Michango ya wabunge wetu ipo chini sana, hawana HOW kwenye michango yao

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Na Thadei Ole Mushi.

Nimekuwa nikifuatilia michango ya wabunge wetu bungeni naona tuna tatizo kubwa mahali. Mbunge anapewa dakika kumi kuchangia mfano wizara ya viwanda na Biashara.

Dakika tano anatumia kuwashambulia Chadema. Dakika tatu anasifia Serikali ya awamu ya tano, dakika Moja anasema tufufue viwanda na dakika Moja anaunga mkono budget dakika kumi zinakuwa zimeisha.

Michango ya wabunge wetu ipo chini sana, hawana HOW kwenye michango yao, hawajatafiti kabla ya kuchangia na hawana connection ya Mambo mengi. Miaka miwili mitatu tulikuwa na shida kubwa hapa ya soko la Korosho,Pamba, Njegere nk. Ni Mchango wa Mbunge gani uliouona umeleta tija kwenye maeneo haya?

Narudia

Ni wakati wa CCM kumsaidia Mh Rais kuachana na wabunge ambao aliwarithi awamu nyingine. Bunge ni chombo Cha muhimu Sana kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa lolote lile. Tunapopeleka watu dhaifu pale kichwani tunajichelewesha wenyewe kwenye maaendeleo yetu.

Umefika wakati Sasa wa CCM kutusaidia ku screen watia nia na kushawishi watu wenye quality kugombea. Tukumbuke wabunge wetu ndio kitalu Cha Baraza la mawaziri ambao ndio washauri wakuu wa Rais wetu. 2015 Mh Rais alipata wakati mgumu Sana kuteua Baraza la mawaziri kutokana na kupeleka wabunge wa Low Quality Bungeni. Ndio maana ilibidi ateue wengine toka njee ya wabunge wa kuchaguliwa.

Natamani watia nia waitwe kwa makundi pale Lumumba wapeleke CV zao, waangaliwe waliwahi kufanya nn, na wapimwe Exposure waliyonayo kitaifa na kimataifa. Kuna vishoia wengi Sana wameanza kujipitisha pitisha nao wanataka kugombea, yaani Ubunge wa Tanzania tumeurahisha Sana.... hata wajinga wanautamani.

Naomba Bunge likivunjwa tu team maalumu itengenezwe ikatutafutie watu huko mtaani wanaoweza kutupeleka kwa kasi tuifikie South Korea, Singapore nk. Tusiishie kusema tu Kuna kipindi Singapore ilikuwa sawa na sisi.... Haitusaidii Sana.

Prof Lumumba wa Kenya katika Moja ya mihadhara yake aliwahi kusema nanukuu "In Africa those with powers have No ideas and those with ideas have No power" hili ni tatizo kubwa kwa nchi nyingi Africa.

Ukiniuliza wanapitiaga wapi hadi wanafika Bungeni siwezi kukuambia. Tunaweza kuwapa kazi nyingine za kufanya ila si kwenda Bungeni, chonde chonde CCM yangu mna jukumu la kuifikisha nchi hii katika Uchumi wa kati. Hatutaweza kamwe kufikia huko kwa aina ya wabunge wengi tulionao....

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiona utajiri na Umaskini vipo sehemu Moja Basi elewa Kuna tatizo mahali. Haiwezekani kwa utitiri wa utajiri tulionao bado tushindwe kuwapa wananchi wetu maisha ya kiwango Cha juu inawezekana hata Afya ikatolewa bure kabisa. Mpaka Leo tunatafuta maji, mpaka leo Kuna watu wanasomea chini ya miti nk.

Ole Mushi
0712702602.

Hasta la victoria siempre
 
Ujinga ndo mtaji wa chama chetu hiki.. hatutaki wajuaji
Tunataka mtupatie watu ambao wataisaidia nchi ya Tanzania na siyo kukisaidia hicho mnachokiita chama chenu.Busara ni chama kutokutuletea watu wake tuwalipe kwa kodi zetu, wahudumieni watetezi wa chama,sisi tunataka wabunge toka CCM waje kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao.
 
Well said, Tufike mahali tuchague viongizi wenye uelewa na ujuzi wa mambo. angalau wanaweza kutusaidia kwa kiwango fulani. kwa ujumla tunatatizo kubwa la kupata viongozi enye weledi na nia ya dhati ya kusoeza mbele Taifa letu.

Wakati mwingingine ukisikiliza michango ya wabunge unaona aibu kama Mtanzania. Sipendi kujilinganisha na Wakenya lakini wenzetu pamoja na ufisadi wao lakina wanachagua viongozi waelewa. Kenya huwezi kuwa Mbunge au Gavana kama huna. shahada na huwezi kuwa diwani (MCA) kama huna angalau dilpoma.

Hata kama wakati mwingine wasomi wanatuangusha lakini huwezi kuchagua class 7 awe mbunge kwa wakati huu. Nakumbuka marehemu Majimarefu MB wa Korogwe, std 7 na mganga wa kienyeji kweli. Watanzania tubadilike tutambue umuhimu wa elimu katika uongozi na maendeleo yetu.
 
