Watanzania tuna njaa

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
341
301
Milo mitatu kwa watanzania bado ni changamoto kubwa. Binafsi sina uhakika kila siku kupata milo mitatu kutokana na hali yangu ya kiuchumi. Hali hii inawakumba watanzania ambao walipata uhuru zaidi ya miaka 58 iliyopita.

Kampeni za siasa zimepamba moto kila kona ya nchi.Kila chama cha siasa kinaendelea kunadi sera zake kwa wananchi.Ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa zinagusa matatizo yanayoikabili Tanzania kwa sasa utofauti wao upo kwenye vipaumbele.

Binafsi nimeguswa na kuvutiwa zaidi na sera za chama cha CHAUMMA.Sera ya Mzee wetu Hasheem Rungwe ya kugawa chakula kwa watanzania ni sera inayogusa tatizo kubwa linalowakabili watanzania tulio wengi.

Upatikanaji wa lishe bora ni changamoto kwa watanzania japo wanasiasa wanatumia muda mwingi kuhubiri maendeleo ya vitu zaidi. Sera ya kugawa ubwabwa ni sera ambayo imeeleka kirahisi na kuzua gumnzo kubwa katika mitandao ya kijamii.

Moja ya mahojiano yake aliyofanya na vyombo vya habari amesikika akisema;
“Mapema tu Oktoba tukavyo ingia ikulu swala la kwanza nitaanza na “IJUMAA BIRIYAN HOLIDAY” siku hiyo hakutakua na masomo wala kazi ni biriani kuku asubuhi mpka jioni, litapita mitaa yote ya Tanzania. Ni kwa kila ijumaa kwa maana weekend itaanza ijumaa asubuhi.”

Mzee wetu Rungwe anapolizungumzia swala la lishe kwa watanzania baadhi ya watu wamelichukilia kimzaha na kageuka gumnzo kubwa katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu wanaiona kama ni sera ya kichekesho, lakini kwangu mimi binafsi ni sera yenye hoja na mantiki kubwa kwa jamii ya watanzania. Nampongeza sana Mzee wetu Hasheem Rungwe kwa kulisemea tatizo la njaa kwani wanasiasa wengi hawajaliona kama ni tatizo.

Mzee wetu Hasheem Rungwe anaposema “Watoto wenu wana njaa, wanakwenda shule hawaelewi kitu sababu ya njaa, nitahakikisha wanapata ubwabwa, mimi nimewahi kulazwa hospitali moja hapa Dar es Salaam ila nikaondoka kisa njaa, hamna chakula Hospitali, kote nitapeleka ubwabwa”- maneno hayo aliyasema Manzese kwenye mkutano wake wa siasa.

Maneno yake yana ukweli mtupu ndani yake. Watanzania tulio wengi bado lishe bora ni changamoto kubwa kwetu.Tatizo hili limekita mizizi na kuwaathiri zaidi watoto wa kitanzania wanaosoma shule za msingi na sekondari.

Ukweli ni kwamba bado watoto wetu wanashinda na njaa wawapo mashuleni.
Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi wakati wa mchana ilitupasa turudi nyumbani tupate chakula cha mchana na turudi tena shuleni kuendelee na masomo. Umbali kutoka nyumbani nilipokuwa naishi hadi shuleni ni 2km na kuna ambao walikuwa wanatoka mbali zaidi ya hapo.

Kuna nyakati unafika nyumbani na unakuta wazazi bado hajaanda chakula na inakugharimu urudi shuleni na njaa. Hali ile ya njaa iliniletea unyonge na kulala darasani wakati walimu wakiwa wanafundisha masomo ya mchana.

Historia yangu ni ya miaka kumi na tatu iliyopita kwani nilihitimu darasa la saba mwaka 20007. Nasikitika kuona bado mambo hayajabadilika na kuna wanafunzi wengi wa shule za msingi nchini Tanzania wanaoshinda na njaa.

Repoti ya utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Uwezo Tananzia, ARE OUR CHILDREN LEARNING ? Uwezo Tanzania Learning Assement Report 2019 inasema kwamba “Results from the Uwezo 2017 assessment reveal that, nationally, only 23.4% of primary schools in Tanzania provide children with meals.”

