raymbilinyi
Member
- May 25, 2016
- 13
- 11
Watanzania tumekuwa tukilia kila uchwao kuhakikisha nchi yetu Tanzania inapata kiongozi bora, asiyependa rushwa, makini katika usimamiaji wa haki, mwenye kuheshimu kila mtu, mtu wa maadili, mpenda watu hasa wanyonge/wasiojiweza, msimizi mzuri wa sheria/katiba, msimamizi wa rasilimali na sifa kedekede ambazo tumekuwa tukimlilia Mungu atupatie kiongozi atakae tuvusha hapa na kutupeleka katika nchi ya uchumi wa kati.
Jibu la hili ni laisi sana maana Mungu kasikia kilio chetu katupatia Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli, kiongozi mwenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko makubwa katika nchi hii Tanzania ambayo ni nchi tajiri sana na yenye rasilimali nyingi kila pembe ya nchi. Nasababu kwanini nasema Dr. JPM ni kiongozi sahihi wakutuvusha hapa tulipo.......Nitajitahidi kila siku kufafanua kwanini nasema Tanzania sasa imepata kiongozi mzuri ambae anaweza kutuvusha hapa tulipokuwa tumekwama kama nchi......................... Fuatilia (SERIES 1)
SERIES:1. ANPAMBANA NA RUSHWA KWA VITENDO
Leo nitalifafanua hili tu la rushwa ambalo ni moja ya vitu mbavyo Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli amekuwa akipambana na wala rushwa, mafisadi, walanguzi, mchwa na wezi wa mali za umma. Rushwa ni adui namba moja wa haki hasa kwa watu wanyonge na pia ni kansa inayotafuna taifa lolote lile hasa kiuchumi.
Kwahiyo ni jambo baya ambalo limekuwa likitesa nchi nyingi sana duniani na limekuwa likisababisha na viongozi waliopo madarakani hasa ngaizi ya Urais kwa kushindwa kuchukua hatua au kuwa sehemu kwakushirikiana na wala rushwa na mafisadi. Lakini kwa nchi yetu Tanzania Rais wa awamu hii ya tano ndani ya miezi michache aliyokuwa madarakani ameweza kupambana na wala rushwa kwa vitendo bila ajizi, huruma na wala kumuonea mtu. Madhara yatokanayo na rushwa ni mengi sana kwa nchi yoyote ile duniani.
MADHARA YA RUSHWA
a). Kuifanya nchi kukosa fedha za kujiendesha maana pesa yote inabaki kwa watu na kuifanya serikali kushindwa kujiendesha kwa kuwahudumia wananchi.
b). Rushwa ni dui wa haki na hasa wanyonge maana wenye pesa husikilizwa zaidi kuliko mtu asie nacho. Rushwa hudhulumu haki za watu wasiojiweza.
c). Kusababisha miradi ya maendeleo kukwama au kujengwa chini ya kiwango maana pesa inayoelekezwa huliwa na wajanja wachache.
d). Husababisha vitu kupanda bei....Mfano mzuri ni sukali, wenye pesa hununua na kuhothi/kuficha sukali ili ipande bei.
e). Kupoteza ushindani maana hata wasio na sifa hupata kitu wasicho staihili. Mfano watoto wa vigogo kupata kazi kubwa katika mashirika bila hata ushindani na wengine.
f). Husababisha mali za wanyonge kudhulumiwa na watu wenye mapesa waliyoyapata kifisadi.
g). Huongeza ugumu wa maisha hasa kwa wanyonge.
h). Husababisha makampuni, mashirika na hata viwanda kufa.
i). HUsababisha rasilimali kupotea kilahisi mfano madini, samaki, wanyama wa polini n.k
j). Husababisha uharibifu wa kimazingira mfano ukataji miti kiholela kwa utoa hongo kwa wahusika na kuvuna pasipo utaratibu.
k). Husababisha uasi kama mauwaji, ujambazi, uvutaji madawa maana huachwa wauzaji kupitisha ndani ya nchi. maana weye pesa wanaweza kujiingiza katika kufadhiri hata ugaidi ndani ya nchi.
l). Husababisha uvunjivu wa maadili ya taifa
m). Husababisha ajali za kisembe.....matrafiki kupokea rushwa anashindwa kufanya ukaguzi vizuri.
n). Husabisha uchumi wa nchi kutokua kabisa kutokana na watu kukwepa kodi, kitu ambacho imesababisha nci nyingi za Afrika kubaki nyuma licha ya kuwa na rasilimali nyingi sana ambazo wamebalikiwa na Mungu.
