Watanzania tutafika kweli!

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
Jamani kwa hali hii mbona kila siku bora Jana? Hivi hii sikukuu iliyo mbele yetu italika kweli? Mbona kila mtu analia hali inazidi kuwa mbaya? Na biashara mbona zinazidi kufungwa tu, vijana hawapati ajira, mishahara haipandi, viwanda hatuvioni wiki mbili mfululizo nakutana na watu barabarani wanaongea wenyewe, jamani nauliza tutatoka kweli? Nani wa kumsaidia mwenzanke? Sasahivi unaweza tafuta chenji ya elfu kumi au elfu tano kwa muda wa dakika kadhaa na usipate.

Mungu wangu tuokoe
 
usiseme tanzania tutafika,sema mimi nitafika?,maana wapo waliofika
 
usiseme tanzania tutafika,sema mimi nitafika?,maana wapo waliofika
Unajua principality ya 50% inavyopaswa itimike?
Darasa likiwa na wanafunzi 40 na kati yao 50% au zaidi wakiwa ni viziwi mtu huruhusiwa kuliita lile darasa kuwa ni la viziwi. Naamini huyu kacheki asilimia pia
 
Wengi hatutafika na wale wachache watakaofika watafika wakiwa na majeraha ya kutosha.

Dereva mwenyewe kasema msimpangie kwahiyo hata akipitisha kwenye mitaro tutulie tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom