana. Wanapoteza muda makusudi Ili siku ziwe nyingi posho na marupurupu ziongezeke. Ebu wananchi tuamke tukemee tabia hii.
 
Wakati anasifiwa Magufuli hadi kufafananishwa na Mungu hamkuona? ama kwa kuwa leo rungu na bakuli la asali wanalamba wengine? mkae kwa kutulia gang.
 
Serikali imeshapanga mambo yake

Sidhani kama kuongea kwa ukali au kufoka foka kwa mbunge wako wa jimbo kunaweza kubadili mipango ya serikali

Hawa wabunge ni kama wanaenda kubariki tu mchakato lakini kila kitu kimeshapangwa
 
Mkuu hakuna kitu kibaya kama kufanyiwa hisani, yaan lazima umtumikie aliekupa hisani na sio vinginevyo!! Usitegemee mbunge wa CCM apambane kwa hoja na serikali kwaajil ya maslahi ya wananchi!!! Washakwambia... Maslahi ya chama kwanza mengine baadae.
 
Nakerwa sana na tabia za wabunge wa ccm wakati wa kuchangia mijadala bungeni. Hii fashion ya kutumia karibu robo ya muda wa kuchangia kumsifia rais naona ni waste of time. Kumbe kikao Cha budget kinaweza kufupishwa muda na kufanyika kwa mwezi 1½ tu. Mbunge anapewa dk 15 achangie MASUALA ya msingi lakini yeye dk karibu 7....8 anatumia kumsifia rais. Ndio maana hawawezi kusimamia serikali na badala yake ni kujipendekeza pendekeza tu huku miradi ikipigwa Hela kiasi CAG Kila mwaka kirudi kubainisha hasara ya mabilioni kupotea.
Wabunge wetu Wana mizaha sana. Wanapoteza muda makusudi Ili siku ziwe nyingi posho na marupurupu ziongezeke. Ebu wananchi tuamke tukemee tabia hii.
Miye siku hizi hata taarifa ya habari siangalii maana hata mtu alijifungua salama utasikia ni Kwa juhudi za Mhe Dokta Rais Samia Suluhu Hassan ndo nikaweza kupanua miguu vizuri ndo mtoto akatoka bila shida
 
Watanzania gani unaowasema? Maama watanzania wa Tanzania hawajui hata kama Kuna Bunge linaendelea.
 
Miye siku hizi hata taarifa ya habari siangalii maana hata mtu alijifungua salama utasikia ni Kwa juhudi za Mhe Dokta Rais Samia Suluhu Hassan ndo nikaweza kupanua miguu vizuri ndo mtoto akatoka bila shida
Mzee sikiliza DW au BBC ni za mabeberu lkn unapata hbr na facts za msingi. Sina kumbukumbu mara ya mwisho nimesikiliza hbr au kuangalia hbr za vyombo vyetu ilikua mwaka gan!!
 
Back
Top Bottom