NINI KIMEFANYWA NA MH. RAIS DR. J.P.MAGUFULI
1. Cha kwanza kaanza kwa kuhakikisha kila mmoja analipa kodi.
Nchi yetu Tanzania watu wasiowaaminifu kwa kushirikiana na wafanyakazi wa serikali na wafanya biashara wamekuwa wakikwepa kodi na kuisababishia nchi kukosa mapato. Nchi yoyote ile inategemea kodi lakini nchi yetu ilifikia hatua mbaya sana kwa zaidi ya makotena elfu mbili (2000) kupita bila kulipiwa kodi bandarini. Kila mmoja ameshuhudia jinsi Mh. Waziri Mkuu Cassim Majariwa alivyopambana na wakwepa kodi bila huruma katika nyanja zote bandaini na upakuaji wa mafuta. Sasa kila mtu analipa kodi kitu ambacho kimeababisha mapato kuongezeka kutoka Bilion 600 kwa mwezi hadi kufikia zaidi Trilioni moja.
2. Watumishi na wafanyakazi hewa
Nchi hii ilifika mahali pabaya sana hadi kufikia kuwa na watumishi hewa ndani ya taasisi za serikali na mashirika na kusababisha upotevu wa pesa za serikali. Watu wanalipwa mishahara wakati hawapo kiuhalisia kitu ambacho kinanyima fursa za vijana kupata ajira na kuisababishia serikali hasa kubwa sana kufikia karibu billion 16 kwa mwezi kitu ambacho chini ya uongozi wa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi sahihi wa saidizi wake na kubaini na kuokoa upotevu mkubwa wa pesa za walipa kodi kitu ambacho kinasababisha nchi kutoendelea.
3. Wanafunzi hewa.
Wizara ya elimu chini ya Mh. Prof. Joyce Ndalichako kafanya kazi yake vizuri sana katika sekta ya elimu kwa kubaini uozo mkubwa sana hasa kwenye bodi ya mikopo kwa kubaini wanafunzi hewa wanaochukuwa pesa bodi ya mikopo bila kuwa wanasoma darasani. Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli katoa maagizo maana yeye hashirikiani na wezi na wala rushwa hivyo hata ma waziri wanafanya kazi kuendana na kasi ya kiongozi mkuu wa nchi.
Hapa pia tumeona MH. Ally Salum Hapi na Mh Mrisho Gambo wameweza kubaini wanafunzi hewa katika shule za msingi na sekondari kitu ambacho walimu wakuu wameongeza idadi ya wanafunzi kwa lengo la kujipatia kipato kwa pesa serikali inatoa kugharamia elimu bure. Vijana hawa ambao ni ma DC na RC wamekuwa wakifanya kazi zao izuri sana na wanastahili hongera sana maana wanafanaya serikali iokoe pesa na pia kupata watu wenye sifa.
4. Kuanzishwa mahakama ya mafisadi
Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli amelisisitiza hili wakati wote wa kampeni zake na sasa bunge la bajeti llipitisha kwa kauli moja uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi nchini, yenye jukumu la kuwashughulikia mafisadi kwa haraka zaidi bila kuwachelewasha. Na wabathirifu wameshaanza kufikishwa mahakamani bila ya huruma au bila kujali ni wa chama chake au la na wengine kusimamishwa kazi. Taasisi nyingi na mashirika mengi yenye watendaji weneye tabia hizi katika kipindi hiki tutawashuhudia wakifikishwa mahakamani. Niwasihi watu waliokuwa na tabia hizi kuacha mara moja maana Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli hana ajizi wala huruma na walarushwa.