Ikimaanisha kwa ngazi ya kitaifa ni asilimia 23.4% kwa shule za msingi nchini Tanzania ndizo zinatoa chakula cha mchana hizo ni takwimu zilizokusanywa mwaka 2017. Nawashukuru sana Uwezo kwa kulionyesha tatizo hili kisayansi.

Kukosekana kwa chakula mashuleni kunapelekea utoro na ufaulu duni kwa watoto wetu. Vilevile watoto wetu wawapo darasani hushindwa kuwasikiliza kwa umakini walimu wanapokuwa wanafundisha. Matokeo yake ni kushuka kwa ubora wa elimu nchini kwetu.

Namshukuru tena Mzee wetu Hasheem Rungwe kwa kutukumbusha kuwa taifa linahitaji sera ya kugawa chakula bure kwa shule zote za msingi na sekondari. Kama tulivyoweza kuanzisha sera ya elimu bure tunahitaji hatua nyingine ya chakula bure mashuleni.

Naongea hivi kwa sababu wazazi wengi wanashindwa kuchangia michango ya chakula mashuleni kwa sababu ya hali zao duni za kipato. Vilevile kuna tofauti kubwa kati ya mkoa mmoja na mwingine kiuchumi na uelewa wa mambo ya elimu hivyo basi jukumu hili linapaswa lile la serikali kuu.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba watanzania tunao maadui watatu ujinga, umaskini na maradhi. Itoshe kusema kwamba umaskini unapelekea ujinga na maradhi.Taifa litaweza kuutokomeza umaskini ikiwa tuu watu wake wana nguzu za kufanya kazi na nguvu huja kwa kupata lishe bora.

Mwisho
 
Spunda mzugaji tu.

Hiyo Ijumaa biriani holiday nchi iache uzalishaji Ijumaa kula biriani, kwa bajeti gani? Hapo tutapoteza productivity kiasi gani?

I am sorry to say this.

Hili ni suala muhimu sana, na linafaa kujadiliwa kwa umakini.

Rungwe anavyofanya kampeni ni kama anafanya mzaha.
 
Ndugu simpigie kampeni ila nampongeza kwa kuibua hoja yenye mantiki na tija kwa watanzania.

Nadhani taifa linahitaji kuliangalia hili swala la lishe bora kwa watanzania kwa upana kwa ni bado kuna watoto wengi hapa nchini Tanzania wenye utapia mlo

Nadhani inatupasa wote kuliangalia kwa upana swala hili na sio wanasiasa peke yao.

Nashukuru sana ndugu kwa maoni yako
 
Milo mitatu kwa watanzania bado ni changamoto kubwa. Binafsi sina uhakika kila siku kupata milo mitatu kutokana na hali yangu ya kiuchumi. Hali hii inawakumba watanzania ambao walipata uhuru zaidi ya miaka 58 iliyopita.

Kampeni za siasa zimepamba moto kila kona ya nchi.Kila chama cha siasa kinaendelea kunadi sera zake kwa wananchi.Ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa zinagusa matatizo yanayoikabili Tanzania kwa sasa utofauti wao upo kwenye vipaumbele.

Binafsi nimeguswa na kuvutiwa zaidi na sera za chama cha CHAUMMA.Sera ya Mzee wetu Hasheem Rungwe ya kugawa chakula kwa watanzania ni sera inayogusa tatizo kubwa linalowakabili watanzania tulio wengi.

Upatikanaji wa lishe bora ni changamoto kwa watanzania japo wanasiasa wanatumia muda mwingi kuhubiri maendeleo ya vitu zaidi. Sera ya kugawa ubwabwa ni sera ambayo imeeleka kirahisi na kuzua gumnzo kubwa katika mitandao ya kijamii.

Moja ya mahojiano yake aliyofanya na vyombo vya habari amesikika akisema;
“Mapema tu Oktoba tukavyo ingia ikulu swala la kwanza nitaanza na “IJUMAA BIRIYAN HOLIDAY” siku hiyo hakutakua na masomo wala kazi ni biriani kuku asubuhi mpka jioni, litapita mitaa yote ya Tanzania. Ni kwa kila ijumaa kwa maana weekend itaanza ijumaa asubuhi.”