Huo ndiyo mtaji mkubwa wa CCM,imejitahidi kuwekeza mpaka wanachama wa aina hiyo.

Ambao wao ukiwapa Kofia,T-shirt , Kanga na Madera basi watakuchagulia wabunge wa aina ya Msukuma,Kibajaji na wale wanaofanana nao.
 
CCM INA NAFASI YA KUBADILI AINA YA WABUNGE ILIYONAYO.

Na Mushi.

Nimekuwa nikifuatilia michango ya wabunge wetu bungeni naona tuna tatizo kubwa mahali. Mbunge anapewa dakika kumi kuchangia mfano wizara ya viwanda na Biashara.

Dakika tano anatumia kuwashambulia Chadema.
Dakika tatu anasifia Serikali ya awamu ya tano, dakika Moja anasema tufufue viwanda na ,
Dakika Moja anaunga mkono budget
dakika kumi zinakuwa zimeisha.

Michango ya wabunge wetu ipo chini sana, hawana HOW kwenye michango yao, hawajatafiti kabla ya kuchangia na hawana connection ya Mambo mengi. Miaka miwili mitatu tulikuwa na shida kubwa hapa ya soko la Korosho,Pamba, Njegere nk. Ni Mchango wa Mbunge gani uliouona umeleta tija kwenye maeneo haya?

Narudia

Ni wakati wa CCM kumsaidia Mh Rais kuachana na wabunge ambao aliwarithi awamu nyingine. Bunge ni chombo Cha muhimu Sana kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa lolote lile. Tunapopeleka watu dhaifu pale kichwani tunajichelewesha wenyewe kwenye maaendeleo yetu.

Umefika wakati Sasa wa CCM kutusaidia ku screen watia nia na kushawishi watu wenye quality kugombea. Tukumbuke wabunge wetu ndio kitalu Cha Baraza la mawaziri ambao ndio washauri wakuu wa Rais wetu. 2015 Mh Rais alipata wakati mgumu Sana kuteua Baraza la mawaziri kutokana na kupeleka wabunge wa Low Quality Bungeni. Ndio maana ilibidi ateue wengine toka njee ya wabunge wa kuchaguliwa.

Natamani watia nia waitwe kwa makundi pale Lumumba wapeleke CV zao, waangaliwe waliwahi kufanya nn, na wapimwe Exposure waliyonayo kitaifa na kimataifa. Kuna vishoia wengi Sana wameanza kujipitisha pitisha nao wanataka kugombea, yaani Ubunge wa Tanzania tumeurahisha Sana.... hata wajinga wanautamani.

Naomba Bunge likivunjwa tu team maalumu itengenezwe ikatutafutie watu huko mtaani wanaoweza kutupeleka kwa kasi tuifikie South Korea, Singapore nk. Tusiishie kusema tu Kuna kipindi Singapore ilikuwa sawa na sisi.... Haitusaidii Sana.

Prof Lumumba wa Kenya katika Moja ya mihadhara yake aliwahi kusema nanukuu "In Africa those with powers have No ideas and those with ideas have No power" hili ni tatizo kubwa kwa nchi nyingi Africa.

Ukiniuliza wanapitiaga wapi hadi wanafika Bungeni siwezi kukuambia. Tunaweza kuwapa kazi nyingine za kufanya ila si kwenda Bungeni, chonde chonde CCM yangu mna jukumu la kuifikisha nchi hii katika Uchumi wa kati. Hatutaweza kamwe kufikia huko kwa aina ya wabunge wengi tulionao....

Kumbuka Mwigulu alitumbuliwa wizarani, amekaa benchi , kaamua kuweka phd yake pembeni akajiunga praise and worship team, karudishwa, hii inaonyesha Raisi hana chagua na wengi ni magarasha tu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiona utajiri na Umaskini vipo sehemu Moja Basi elewa Kuna tatizo mahali. Haiwezekani kwa utitiri wa utajiri tulionao bado tushindwe kuwapa wananchi wetu maisha ya kiwango Cha juu inawezekana hata Afya ikatolewa bure kabisa. Mpaka Leo tunatafuta maji, mpaka leo Kuna watu wanasomea chini ya miti nk.

Ole Mushi
0712702602.
 
Kazi yao kuu Ni kugonga meza Na kupongeza basi. Huku wakilipwa posho mbili kwa mpigo Dodoma yaani ya kujikimu Na ya makalio yaani sitting allowance duh.Ule Ni wizi mkubwa
 
Ukiniuliza wanapitiaga wapi hadi wanafika Bungeni siwezi kukuambia. Tunaweza kuwapa kazi nyingine za kufanya ila si kwenda Bungeni, chonde chonde CCM yangu mna jukumu la kuifikisha nchi hii katika Uchumi wa kati. Hatutaweza kamwe kufikia huko kwa aina ya wabunge wengi tulionao....
Kwa mfano Job Ndugai...
 
Wabunge wa Chadema mmejifucha Dar mnakula kodi za Watanzania

Majukumu yenu bungeni mmeyaacha
 
Back
Top Bottom