5. Kuanza kusafisha hadi kwenye Chama chake
Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli sio mtu mnafiki maana angekuwa kiongozi mwingine katika vita hii angechagua wakupigana nao lakini yeye bila ya kujali ameanza kusafisha chama cha mapinduzi (CCM) chama chake yeye mwenyewe maana anaimani nako kuna watu wasio safi ambao wanajihusisha na rushwa licha ya wengine kukimbilia vyama vingine vya upinzania baada kuona ujio wake. Tumeona UVCCM ikiwachukulia hatua walanguzi wote ndani ya chama hasa watu walioshiriki wizi ndani ya jumuiya pia bado baadhi ya makada kama James Rock Mwakibinga wakija na tuhuma nyingine nyingi sana juu ya jumuiya kitu ambacho nashauri uongozi wa juu wa chama ione haja wakutopuuza mawazo ya kada huyu maana nikama anafahamu mengi sana ya wafujaji wa pesa za jumuiya ya UVCCM.
Nimengi sana Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli anafanya na anaendelea kufanya katika eneo hili la rushwa ambalo lilikuwa kubwa sana katika nchi yetu nkusababisha wanyonge kukosa haki na maisha kupanda na pia kuifanya serikali ishindwe kujiendesha. Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli anapambana kwa vitendo katika haya ya rushwa jambo moja ni sisi watanzania wote tumuunge mkono katika vita hii ambayo ni kubwa sana maana ninadra sana viongozi wakuu wa nchi hasa za kiafrika kupambana na rushwa kubwa tena bila ajzi au uswaiba na mtu au kutoshirikiana nao.
Tuendelee kumuombea Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli aendelee hivi hivi maana anaweza akaamua kuiunga nao kama sisi hatutakuwa tukimsapoti katika vita hii ambayo ni kubwa sana maana mengi sana sijafafanua na kueleza uwizi unavyofanywa na watu waliopewa dhamana kutuongoza sisi. Ilitufikie nchi ya uchumi wa kati kama taifa laazima tuichukie hii tabia ya wizi, ufisadi na rushwa kwa kukemea, kufichua na hat kuwatia moyo na kuwanga mkono viongozi wetu pale wanapo chukua hatua ya kuwashughurikia walarushwa katika nchi.
USHAURI
Kwenye eneo hili ni shauri
1). Kuwafikisha mahakamani (Mahakama ya mafisadi) kwa haraka bila kuwachelewesha mara tu ushahidi ukikamilika.
2). Kutoa elimu ya uzalendo kwa wanafunzi ngazi zote kuanzia shule za msingi.
3). Kukagua akaunti na mali za watumishi na wafanya biashara wakubwa ilikubaini vyanzo vya mapato na kodi waliyokwishalipa.
4). Watumishi katika idara serikali watoe ripot zao za kazi kila mwezi kwa wakuu wao ili kama kuna mipango ovu iweze kuzuiliwa kabla ya kufika mbali.
5). Ukiharibu usihamishiwe sehemu nyingine bali usimamishwe na uchunguzi ufanyike na kufikishwa mahakani na kazi hiyo itolewe au ichukuliwe na mtu mwingine.
6). Uweke utaratibu mzuri wa kuwaashughurikia wezi wa mali za nchi pasipo kumuonea mtu ambae hajafanya kosa.
7). Katika katibu kipengele cha maadili ya watumishi wa serikali iangaliwe vizuri ili katiba inayotarajiwa utengenezwe kuhakikisha maovu ya naondolewa kwakuwekewa mfumo mzuri sana wa sera na sheria.
Leo niishie hapa maana eneo hili nipana sana. Kwauwekezaji huu unaofanywa na Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli kwakupambana na mafisadi kivitendo utaifanya nchi yetu kukua na kufikia uchumi wa kati chamsingi tumuunge mkono na tumpe muda mambo yetu yatakuwa safi.
Nitaendelea kueleza baadhi ya mambo mazuri yanafanya na kiongozi wetu Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ambae mie binafsi naamini ni zawadi tuliyoiomba muda mrefu na hatimae kiliochetu kimesikika na wakutufuta machozi sisi watanzania wanyonge ashapatikana. Asanteni woteeeee........
PIGA KAZI MAANA NDIO MSINGI WA MAENDELEO WA NCHI YOYOTE ILE ..........TANZANIA KWANZA.
By
Richard Mbilinyi