Mzee wetu Rungwe anapolizungumzia swala la lishe kwa watanzania baadhi ya watu wamelichukilia kimzaha na kageuka gumnzo kubwa katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu wanaiona kama ni sera ya kichekesho, lakini kwangu mimi binafsi ni sera yenye hoja na mantiki kubwa kwa jamii ya watanzania. Nampongeza sana Mzee wetu Hasheem Rungwe kwa kulisemea tatizo la njaa kwani wanasiasa wengi hawajaliona kama ni tatizo.

Mzee wetu Hasheem Rungwe anaposema “Watoto wenu wana njaa, wanakwenda shule hawaelewi kitu sababu ya njaa, nitahakikisha wanapata ubwabwa, mimi nimewahi kulazwa hospitali moja hapa Dar es Salaam ila nikaondoka kisa njaa, hamna chakula Hospitali, kote nitapeleka ubwabwa”- maneno hayo aliyasema Manzese kwenye mkutano wake wa siasa.

Maneno yake yana ukweli mtupu ndani yake. Watanzania tulio wengi bado lishe bora ni changamoto kubwa kwetu.Tatizo hili limekita mizizi na kuwaathiri zaidi watoto wa kitanzania wanaosoma shule za msingi na sekondari.

Ukweli ni kwamba bado watoto wetu wanashinda na njaa wawapo mashuleni.
Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi wakati wa mchana ilitupasa turudi nyumbani tupate chakula cha mchana na turudi tena shuleni kuendelee na masomo. Umbali kutoka nyumbani nilipokuwa naishi hadi shuleni ni 2km na kuna ambao walikuwa wanatoka mbali zaidi ya hapo.

Kuna nyakati unafika nyumbani na unakuta wazazi bado hajaanda chakula na inakugharimu urudi shuleni na njaa. Hali ile ya njaa iliniletea unyonge na kulala darasani wakati walimu wakiwa wanafundisha masomo ya mchana.

Historia yangu ni ya miaka kumi na tatu iliyopita kwani nilihitimu darasa la saba mwaka 20007. Nasikitika kuona bado mambo hayajabadilika na kuna wanafunzi wengi wa shule za msingi nchini Tanzania wanaoshinda na njaa.

Repoti ya utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Uwezo Tananzia, ARE OUR CHILDREN LEARNING ? Uwezo Tanzania Learning Assement Report 2019 inasema kwamba “Results from the Uwezo 2017 assessment reveal that, nationally, only 23.4% of primary schools in Tanzania provide children with meals.”

Ikimaanisha kwa ngazi ya kitaifa ni asilimia 23.4% kwa shule za msingi nchini Tanzania ndizo zinatoa chakula cha mchana hizo ni takwimu zilizokusanywa mwaka 2017. Nawashukuru sana Uwezo kwa kulionyesha tatizo hili kisayansi.

Kukosekana kwa chakula mashuleni kunapelekea utoro na ufaulu duni kwa watoto wetu. Vilevile watoto wetu wawapo darasani hushindwa kuwasikiliza kwa umakini walimu wanapokuwa wanafundisha. Matokeo yake ni kushuka kwa ubora wa elimu nchini kwetu.

Namshukuru tena Mzee wetu Hasheem Rungwe kwa kutukumbusha kuwa taifa linahitaji sera ya kugawa chakula bure kwa shule zote za msingi na sekondari. Kama tulivyoweza kuanzisha sera ya elimu bure tunahitaji hatua nyingine ya chakula bure mashuleni.

Naongea hivi kwa sababu wazazi wengi wanashindwa kuchangia michango ya chakula mashuleni kwa sababu ya hali zao duni za kipato. Vilevile kuna tofauti kubwa kati ya mkoa mmoja na mwingine kiuchumi na uelewa wa mambo ya elimu hivyo basi jukumu hili linapaswa lile la serikali kuu.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba watanzania tunao maadui watatu ujinga, umaskini na maradhi. Itoshe kusema kwamba umaskini unapelekea ujinga na maradhi.Taifa litaweza kuutokomeza umaskini ikiwa tuu watu wake wana nguzu za kufanya kazi na nguvu huja kwa kupata lishe bora.

Mwisho
Huwezikuwa na njaa ukaandika maneno yote hayo
Kuna vibarua vya ujenzi kwenye mabarabara na madaraja nenda kafanye kazi.
 
Back
Top Bottom