tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Jamii imetakiwa kuacha tabia ya unyanyapaa kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi hususani vijana. Badala yake iwape ushirikiano ili kuwafanya wajisikie vizuri pamoja na kupata nafasi ya kuonyesha walichonacho katika jamii wanazoishi.
Wito huo umetolewa na Daniel Moses muelimishaji rika kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma leo Jumamosi Agosti 16, 2025.
Moses amesema, vijana waliougua ugonjwa huo hujikuta wakikata tamaa kutokana na jamii inayowazunguka kutowathamini na kuwaona hawana tija kitu ambacho si kweli.
Soma pia: Kuna watu ambao hawapati maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU)
Amengeza kuwa jamii inapaswa kukumbuka kuwa vijana waliougua ugonjwa huo bado wanategemewa na taifa lakini pia wanahitaji kutimiza ndoto zao hivyo ni lazima jamii iwaunge mkono.
Kwa upande wake Agnes Williamu amesema Serikali na jamii kwa ujumla zinatakiwa kuandaa programu mbalimbali ili kuwaelimisha vijana wanaoishi na tatizo hilo kufahamu namna ya kuishi katika hali hii.
Lakini pia wale ambao hawajaugua wajengewe uwezo wa kujilinda ili kupunguza idadi ya vijana wanaougua tatizo hili katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia.