Watanzania tupende kufanya utalii wa ndani

FATUMA SELEMANI 24

New Member
Jul 13, 2021
2
0
Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii ikiongozwa na nchi ya Brazil. Lakini licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya kitalii ni chini ya asilimia mbili {2%} tu ya watanzania wanaotembelea katika vivutio hivyo ukilinganisha na wageni wanaokuja kuvitazama vivutio hivyo.

Zipo nchi ambazo huwa zinategemea watalii kutoka nchi nyingine kwa asilimia
(5%, 10%) na hazizidi asilimia (15% )ya watalii wa nje tofauti na nchi yetu ambayo inashika nafasi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii na watanzania wanaoshiriki katika kufanya utalii wa ndani ni chini ya asilimia mbili(2%).

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KILI BASE ADVENTURES iliyopo Moshi, Kilimanjaro Bw. Sifael Malle alisema kuwa kitendo cha watanzania kufanya utalii wa ndani ni mojawapo ya uzalendo mkubwa sana katika nchi.

Alisema kuwa watanzania wakishiriki katika kufanya utalii wa ndani wanakuwa wazalendo katika nchi yao kwa kuwa kwa kufanya hivyo inachangia mambo mbalimbali na watu waliofanikiwa katika nchi zilizoendelea ni kutokana na kuwa wazalendo katika nchi zao.

"Ni muhimu sana watanzania wakishiriki kufanya utalii wa ndani kwasababu kwa kufanya hivyo ni sehemu ya kutengeneza ajira, ni kuchangia pato la taifa alafu ni burudania ambayo hata kwa imani ni burudani nzuri" Alisema .

Ipo haja kubwa ama umuhimu wa watanzania kuona kuwa suala la kushiriki katika kufanya utalii wa ndani ni faida kubwa sana katika nchi na kwao pia kwa kuwa kwa kufanya hivyo itachangia pato la taifa letu na hivyo kukuza uchumi wa nchi.

Bw. Sifael alisema "Mataifa yaliyo katika bara la Asia yamefanikiwa sana kiuchumi na moja ya vitu vilivyosababisha wafanikiwe sana ni uzalendo wa kushiriki kwenye utalii wa ndani kwahiyo vivutio vya kwao huwa wanavitembelea wao wenyewe kwanza na watu wengine wakivutiwa wanashiriki huwa ni mara chache wao kutegemea watu kutoka mataifa ya nje"

Alisema kuwa licha ya kuwa nchi yetu ina vivutio vingi vya kitalii vya asili lakini inashangza kuona bado mwamko wa watanzania katika kufanya utalii wa ndani bado ni mdogo.

"Licha ya kwamba tuna vivutio vingi na vya kipekee sana vivutio ambavyo ni vya kipekee tulivyojaaliwa na mwenyezimungu na sio vya kutengenezwa lakini bado watanzania hawana hamasa ya kufanya utaili" Alisema bw. Sifael

Wakati umefika sasa kwa watanzania kuwa na hamasa ya kufanya utalii na kuwa wazalendo kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutakuza uchumi wa nchi kwa kujitoea kushiriki katika utalii wa ndani.

Bwana Sifael alisema kuwa katika kipindi cha mwisho wa wiki itapendeza zaidi kama wazazi watawatembeza watoto katika vivutio mfano katika mbuga za wanyama kwa kuwa hii itawasaidia watoto kujifunza na kuwa wazaendo.

Ifahamike kuwa kwa wingi ambao watanzania upo endapo tutajitokeza katika kufanya utalii mbali na kuchangia pato la taifa lakini pia hii itasaidia kuongeza ajira na kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania.

"Unajua kwenye uchumi ni jambo zuri sana kwa kuwa tunakuwa na uhakika na watalii wa ndani na kuwategemea wao kuliko watalii wa nje kwa mfano lilipotokea tukio la ugojwa ule wa ebola kule nchi za magharibi mwa Afrika , watalii waliokuwa wanatoka nchi za bara la Ulaya na Marekani wao wakakatisha safari za kuja huku Tanzania kwa kuhisi kuwa Afrika nzima kuna Ebola" Alisema Bw. Sifael

Aidha alisema kuwa kutokana na tukio hilo kulitokea mtikisiko katika soko la utalii kwa kuwa watalii walipungua kuingia nchini bila kuelewa kuwa zile nchi ambazo zilikubwa na ugonjwa wa ebola zilikuwa mbali sana na Tanzania.

Kwahiyo basi kwa kulitazama hilo kama nchi yetu ingekuwa na utalii wa ndani ulio imara zaidi kwa kipindi hicho soko la utalii lisingetikisika kwa kuwa watanzania wangeshiriki kikamilifu katika kufanya utalii huo.

Bw. Sifael alisema kuwa kutokana na marekebisho yaliyofanyika katika sera ya utalii kwa sasa ni nzuri kwa kuwa gharama ni ndogo kwa watalii wa ndani lakini pia kiwango cha tozo kw watalii wa ndani katika nchi za Afrika mashariki ni kimoja.

"Nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki bei ni sawa katika kuingia mbuga za wanyama na kutembelea mlima Kilimanjaro bei ni moja, kwa hiyo nitumie fursa hii kuwaalika wananchi wa nchi hizi za Afrika Mashariki waje Tanzania kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini" Alisema Bw. Sifael

Inawezekana watanzania walikuwa wanaogopa kutembelea katika vivutio hivyo kwa kuhofia gharama kuwa ni kubwa au kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu masuala ya utalii hivyo basi kwa kupitia makala haya upo umuhimu wa watanzania kufanya utalii wa ndani .

Bw. Sifael alisema kuwa watanzania wengi hawana muamko wa kufanya utalii wa ndani kutokana na kuwa hawajajengewa utamaduni wa kufanya utalii, kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu utalii lakini pia kuwa na dhana ya kuwa suala la kufanya utalii ni kwa ajili ya wazungu tu {wageni kutoka nchi za Magharibi}

Alisema "utamaduni wetu tangu mwanzo haukujengwa kwenye misingi ya starehe za namna hiyo kwamba watu walikuwa hawajajengewa huo utamaduni wa kwenda kutalii kwahiyo tatizo letu kubwa ni utamaduni tuliojengewa"

Kutokana na hilo jamii haina budi kujijengea utamaduni wa kufanya utalii kwa kuwajengea na kuwafundisha watoto juu ya umuhimu wa kufanya utalii wa ndani ikiwemo kuwatembeza katika vivutio hivyo.

Aidha Bw. Sifael ametoa wito kwa serikali kuweka elimu ya kufanya utalii wa ndani kwa wanafunzi katika ngazi zote za elimu kuanzia elimu ya msingi.

"Kwenye mitaala yetu kuwe na somo la kuhamasisha kufanya utalii wa ndanikwa watoto lakini pia kuwe na midahalo y kujenga ufahamu wa watoto zaidi kuhusu masuala ya utalii lakini pia wawe wanatembele katika mbuga hizo na vivutio hivyo" Alisema Bw. Sifael

Kwa kuwa nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii na nchi nyingine zinatamani nafasi hiyo ni jambo zuri sana endapo serikali itaweka somo la utalii katika mitaala shuleni na kutilia mkazo suala hilo.

Bwana Sifaeli alisema kuwa watanzaa hawajachelewa katika kukuza na kuhamasishana katika kufanya utalii wa ndani endapo tutashirikiana kwa pamoja na kutilia mkazo suala la kufanya utalii wa ndani lazim tutaibadilisha hali iliyopo sasa kwa kuongeza idadi ya watalii wa ndani ambao watakuwa ni watnzania wenyewe.

Lakini pia katika kuhamasisha utalii huo kuwepo na mabanda mbalimbali ambayo yatakuwa yanahusik katika kuhamasisha watnzania kufanya utalii wa ndani kwa kuwa watatoa elimu na umuhimu wa kufanya utalii.

Kwa kufanya mambo hayo lazima utalii wa ndani utakuwa na ajira zitaongezeka, pato la taifa litaongezeka na pia hatutategea wageni kutoka nje ya nchi kwa asilimia kubwa kuja kutembelea vivutio vyetu badala yake sisi ndio tutakuwa na asilimia kubwa
 
Back
Top Bottom